Majibu ya madaktari yamegongana nifanyeje?

MR. MORRIS T. J.

JF-Expert Member
Apr 18, 2013
1,167
402
Mzee wangu anatibiwa katika hospital moja jina naomba nisilitaje kwa usalama wa mgonjwa.kapiga CT I.V.U Majibu Yakatoka Tukayapeleka Kwa Specialist Wa Matatizo Ya Figo.Huyu Akasema Kwenye Figo Hakuna Tatizo Ila Kwenye Ureta Ya Mkojo Kuna kauvimbe,akasema Tumuone Specialist Wa Vibofu Vya Mkojo.

Tukamuona Huyo Wa Vibofu,majibu Ya Mtaalam Wa Vibofu Kasema Figo Imekufa.Sasa Dr Wa Figo Yeye Kasema Figo Inafanya Kazi Na Akasema Tatizo Hl Halimhusu,akatuelekeza Kwa Daktari Wa Vibofu Na Mfumo Wa Ukojoaj,majibu Ya Huyu Kasema Figo Imekufa Na Iondolewe.

Na Wote Ni Madaktari Wapo Hosp Moja.Na Wote Ni Madaktar Bingwa,SASA NIFANYEJE? Ni Figo Imekufa Au Ni Uvimbe Wa Kwenye Ureta? Figo Yenyewe Imejaa Maji.Kwa Mujibu Wa Dk Wa Figo.

Naombeni Ushauri.
 
Kwanza pole kwa Mzee wetu na kwako pia. Mimi si daktari lakini najua tatizo hilo huwapata wazee wengi na huwa ni gumu sana kwa madaktari. Ushauri kama inawezekana wangeshirikiana wote pamoja na wengine wanaoweza saidia wao madaktari wanajuana. Tafuta namna nzuri ya kuongea nao, wengine huwa hawapendi sana ushauri,(sijui kwa nini). Tuombe madaktari wapitie hapa wao wao watakua na ushauri mzuri zaidi!
 
mtaalam wa vibofu anasema figo immekufa wakati mtaala wa figo anasema figo nzima. hapo tafuta daktari wa 3,4,5 sikia wanasemaje, pia wakuonyeshe picha za uchunguzi
 
mzee wangu anatibiwa katika hospital moja.jina naomba nisilitaje kwa usalama wa mgonjwa.kapi CT I.V.U Majibu Yakatoka Tukayapeleka Kwa Specialist Wa Matatizo Ya Figo.Huyu Akasema Kwenye Figo Hakuna Tatizo Ila Kwenye Ureta Ya Mkojo Kunakauvimbe,akasema Tumuone Specialist Wa Vibofu Vya Mkojo. Tukamuona Huyo Wa Vibofu,majibu Ya Mtaalam Wa Vibofu Kasema Figo Imekufa.Sasa Dr Wa Figo Yeye Kasema Figo Inafanya Kazi Na Akasema Tatizo Hl Halimhusu,akatuelekeza Kwa Daktari Wa Vibofu Na Mfumo Wa Ukojoaj,majibu Ya Huyu Kasema Figo Imekufa Na Iondolewe. Na Wote Ni Madaktari Wapo Hosp Moja.Na Wote Ni Madaktar Bingwa,SASA NIFANYEJE? Ni Figo Imekufa Au Ni Uvimbe Wa Kwenye Ureta? Figo Yenyewe Imejaa Maji.Kwa Mujibu Wa Dk Wa Figo. Naombeni Ushauri.

Rudi kwa dokta wa figo na majibu yako.
 
Pole sana mkuu!! kwa tatizo la mzee wetu.

lakn mimi nilikuwa nakuomba ujaribu kuwakutanisha madaktari wote na uwaelezee, ikiwazekana washirikiane kutatua tatizo la mzee wetu kama inawezekana
 
Kama alifanya ct na ivu ambavyo ni vipimo vinavyoweza kuangalia vizuri soft tissue zinavyooneka probably the vivimbe vinaweza onekana, lakin alibidi afanyiwe vipimo vya damu ambavyo vingetuonyesha hali za figo zinaendaje. Lakini cha msingi mzee wako ulimpeleka hospitalini akiwa anasumbuliwa na tatizo gani?
 
kwanza nawashukuruni sana ndugu zangu, ushauri wenu wa kuuliza kwa madaktari wengine nimeshaanza kuufanyia kazi, nipo njiani kwenda hosptal zingine kuomba kuonana na madaktari wengine.
 
Kama alifanya ct na ivu ambavyo ni vipimo vinavyoweza kuangalia vizuri soft tissue zinavyooneka probably the vivimbe vinaweza onekana, lakin alibidi afanyiwe vipimo vya damu ambavyo vingetuonyesha hali za figo zinaendaje. Lakini cha msingi mzee wako ulimpeleka hospitalini akiwa anasumbuliwa na tatizo gani?

anadai tumbo linamuuma.upande wa kulia.ambapo daktari wa figo akasema imejaa maji kwani kwenye ureta kuna uvimbe mkojo unashindwa kupita vzr. dokta akasema figo ni nzima ila imejaa maji.akasema tumuone wa vibofu wa vibofu.nae kasema figo haifanyi kazi ni ya kutolewa.pengine kama kuna daktari naweza nikaonana.
 
Kuna maswal mengine waweza kuuliza, je mkoja wake unatoka kawaida nkimanisha kama hatumii nguvu nyingi wakati wa kukojoa, vipi maumivu wakati wa kukojoa, kiwango cha mkojo unaotoka,kuvimba uso, tumbo au mwili mzima, eneo ambambapo anasikilizia hayo maumivu na huyo hali ipo kwa muda gani? Kwa majibu ya hapo pamoja na vipimo tunaweza kujua pa kwenda
 
Umri Miaka 64, Mkojo Unatoka Kidogo Kidogo,hajisikii Maumivu Wakati Wa Kukojoa Ila Mkojo Anatumia Nguvu, Hajavimba Sehemu Yoyote Ile,maumivu Anasikia Upande Wa Kulia Mwa Tumbo Lake Lakini Kwa Sasa Maumivu Anasikia Kwenye Kiuno Hasa Anapotembea Kwenda Uwani.
 
Pamoja na maelezo yako ni vizuri kama ungeambatanisha majibu ya vipimo, ikiwa ni maandishi/tarakimu/picha.. bila jina la mgonjwa, hospitali ili kupata msaada zaidi.
 
CONCLUSION; RIGHT SEVERE HYDRONEPHROSIS AND HYROURETER TO THE PELVIC CAVITY PROMINENT CALCIFICATION WITHIN THE REGION OF URETERIC OBSTRUCTION SUGGEST GRANULOTOUS INFECTION AS OBSTRUCTION EXPOSURE. CT IVU IMAGES REVEAL. Right Severe Hydronephrosis Noted.There Is No Reserved Function Of The Cortex Seen Post Contrast.It Is Associated With Mega Ureter With Urine Hold At The Level Of Pelvis.Within The Pelvis At The Level Of Ureteric Obstruction Appear Prominet Calcification .Soft Tissue Around Appear With Fat Stranding.The Left Kidney Appear Normal In Size And Function] Prostate Appear Prominent Measuring 50gm=BPH Liver Appear Normal In Size And Attenuation.There Is No Parenchyma Lesion Seen. Pancreas And Spleen Appear Normal.
 
Mr. MORRIS T.J,

Kwa majibu hayo(ingawa hakuna picha/image) Naamini ulionana na Nephrologist(daktari bingwa wa figo) ambaye baada ya kuona majibu alikutuma kwa daktari wa mfumo wa mkojo na viungo vya uzazi vya kiume Urologist), sasa basi endapo majibu ni sahihi.

Nephrologist hana/hatakuwa na msaada sana(atakushauri upime ufanyaji kazi wa figo kuangalia, kipimo/vipimo vya Serum Creatinine na Urea)...vipimo hivi pia vinahitajika kabla ya kuonana na Urologist.

Urologist, anaweza kufanya upasuaji kutokana na uvimbe husika ulioonekana, lakini ni vizuri kufanya kipimo kingine, kuangalia/kurudia tena. Endapo kujaa kwa mirija na figo vitakuwa vinasababishwa na uvimbe/pengine uvimbe unaoongezeka muhimu kupata ufafanuzi kutoka kwa Urologist mwingine.
 
Last edited by a moderator:
CONCLUSION; RIGHT SEVERE HYDRONEPHROSIS AND HYROURETER TO THE PELVIC CAVITY PROMINENT CALCIFICATION WITHIN THE REGION OF URETERIC OBSTRUCTION SUGGEST GRANULOTOUS INFECTION AS OBSTRUCTION EXPOSURE. CT IVU IMAGES REVEAL. Right Severe Hydronephrosis Noted.There Is No Reserved Function Of The Cortex Seen Post Contrast.It Is Associated With Mega Ureter With Urine Hold At The Level Of Pelvis.Within The Pelvis At The Level Of Ureteric Obstruction Appear Prominet Calcification .Soft Tissue Around Appear With Fat Stranding.The Left Kidney Appear Normal In Size And Function] Prostate Appear Prominent Measuring 50gm=BPH Liver Appear Normal In Size And Attenuation.There Is No Parenchyma Lesion Seen. Pancreas And Spleen Appear Normal.

Inaelekea figo kweli ni nzima ila sasa hiyo Calcification ndio inaweza kuwa imesababisha yote haya, endelea na uchunguzi hasa ni vizuri kama watachukua Biopsy kutoka kwenye hiyo Calcification na majibu yake yatatoa mwanga wa matibabu, KCMC na Muhimbili ni wazuri sana kwa magonjwa kama haya ..Au kamwone Dr Mbwambo private Hospital (Moshi) na ni mzuri sana kwa mikojomikojo
 
Kwa Dar Nimuone Dokta Nani? Maana Tunaishi Dar
 
Back
Top Bottom