Kuna umuhimu wa kuwapima akili wote waliopewa dhamana ya kutoa leseni, na baadae wapimwe akili wanaoomba leseni.
Utakuta dereva wa daladala au mara nyingine hata wa basi kubwa la mkoani anaendesha akiwa rafu rafu kuanzia mavazi hadi usafi wa mwili (hajachana nywele, hajapiga mswaki). Hizi ni dalili za awali kuwa huyu ni mtu wa hovyo, na bila shaka uhuni wake hautaishia kwenye kuvalia suruali matakoni, bali utaendelea hadi kwenye uendeshaji wake na matumizi mengine ya barabara...lkn utashangaa ana leseni Class C
Aliyemfundisha darasani, na aliyempa leseni wanafahamu kuwa dereva ni zaidi ya kunyonga usukani?