Jamaa alisoma Project Management akamaliza University akakaa miaka miwili bila kazi. Akaamua kurudi chuo kusoma Diploma ya Lab Technology. Amemaliza anasubiria kazi, amepata kazi kwenye kozi ile ya kwanza aliyomaliza miaka kadhaa iliyopita. Maisha yanahitaji uvumilivu.
Ndio ubaya wa kutafuta elimu kwa nia ya kuajiriwa. Wengine wasioajiriwa baada ya digrii ya kwanza, wanaunganisha Master, wakidhani Master itawafanya competitive kwenye ajira. Watu hata kujitolea kidogo au kuomba internship hawataki.