Maisha yanachosha sana

Sio rahisi kihivyo au kila mtu mwenye ideas angekuwa millionaire.

Kwa africa haya mambo ni 40% reality na 60% fantasy.
Sio kila idea inaweza kutengeneza value
Njia ya kwanza ni kutambua fursa kwa kutambua wapi kuna malalamiko?,kivipi unaweza rahisisha kazi au maisha?,kivipi utafanya watu waburudike?,

Ungeelewa nini maana ya neno "value" ingekua rahisi

Halafu kuwa na idea ni jambo moja,na kulikamilisha na jambo jingine
 
Naona kuna logic
 
Tough Times Never Last But Tough People Do.
In any situation try to be positive rather than to be negative. Then keep you faith in God and Never Give Up. Finally Success will follow. Always try to remember this "Life isn't as nice as you want." Be blessed and the love of God be with you. Amen
 
Jifunze kufurahi kwa kidogo kinachopatikana, vikubwa vinapatikana japo jasho likutoke kwelikweli,

Usisahau katika hustle zako "dunia haina huruma"
 
Mleta uzi umeandika ukiwa n uchungu mwingi na kukata tamaa. Pole sana Pambana kidogo utakachopata ndio halali yako, ikibidi hama ulipo hamia pengine ili isikuwie vigumu kufanikisha.

Ila kusema kweli Kama hufanikiwi Maisha yanachosha wakati mwingine,japo hatutakiwi kukata tamaa!!
 
Ungeelewa nini maana ya neno "value" ingekua rahisi
Naelewa.
Halafu kuwa na idea ni jambo moja,na kulikamilisha na jambo jingine
Utekelezaji wa Idea unahitaji supportive environment ili idea iweze perform inavyotakiwa.

Huku africa unaweza ukawa na idea itakayoleta faida kwako na kwa jamii nzima ila mazingira yatakuangusha hata kama uwezo wa kutekeleza idea yako upo.

Ila kwa idea hiyohiyo ukiwa marekani ingeweza perform vilivyo kutokana na mazingira yake yalivyo'supportive.

Mazingira ya tanzania kwa asilimia kubwa siyo supportive kwa mafanikio wanayoota vijana wengi.
 
Nikwambie tu pesa kubwa inaletwa na pesa ndogo. Weka vyeti ndani Piga kazi yoyote mkuu wewe kajichanganye stand kuu hapo ulipo unga unga.

Huko ndiko utakutana na connection, amini utavyopiga izo dili wewe ni tofauti sana na darasa la 7.

Kumbuka pesa ndogo ndio inaleta pesa kubwa. Komaa
 
Sio rahisi kihivyo au kila mtu mwenye ideas angekuwa millionaire.

Kwa africa haya mambo ni 40% reality na 60% fantasy.

40% ni kubwa sana shusha shusha hadi 10% reality mkuu alafu 90% fantasy. Haya mambo sio rahisi kutekelezeka kabisaaa. Na ukweli mchungu ni kuwa PESA INAFUATA PESA ILIPO

Ukiwa na idea inatakiwa uwe na pesa yakukufikisha kwa hao utakaowapa iyo idea wakusapoti, lazima uwe na pesa ya kununua kahawa kikombe 6,000 restauranti ili udiscuss idea na vibopa vibopa hawakai kijiweni wana maeneo yao

Sasa watu wengi huu ukweli hawaambiwi wanabaki kukariri tu ooh ukiwa na idea ukipelekea watu utapewa pesa, nani kasemaaa!!?
 
Hiyo ni dhana potofu.

Maisha hayana muda, Maisha hayana wakati.

Maisha hayana mwenyewe.

Maisha hayana ujanja.

Maisha hayana mjanja, Maisha hayana FALA.

Maisha hayana mkubwa, Maisha hayana mdogo.

Maisha hayana kanuni.

Maisha yanabadilika muda wowote.

Wewe endelea kupambana, mambo yatajipa.

Achana na kufikiria Maisha ya watu, wewe ishi Maisha yako.

Jiamini, usikate tamaa.

Utafikia Malengo yako
 
Yaani unawaza wakati umelala unaangalia juu yaa paa la chumba chako,wakati unaowawazia wanapiga kazi kwenye jua kali pole sana mtoto wa mama kama hata kubeba zege huwezi huku ukijivunia elimu yako inayokudanganya
 
Ni kweli yanachosha lakini ni ajabu sana ! Hapo hapo katika Hali uliyonayo wewe ni mwenye nguvu Sana Kama unaweza kuamka asubuhi na kwenda kuchukua carton ya maji kuuza kwa abiria wanaopita barabarani kwenye mabasi.
Wengine hawawezi kwakuwa wanasumbuliwa na matatizo mbali mbali ya kiafya na hawawezi. Kikubwa aliyenacho asimsahau kabisa asiye nacho na mwenye afya azidi kuombea wenye magonjwa wapone na kuwapa faraja.

Kunawakati tunapitia kwenye magumu sio kwamba tutakuwa kwenye magumu hayo daima la. Ni ili tunapofanikiwa tujue hisia za wale walio katika magumu ambayo nasi tuliyapitia na tuwe sehemu ya msaada kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…