Maisha ya ndoa na changamoto hii

August_Shao

Senior Member
Joined
Nov 23, 2007
Posts
166
Reaction score
49
Kuna hili jambo naombeni msaada wenu:

MWANAUME:

Umeo na unaishi na mkeo katika ndoa na mnawatoto wazuri. Inatokea kwa bahati mbaya Mkeo anasafiri na kupatwa na Ajali mbaya sana ambapo katika ajali hiyo imetangazwa hakuna aliyopona, mbaya zaidi mwili wa marehemu mkeo haujapata kuona pia, na mkeo kweli haonekani, familia mnakaa na kuamua kuwa kweli mkeo amekufa na pengine amezikwa na JIJI, inapita miaka mingi kama 10 vile na unaamua kuoa mke mwingine na kuzaa watoto. Inatokea kwa Maajabu ya Mwenyezi Mungu Mkeo wa kwanza ambaye alipata ajali Anarudi Nyumbani.

SWALI: kwa waumini Wakristo na Wakiisilamu ni yupi hapa kati ya Wanawake hawa Wawili ni Mkeo wa halali na ikiwa umefunga ndoa zote hizo kihalali?

MWANAMKE:

Umeolewa na unaishi na mumeo katika ndoa na mnawatoto wazuri. Inatokea kwa bahati mbaya Mumeo anasafiri na kupatwa na Ajali mbaya sana ambapo katika ajali hiyo imetangazwa hakuna aliyopona, mbaya zaidi mwili wa marehemu Mumeo haujapata kuona pia, na Mumeo kweli haonekani, familia mnakaa na kuamua kuwa kweli Mumeo amekufa na pengine amezikwa na JIJI, inapita miaka mingi kama 10 vile na unaamua kuolewa na Mume mwingine na kuzaa watoto. Inatokea kwa Maajabu ya Mwenyezi Mungu Mumeo wa kwanza ambaye alipata ajali Anarudi Nyumbani.

SWALI: kwa waumini Wakristo na Wakiisilamu ni yupi hapa kati ya Wanaume hawa Wawili ni Mumeo wa halali na ikiwa umefunga ndoa zote hizo kihalali?
 
wote ni wake zako kihalali.......maana ndoa ni agano.......swala gumu ni kuishi nao wote,hapo ndo kimbembe
 
Mimi nisingesubiri mpaka miaka 10.:behindsofa::bange::bange::bange::behindsofa:
 
Hakuna maajabu ya namna hii. Labda uniambie hawakua ktk hiyo ajali bali ndugu walihisi tu. Sasa kama hawakuwemo kwenye hiyo ajali ni kwamba watakaporudi home itabidi huyo mke/mme ajieleze alikua wapi na kwa nini hakuwahi kuwasiliana na nyumbani. Mke/mume halali ni yule ulie nae kwa sasa kwa vile huyo wa kwanza si mwaminifu na hana ubinadamu alishindwaje kuwasiliana na wewe kwa kipindi choooote hicho na alikua wapi huko kusikokua na mawasiliano.
 
sasa hiyo miaka kumi yote alikuwa wapi?
 
Ningoje tutoke wote. Miaka 10 alikuwa kwenye coma kwa mganga wa kienyeji ama?
Samahani shosti kwa kukuacha mi nilishasepa kuona mambo ya if....ila nakupitia twenzetu hapa naona pameshindikana kukaa.
 
we unasema miaka kumi'? Mingi ivyo, mwaka tu navuta mzigo mpyaaa, akirudi sijui itakuwaje
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…