Tunachochagua kwa akili zetu ni kukubali au kukataa njia fulani hapo tu basi, ila baada ya kukubali njia husika matokeo ya kukubali hupangi wewe ni hatma itaamua, na ukikataa pia vivyohivyo, matokeo baada ya kukutaa hujipangii wewe, ni sawa na form six leaver anayejaribu kuchagua course ya kusoma chuo, uhuru huwa anao kabla ya kuchagua, ila akiishachagua, matokeo ya uchaguzi hapangi yeye ni hatma itaamua,labda tuseme akachagua kusoma Sheria, hawezi tena kusema kupitia hii course ya Sheria nitakuja kuwa Daktari mzuri sana, hapo hachagui tena ila hupata matokeo kulingana na uchaguzi wa awali, yaani atakuwa tu mwanasheria maadamu ndicho alichochagua, mpaka labda akatishe masomo hayo, au aende mpaka mwisho, akiwa huru tena afanye maamuzi mengi labda tuseme akasome udaktari baada ya kumaliza au kukatisha masomo yake ya sheria, na akichagua udaktari hawezi sema kupitia udaktari huu nitakuja kuwa engineer mkubwa baadae ni kitu kisichowezekana, uhuru tulionao wanadamu ni katika kufanya maamuzi tu yaani kukubali au kukataa jambo, lakini ukishalikubali au kulikataa matokeo yake huamui wewe yaweje, ni hatma itaamua kulingana na ulivyochagua.