Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 5,175
- 10,484
Imam Hussein alikuwa ni mjukuu wa Mtume Muhammad s.a.w: Alikuwa na ndugu yake mwengine akiitwa Hassan.Hivi huyu Imamu Hussein alikuwa na wadhifa gani? Aliuawa na kina nani? Na kwanini?
Baada ya Makhalifa 4 tangu alipofariki Mtume yaani kuanzia Abuu Bakr, Umar, Uthman na Ally. Kulitokea mvurugano wa madaraka na vuguvugu lilianza baada ya kuuliwa Umar. Baadaye akauliwa na Uthman baadaye akauliwa Ally. Hao wote ni Maswahaba wa Mtume waliyoishi na Mtume.
Umar aliuliwa na Abuu Lulu. Abuu Lulu alikuwa ni muajemi, ni mateka wa vita na alikuwa ni Juusi. Juusi ni watu wanaoabudu moto. Alikuwa ni mtengeneza jambia, silaha ya vita. Alimuua Umar wakati Umar akisalisha Waislam. Sababu ya kumuua alikwenda kuomba kitu kwa Umar akamwambia kuwa kuwa mwenye kusubiri, kuwa mvumilivu. Akamvizia akampiga jambia.
Uthman aliuliwa na waasi wakati amekaa nyumbani kwake akisoma Quran. Ally aliuuliwa Iraq na kama sijakosea ni mji wa Kufa. Aliuliwa na jamaa anayeitwa Abdulrahman ibn Muljuk, alimpiga panga Ally kipindi Ally anakwenda kusali. Ally ndiye baba mzazi wa Hassan na Hussein. Ambao ndiyo vijukuu vya Mtume.
Kipindi cha utawala cha Yaziid Ibn Munawia wakazi wa Kufa nchi ya Iraq walituma ujumbe kwa Imam Hussein kuwa hawamtaki yeyote uwatawale na awaongoze kwa maslahi ya Dini isipokuwa mjukuu wa Mtume. Hizo taarifa hazikutumwa mara 1 bali zilitumwa mara nyingi. Imam Hussein akamtuma ndugu yake kwa jina Muslim Ibn Aqiiy kwenda kuangalia mazingira kama yanayosemwa ni ya kweli.
Nia ya Imam Hussein haikuwa ni madaraka! Bali ni kutaka kusamamisha haki. Muslim Ibn Aqiiy alivyofika Kufa Iraq akaona kweli wanachokitaka watu ni mjukuu wa Mtume. Akamtumia barua Imam Hussein Madina na barua ikisema; walichodhmiria ni sahihi na wanakuhitaji wewe Hussein, na huku Kufa kuna jeshi la watu 30,000 wamejitolea kukulinda.
Imam baada ya kupata barua akataka kufunga safari lakini Maswahaba wa Mtume wakamnasihi. Wakamwambia Hussein kama unataka kuhama ni bora ukahamie Makkah. Huko patakufaa lakini siyo Iraq. Kwani iraq ni karibu na Sham(Syria ya zamani) na Sham kuna Yaziid Ibn Munawia ambaye yeye ndiye mtawala wa huko. Licha ya hivyo, Maswahaba wakamnasihi kumwambia, huko unapotaka kuelekea Kufa ambapo ni Iraq ndipo alipouliwa baba yako ewe Hussein. Na walimpa tabu baba yako mpakq alitamani kufa. Na wakamwambia kama wanakutaka wewe uwe kiongozi wao basi kwanza hao wakazi wa Kufa wamuondoe kiongozi wao wa huko. Miongoni mwa Maswahaba waliyomnasihi ni Abdallah Ibn Abbas, Abdullahi Ibn Umar na wengineo. Lakin Imam Hussein akasema anataka kuiweka haki mahala pake. Kwa hiyo akafunga safari.
Akatoka na baadhi familia yake pamoja na baadhi ya watoto wa ndugu yake Hassan. Maswahaba wakamsihi. Wakamwambia hapana! Wakamwambia tunafahamu kwamba umedhamiria kutoka lakini tunakushauri uwaache nduguzo kwa hiyo safari uliyodhamiria. Lakini Hussein alifunga msafara nao wale aliyodhamiria nao. Wakati wapo njiani kuelekea Kufa mji uliyopo Iraq, lile jeshi la watu 30,000 lilikula kiapo kumlinda Imam Hussein likaanza kupungua. Viongozi wa makabila wakapewa hongo wakahongeka na hakukuwa tena na Jeshi.
Kazi hiyo ilifanywa na gavana wa hilo jimbo aliyeitwa Inb Ziyad. Muslim Ibn Aqiiy aliyetuma akaangalie mazingira ya Kufa na Hussein akabaki peke yake. Akauliwa. Imam Hussein alipokuwa njiani kuelekea Kufa njiani akakutana na mshairi. Akamuuliza vipi huko Kufa! Mshairi akamjibu, habari za huko siyo njema. Miooyo yao ipo pamoja na wewe na panga zao zipo juu ya shingo yako, na Mungu ndiye mwenye kuhukumu na anafanya anachotaka.
Alipokuwa njiani kuelekea Kufa Imam Hussein akakutana na sehemu ndogo la jeshi la Gavana wa huko ambaye alitumwa kutizama mazingira kuhusu Hussein. Kiongozi wa hilo Jeshi alikuwa Al hurru Ibn Yazzid. Akamuuliza Hussein unakwenda wapi? Hussein akajibu anaelekea Kufa. Al Hurru Ibn Yaziid akamwambia huko unakoelekea sijaacha heri ya namna yoyote kuhusu wewe, na Al Hurru ibn Yaziid jeshi lake lilikuwa la watu 40, akamwambia nakushauri urudi.
Imam Hussein akasogea nyuma kidogo. Alipofikia akauliza ardhi hii inaitwaje? Wakamjibu Karbulaa. Baada ya kujibiwa hivyo Hussein akasema, Karbun wa balaa, akimaanisha majanga na dhiki. Alipulizwa kwa nini unasema hivyo? Akasema nimemuota Mtume. Wakamuuliza amekuambia nini? Akajibu siwezi kutoa siri ya nilichoambiwa.
Kwa ghafla! Likaja jeshi jengine la Gavana! Akaongeza wanajeshi likawa jeshi la watu 5000 likamfuata Hussein nao wakamwambia Hussein arudi alipotoka na wakamuweka akawa kizuizini. Hussein akawaambia nawaomba mniwasilishie masuala 3 kwa kiongozi wenu. Suala la kwanza alilowaomba Wamuache arudi nyumbani alipotoka, 2. Kama la kwanza haliwezekani basi wamuache akakutane na mtawala wa Sham Yazid ibn Muawia. Kama hayo yote hawayataki wamuache aende mahala popote kwenye kambi za waislam aendeleze masuala ya Dini.
Maombi yalipomfikia mtawala(Gavana) Ibn Ziyaad akasema mpeni anachotaka. Pembeni alikuwa mshauri jina lake ni Shamra Ibn Jawshan.Akamwambia Gavana tangu lini mateka akawaa anasema ni nini cha kufanywa. Gavana akamwambia nenda na mumkamate Hussain. Hiyo amri ukiona wanasita sita kuanzia hapo wewe ndiye kiongozi wa hilo jeshi. Shamra alivyofika akawaamuru wanajeshi wamteke Hussein na kumfanya mateka. Al Hurru Ibn Yaziid akakataa. Akawaambia yeye hawezi kumkamata Hussein. Akahama pamoja na wanajeshi wake 40 wakawa upande wa Hussein. Shamra akatoa amri vita vikaanza.
Hussein alikuwa na watu wake kama 70 ukijumlisha jeshi la watu 5000 hawafui dafu. Kwa hiyo watu wa Iraq wa Kufa walimlaghai na Jeshi la upande wa Gavana walikataa maombi yake 3. Hata lile la kumuacha aondoke zake walilikataa. Imam Hussein pamoja jumlisha msafara wake pamoja na lile jeshi lililomuunga mkono la watu 40 waliuliwa wote. Imam Hussein kichwa chake na vya wenzake vikakatwa kutenganishwa na kiwiliwili.
Hussein hakuuliwa na Ahlul Sunni wal jamaa kama Shia wanavyoeleza. Bali maswahaba wenyewe ni ahlul sunni waljamaa. Kama kumuua Hussein wangemuua huko kabla.