Mahujaji 31 wa Shiite wafariki na 100 kujeruhiwa kutokana na mkanyagano msikitini

Hivi huyu Imamu Hussein alikuwa na wadhifa gani? Aliuawa na kina nani? Na kwanini?
Imam Hussein alikuwa ni mjukuu wa Mtume Muhammad s.a.w: Alikuwa na ndugu yake mwengine akiitwa Hassan.

Baada ya Makhalifa 4 tangu alipofariki Mtume yaani kuanzia Abuu Bakr, Umar, Uthman na Ally. Kulitokea mvurugano wa madaraka na vuguvugu lilianza baada ya kuuliwa Umar. Baadaye akauliwa na Uthman baadaye akauliwa Ally. Hao wote ni Maswahaba wa Mtume waliyoishi na Mtume.

Umar aliuliwa na Abuu Lulu. Abuu Lulu alikuwa ni muajemi, ni mateka wa vita na alikuwa ni Juusi. Juusi ni watu wanaoabudu moto. Alikuwa ni mtengeneza jambia, silaha ya vita. Alimuua Umar wakati Umar akisalisha Waislam. Sababu ya kumuua alikwenda kuomba kitu kwa Umar akamwambia kuwa kuwa mwenye kusubiri, kuwa mvumilivu. Akamvizia akampiga jambia.

Uthman aliuliwa na waasi wakati amekaa nyumbani kwake akisoma Quran. Ally aliuuliwa Iraq na kama sijakosea ni mji wa Kufa. Aliuliwa na jamaa anayeitwa Abdulrahman ibn Muljuk, alimpiga panga Ally kipindi Ally anakwenda kusali. Ally ndiye baba mzazi wa Hassan na Hussein. Ambao ndiyo vijukuu vya Mtume.

Kipindi cha utawala cha Yaziid Ibn Munawia wakazi wa Kufa nchi ya Iraq walituma ujumbe kwa Imam Hussein kuwa hawamtaki yeyote uwatawale na awaongoze kwa maslahi ya Dini isipokuwa mjukuu wa Mtume. Hizo taarifa hazikutumwa mara 1 bali zilitumwa mara nyingi. Imam Hussein akamtuma ndugu yake kwa jina Muslim Ibn Aqiiy kwenda kuangalia mazingira kama yanayosemwa ni ya kweli.

Nia ya Imam Hussein haikuwa ni madaraka! Bali ni kutaka kusamamisha haki. Muslim Ibn Aqiiy alivyofika Kufa Iraq akaona kweli wanachokitaka watu ni mjukuu wa Mtume. Akamtumia barua Imam Hussein Madina na barua ikisema; walichodhmiria ni sahihi na wanakuhitaji wewe Hussein, na huku Kufa kuna jeshi la watu 30,000 wamejitolea kukulinda.

Imam baada ya kupata barua akataka kufunga safari lakini Maswahaba wa Mtume wakamnasihi. Wakamwambia Hussein kama unataka kuhama ni bora ukahamie Makkah. Huko patakufaa lakini siyo Iraq. Kwani iraq ni karibu na Sham(Syria ya zamani) na Sham kuna Yaziid Ibn Munawia ambaye yeye ndiye mtawala wa huko. Licha ya hivyo, Maswahaba wakamnasihi kumwambia, huko unapotaka kuelekea Kufa ambapo ni Iraq ndipo alipouliwa baba yako ewe Hussein. Na walimpa tabu baba yako mpakq alitamani kufa. Na wakamwambia kama wanakutaka wewe uwe kiongozi wao basi kwanza hao wakazi wa Kufa wamuondoe kiongozi wao wa huko. Miongoni mwa Maswahaba waliyomnasihi ni Abdallah Ibn Abbas, Abdullahi Ibn Umar na wengineo. Lakin Imam Hussein akasema anataka kuiweka haki mahala pake. Kwa hiyo akafunga safari.

Akatoka na baadhi familia yake pamoja na baadhi ya watoto wa ndugu yake Hassan. Maswahaba wakamsihi. Wakamwambia hapana! Wakamwambia tunafahamu kwamba umedhamiria kutoka lakini tunakushauri uwaache nduguzo kwa hiyo safari uliyodhamiria. Lakini Hussein alifunga msafara nao wale aliyodhamiria nao. Wakati wapo njiani kuelekea Kufa mji uliyopo Iraq, lile jeshi la watu 30,000 lilikula kiapo kumlinda Imam Hussein likaanza kupungua. Viongozi wa makabila wakapewa hongo wakahongeka na hakukuwa tena na Jeshi.

Kazi hiyo ilifanywa na gavana wa hilo jimbo aliyeitwa Inb Ziyad. Muslim Ibn Aqiiy aliyetuma akaangalie mazingira ya Kufa na Hussein akabaki peke yake. Akauliwa. Imam Hussein alipokuwa njiani kuelekea Kufa njiani akakutana na mshairi. Akamuuliza vipi huko Kufa! Mshairi akamjibu, habari za huko siyo njema. Miooyo yao ipo pamoja na wewe na panga zao zipo juu ya shingo yako, na Mungu ndiye mwenye kuhukumu na anafanya anachotaka.

Alipokuwa njiani kuelekea Kufa Imam Hussein akakutana na sehemu ndogo la jeshi la Gavana wa huko ambaye alitumwa kutizama mazingira kuhusu Hussein. Kiongozi wa hilo Jeshi alikuwa Al hurru Ibn Yazzid. Akamuuliza Hussein unakwenda wapi? Hussein akajibu anaelekea Kufa. Al Hurru Ibn Yaziid akamwambia huko unakoelekea sijaacha heri ya namna yoyote kuhusu wewe, na Al Hurru ibn Yaziid jeshi lake lilikuwa la watu 40, akamwambia nakushauri urudi.

Imam Hussein akasogea nyuma kidogo. Alipofikia akauliza ardhi hii inaitwaje? Wakamjibu Karbulaa. Baada ya kujibiwa hivyo Hussein akasema, Karbun wa balaa, akimaanisha majanga na dhiki. Alipulizwa kwa nini unasema hivyo? Akasema nimemuota Mtume. Wakamuuliza amekuambia nini? Akajibu siwezi kutoa siri ya nilichoambiwa.

Kwa ghafla! Likaja jeshi jengine la Gavana! Akaongeza wanajeshi likawa jeshi la watu 5000 likamfuata Hussein nao wakamwambia Hussein arudi alipotoka na wakamuweka akawa kizuizini. Hussein akawaambia nawaomba mniwasilishie masuala 3 kwa kiongozi wenu. Suala la kwanza alilowaomba Wamuache arudi nyumbani alipotoka, 2. Kama la kwanza haliwezekani basi wamuache akakutane na mtawala wa Sham Yazid ibn Muawia. Kama hayo yote hawayataki wamuache aende mahala popote kwenye kambi za waislam aendeleze masuala ya Dini.

Maombi yalipomfikia mtawala(Gavana) Ibn Ziyaad akasema mpeni anachotaka. Pembeni alikuwa mshauri jina lake ni Shamra Ibn Jawshan.Akamwambia Gavana tangu lini mateka akawaa anasema ni nini cha kufanywa. Gavana akamwambia nenda na mumkamate Hussain. Hiyo amri ukiona wanasita sita kuanzia hapo wewe ndiye kiongozi wa hilo jeshi. Shamra alivyofika akawaamuru wanajeshi wamteke Hussein na kumfanya mateka. Al Hurru Ibn Yaziid akakataa. Akawaambia yeye hawezi kumkamata Hussein. Akahama pamoja na wanajeshi wake 40 wakawa upande wa Hussein. Shamra akatoa amri vita vikaanza.

Hussein alikuwa na watu wake kama 70 ukijumlisha jeshi la watu 5000 hawafui dafu. Kwa hiyo watu wa Iraq wa Kufa walimlaghai na Jeshi la upande wa Gavana walikataa maombi yake 3. Hata lile la kumuacha aondoke zake walilikataa. Imam Hussein pamoja jumlisha msafara wake pamoja na lile jeshi lililomuunga mkono la watu 40 waliuliwa wote. Imam Hussein kichwa chake na vya wenzake vikakatwa kutenganishwa na kiwiliwili.

Hussein hakuuliwa na Ahlul Sunni wal jamaa kama Shia wanavyoeleza. Bali maswahaba wenyewe ni ahlul sunni waljamaa. Kama kumuua Hussein wangemuua huko kabla.
 
Wenzetu wakristo huenda kuhij alikoishi yesu jerusalem,nazaret,bethelehem,hutembelea pia mapito ya yohana mbatizaji ama watu muhimu wowote katika dini yao mfano kina petero,paulo etc

haihitaji bibilia itoe amri kuwa lazima watembelee maeneo hayo,

haya turudi sasa kwa hawa shia,sidhani kama quran imetoa maagizo ya kutembelea karbala ,simply because imam Husein aliuliwa miaka iliyofuata baada ya mtume kuwa ashakufa na quran ishashuka zamani,kwa hiyo haingii akilini kutaka Quran itoe amri ya kutembelea huko kabla ya haya Husein hajazaliwa,

imamu Husein ni mjukuu wa mtume kwa damu haswaaa,

kwa hiyo kuna kosa kweli watu kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya mjukuu wa mtume?,

hiyo ni kama nyongeza tu kwani washia hawajakatazwa kuhij maka,
 
Mkuu kuna nguzo za uislam ikiwemo moja wapo kuhijji.
Na ktk uislam hutakiwi ufanye vtu nje ya mafundisho.
Shia wameiadhimisha hyo kwao km ibadah ilhali Allah hakupitisha ibadah ya namna hyo eti kujichanja kisa Hussein.
 
Mimi naamini Siku ya Ashura haijatajwa kama nguzo ya 6,haya ni kama maadhimisho tu siyo nguzo,

kuna mambo mengi ambayo sio maamlisho ya dini ya kiislamu,
mojawapo hakuna amri ya kuwa kutakuwa na madhehebu kama sunni,imamu shafi,suffii,wahab,shia etc,

haya yamekuja kufuatana na mapokeo,ndo maana hata shia kuna madhehebu kwa mfano kuna hawa shia kiongozi wao ni ayotollah,kunna shia ismailia kiongozi wao Agha khan,

kuna shia hawa wa yemen,wamamfuata someboby Zyad,

kwa hiyo mapokeo jinsi watu walivyopokea dini na kutafsiri ndo ilizaa madhehebu,

ndo unakuta hata kwa wenzetu kuna roma,protestant,luthran,sabato etc,

lakini hutakuta wakristo waroma wanaita lutheran ni wapangani etc,

sure enzi zinaitwa zama za giza madhehebu ya kikristo pia walikuwa na uhasama lakini baadae hii hali ilitoweka,

kwa waislam hasa sisi sunni tuna tabia ya kuhukumu imani za watu wengine mfano hawa shia ama hata Ahmadiya,

Tukisahau kuwa hata sunni kuna madhehebu kibao ambayo mtume wa Quran haikutoa maamlisho kuwa kutakuwa na madhehebu haya na haya,

again mimi sioni tatizo la shia kufanya maadhimisho ya kumkumbuka mauaji ya mjukuu wa mtume kwani Quran isingeweza kuamlisha hilo kwani limekuja baada ya quran kuwa imeshashuka,

sioni tatizo kwanini historical figure katika uislamu zisikumbukwe eti kwasababu hajaamlisha
 
Mkuu kuna uislam na muislam.
Uislam ni dini ambayo ina taratibu zake zinazotakiwa kufuatwa kwa misingi ya Qur'an na sunnah za Muhammad(s.a.w).
Ktk hii misingi ili uwe muislam bora watakiwa uifuate itakikanavyo,ikitokea umekengeuka isiwe kwa makusudi eidha iwe kwa kughafilika ama ujahili ama makosa tu ya kibinadam.
Ila usikengeuke kimakusudi kwa kujenga matashi na kutaka kufata utashi wa nafsi.
Ukifanya hvyo basi ushakufuru ww hatuwez kukuhesabia kuwa muislam maana uislam hauendeshwi kwa matashi ya nafsi ya mtu.

Mashia hawa watu ni watu ambao wanafata dini kwa matashi ya nafsi zao.
Kiasi wameleta mpk taratibu zao za kiibada na kuziingizia ktk uislam ilhali uislam haujasema hvyo.
1)Wameanzisha ibada ya kujipiga na kujichanja na mapanga kisa Hussein ilhali Allah na mtume wake hawakuweka qatwiyyu dillala ya hzo ibada kuwa zifatwe.
2)Uislam una shahada mbili wao wameeka shahada tatu.
3)Kuzuru miji mitukufu,kufanya hijjah na umrah ni makkah na madinah tuh na misikiti mitukufu ni Masjid haram(makkah),masjid Quba(madinnah) na masjid al aqsa(Palestine ) ila wao wanaenda kutukuza maimam huko karbala.
4)Baadhi ya aya za Qur'an wanatafsiri sivyo ili kukidhi matakwa yao mathalan Ile ayah isemayo "hakika wake zenu ni mashamba yenu waingilieni mtakavyo" wao wametafsiri kuwa Allah karuhusu kufirana ilhali hiyo ayah imekusudiwa kuwa wake zetu ni mashamba yetu tuwazalishe tutakavyo ndio maana Allah kataja shamba ukisema kuhusu kufirana inamaana wake zetu hawatozaa ni sawa na kupanda mbegu fake ktk shamba.

Hiyo kuhiji makkah haijalishi ila tizama kuwa hawa ni waislam wanaofanya vtu kwa utashi wa nafsi zao ktk dini je Allah atawaridhia hawa ilhali wamemzushia uongo hadi Allah ???!!!!
Jibu laah ndio maana nawatamka kuwa sio waislam sahihi.
Waislam jina tu.
Swadaqta! Muanzilishi wa Shia ni Abdillah Ibn Saabah. Ni Myahudi aliyesilimu kinafki.
 
Mimi naamini Siku ya Ashura haijatajwa kama nguzo ya 6,haya ni kama maadhimisho tu siyo nguzo,

kuna mambo mengi ambayo sio maamlisho ya dini ya kiislamu,
mojawapo hakuna amri ya kuwa kutakuwa na madhehebu kama sunni,imamu shafi,suffii,wahab,shia etc,

haya yamekuja kufuatana na mapokeo,ndo maana hata shia kuna madhehebu kwa mfano kuna hawa shia kiongozi wao ni ayotollah,kunna shia ismailia kiongozi wao Agha khan,

kuna shia hawa wa yemen,wamamfuata someboby Zyad,

kwa hiyo mapokeo jinsi watu walivyopokea dini na kutafsiri ndo ilizaa madhehebu,

ndo unakuta hata kwa wenzetu kuna roma,protestant,luthran,sabato etc,

lakini hutakuta wakristo waroma wanaita lutheran ni wapangani etc,

sure enzi zinaitwa zama za giza madhehebu ya kikristo pia walikuwa na uhasama lakini baadae hii hali ilitoweka,

kwa waislam hasa sisi sunni tuna tabia ya kuhukumu imani za watu wengine mfano hawa shia ama hata Ahmadiya,

Tukisahau kuwa hata sunni kuna madhehebu kibao ambayo mtume wa Quran haikutoa maamlisho kuwa kutakuwa na madhehebu haya na haya,

again mimi sioni tatizo la shia kufanya maadhimisho ya kumkumbuka mauaji ya mjukuu wa mtume kwani Quran isingeweza kuamlisha hilo kwani limekuja baada ya quran kuwa imeshashuka,

sioni tatizo kwanini historical figure katika uislamu zisikumbukwe eti kwasababu hajaamlisha
sisi tumekua umma bora kwa sababu ya kuamrishana mema na kukatazana maovu
Uislam umekataza maombolezo jamaa hawa ndio wanafanya
Pia uislam umekataza kujidhuru hawa jamaa ndio wanajikatakata Na kujitoa damu kabisa
Kwa ujumla dini ni muongozo Na sio fikra za mtu kama Wangekua wanafanya tu wenyewe hakuna shida tatizo wanayanasibisha Na uislam na hilo halikubaliki
 
Mimi naamini Siku ya Ashura haijatajwa kama nguzo ya 6,haya ni kama maadhimisho tu siyo nguzo,

kuna mambo mengi ambayo sio maamlisho ya dini ya kiislamu,
mojawapo hakuna amri ya kuwa kutakuwa na madhehebu kama sunni,imamu shafi,suffii,wahab,shia etc,

haya yamekuja kufuatana na mapokeo,ndo maana hata shia kuna madhehebu kwa mfano kuna hawa shia kiongozi wao ni ayotollah,kunna shia ismailia kiongozi wao Agha khan,

kuna shia hawa wa yemen,wamamfuata someboby Zyad,

kwa hiyo mapokeo jinsi watu walivyopokea dini na kutafsiri ndo ilizaa madhehebu,

ndo unakuta hata kwa wenzetu kuna roma,protestant,luthran,sabato etc,

lakini hutakuta wakristo waroma wanaita lutheran ni wapangani etc,

sure enzi zinaitwa zama za giza madhehebu ya kikristo pia walikuwa na uhasama lakini baadae hii hali ilitoweka,

kwa waislam hasa sisi sunni tuna tabia ya kuhukumu imani za watu wengine mfano hawa shia ama hata Ahmadiya,

Tukisahau kuwa hata sunni kuna madhehebu kibao ambayo mtume wa Quran haikutoa maamlisho kuwa kutakuwa na madhehebu haya na haya,

again mimi sioni tatizo la shia kufanya maadhimisho ya kumkumbuka mauaji ya mjukuu wa mtume kwani Quran isingeweza kuamlisha hilo kwani limekuja baada ya quran kuwa imeshashuka,

sioni tatizo kwanini historical figure katika uislamu zisikumbukwe eti kwasababu hajaamlisha
Kuhukumu ni kazi ya Mungu!

Muislam anyemhukumu Shia amechupa mipaka. Kwa maana ameingilia kazi ya Mungu.

Na Uislam umekataza kuikhtalifiana na mtu hata kiimani isiwe ndiyo kama vita. Bali unatutaka tuishi nao kwa Wema na tutakiane mema.
 
Mkuu umeenda nje ya mada kabbisa.
Unapozungumzia kuhusu masuala ya madh'hab ya imam shafii,hambal,Abuu Hanyfah na Malik hayo ni madh'hab ya kielimu.
Lakini yanaelezea misingi mimoja ya iman na yanaelezea yale mtume na Allah walioelezea.
Katafute ktk madh'hab zote za hao maimam hukuti kitu ambacho hakijaelezewa na mtume na Allah.

Kuhusu answar(sunni) answar nadhan unajua historia yake na maana ya answar hao ndio waliopigania dini kaka.
Urafaau rashidiin wote ni answar.
Maimam wakuu wote answar.

Mashia wao wanafanya vtu kwa utashi nje na mafundisho ya uislam bro usitake kuwatetea.

Bro unakumbuka mtume alisema asithubutu mtu yeyote kwenda kulia ktk kaburi lake????

Mashia wamefanya hiyo ni ibada sijui umenielewa?????

Kuna ibada wao wameitengeneza kuadhimisha siku ya kufa Hussein.
Je ww huoni kufanya ibada kinyume na mafundisho ya mtume na Allah ni bidaah????

Embu funguka mkuu.
 
Shia ndo waislamu waliostaarabika kuliko makundi yote ya kiislamu.
Mafunzo yao ni Yale ya kizazi cha mtume wa uislamu.

Makundi yote ya kigaidi duniani ni ya madhehebu ya ki sunni .
Hautokuta shia anjilipua au anaua watu wasio Na hatia.
 
Makafiri tu Kama makafiri wengine
 
Shia ndo waislamu waliostaarabika kuliko makundi yote ya kiislamu.
Mafunzo yao ni Yale ya kizazi cha mtume wa uislamu.

Makundi yote ya kigaidi duniani ni ya madhehebu ya ki sunni .
Hautokuta shia anjilipua au anaua watu wasio Na hatia.
Duuuuuuh we jamaaa embu sema astaghafirullah.
Unapozungumzia makundi ya kigaidi unaenda mbali na utatoka nje ya mada mkuu maana yale makundi hayapiganii dini km unavyoaminishwa.

Halafu shia huwez sema wana mafundisho sahihi kuliko sunni utakua mchawi wa millenium kuwahi tokea.
Shia wanaenda kinyume na mafundisho ya uislam kuwahi tokea.
1)Muhammad ametamka shahada mbili kutoka kwa Allah kuagiza kuwe na shahada mbili ila shia ana shahada tatu.
2)Shia wamezuka karni hii ndugu yangu ilhali hao sunni unaowazungumzia ndio waliopigania dini mpk kufikia hapa.

Answar(sunni) ni wale waloinusuru na kuipokea dini ya Allah kwa kuvutiwa na mienendo ya mtume kabla ya kumuona mtume.
Na hii jina walipewa watu wa madinnah yathrib.Kwasababu wao walimkubali mtume kwa kumsikia kwa watu wafanyabiashara waliokua watoka makkah kwenda madinnah kabla hawajamwona.
Baada ya muhajjirin (waislam waliofanya hijra/kuhama kidini toka makkah kuingia madinnah) walipowasili madinnah nao wakawa ni answar ile muhajjirin waliitwa kutokana na kuhama kwao.
Baada ya hapo answar muktadha wake ukawa ni kila Yule ainusuruye dini ya Allah na kufata maamrisho ya Allah na mienendo sahihi ya mtume(s.a.w).

Ukitizama ktk historia ya kiislam hakukua na shia kipindi cha mtume wala Ahmadia.
Mtume hakuagiza Ally atukuzwe ama Hussein aundiwe ibada ya kujikatakata ila hyo wanafanya mashia.
Mashia wanamtukana Bi.Aisha aisee kuna article zao nilikua nasomaga astaghafirullah mke wa mtume wanavyomtukana Allah hapendi.
Wale shia wanamtukuza Hussein na Ally kupitiliza ht huyo mtume hawamswalii.

Swali dogo tu ;
Allah alitoa agizo tutamke shahada mbili "Laailaha illa Llah Muhammadun rasuulu llah"
Na mtume kaitamka hyo hyo na maswahaba wote wameitamka hyo.
Hii shahada tatu ya "Laailaha illa Llah Ash'hadu anna Ally waliyyu Llah Muhammad rasuulu Llah".
Nambie mtume aliwahi itamka wapi???!!!!!!
Yani unamtanguliza Ally kushinda mtume ??!!!

Kama umeingia kwa hao jamaa waloigeuza ayah ya Allah kuhalalisha ulawiti wa wake zao rejea kwa Allah na mtake msamaha Allah utakua umepotea ukubwa wa kupotea kaka.
 
Kuhukumu ni kazi ya Mungu!

Muislam anyemhukumu Shia amechupa mipaka. Kwa maana ameingilia kazi ya Mungu.

Na Uislam umekataza kuikhtalifiana na mtu hata kiimani isiwe ndiyo kama vita. Bali unatutaka tuishi nao kwa Wema na tutakiane mema.
Ushia ni UKAFIRI.
 
Kumbe na akili zako timamu wewe ni Shia??
Sio kila msuni anaunga mkono Mambo ya alqaeda,ISIS.
Shia ndo waislamu waliostaarabika kuliko makundi yote ya kiislamu.
Mafunzo yao ni Yale ya kizazi cha mtume wa uislamu.

Makundi yote ya kigaidi duniani ni ya madhehebu ya ki sunni .
Hautokuta shia anjilipua au anaua watu wasio Na hatia.
 
Boko Haram....Sunni
Isis........Sunni
Magaidi wote wanafata uislamu feki,uliopotoshwa wa mazehebu ya sunni
 
Ushia ni UKAFIRI.
Nakubaliana na wewe.

Lakini kidini hairuhusiwi hata kwa kafiri kusema huyo ni mtu wa motoni! Na ndicho ninachomaanisha.

Kusema motoni tayari hiyo ni hukumu. Na mwenye kutoa hukumu ya namna hiyo kwa waja ni Mungu tu.
 
Hizi dini uchwara ifike mahala muachane nazo!

Nchi yetu ina matatizo makuu matatu: ujinga, umasikini na maradhi.

Tupambana na hayo!

Hakuna mahali mtu amekufa au kuteseka kwa sababu hana dini!

Lakini kuna watu wamekufa na kuteseka kwa ajili ya dini.

Ugaidi, vita, chuki, wizi.. vyote vimeletwa na dini.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom