Mahaba yaliyo murua

Ado Shaibu

Member
Joined
Jul 3, 2010
Posts
99
Reaction score
111
:A S 11:MAHABA MURUA
Niliripoti chuoni, sina kitu mfukoni
Mawazo tele kichwani, kijana takula nini?
Sina mwenyeji mjini, atanisitiri nani?
Mahaba yako murua, usiniache mpenzi

Zikapita wiki mbili, mpenzi ukaingia,
Shida zangu za awali, taratibu kapungua,
Wewe ukanifadhili, mwandani ukanilea
Mahaba yako murua, usiniache mpenzi

Umenipa pa kukaa, ada ukanilipia
Nikapata vya kuvaa, vyote umegharamia,
Hivi nani asojua, chakula wanipatia?
Penzi lako ni murua, usiniache mpenzi

Kwa vitabu hautoshi, desa* umenipatia
Mara chache kwa ubishi, hovyo ninakutumia,
Nawe vile si aushi*, huishia niumbua
Penzi lako ni murua, usiniache mpenzi

Amini nakuambia, umenitia kiwewe,
Tangu mwanzo wa dunia, jatokea kama wewe,
Penzilo menisisimua, sijaona mfanowe
Mahaba yako murua, usiniache mpenzi

Nakupenda sana bumu*:A S wink:, mpenzi wa moyo wangu
Haitoshi kwa kalamu, kuchora hisia zangu
Ukawiapo kutimu, chuo chote ni kichungu
Mahaba yako murua, usiniache mpenzi

Hata walio nyumbani, wengi wanakukumbuka
Wamehitimu chuoni, bado wanahangaika
Watakufuta kichwani, ndarama* wakizishika
Mahaba yako murua, usiniache mpenzi

©Ado Shaibu ( Komredi wa Malenga). 3/06/2014

Note:
*Desa/madesa: jina linalotumika kwenye vyuo vingi nchini kumaanisha vitini (hand-outs)
*Aushi: kitu cha kudumu/chenye kuishi kwa muda mrefu
*Bumu (Boom): Jina linalotumika kumaanisha pesa za malazi na chakula zitolewazo na Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
*Ndarama: fedha
 
Bumu laweza kuwa sugar mama/demu impliedly apart from narrow interpretation,basing on it tutegemee marioo/ombaomba wengi baada ya kurudi ktk maisha halisi ya mtaa yenye changamoto nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…