Magamba ya Mwanza

Silly

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
569
Reaction score
180
Uchaguzi wa mwaka jana ulizaa matunda na kubadilisha sura ya Mwanza baada kujivua magamba. Ila viongozi waliopata zile nafasi sijaona kama wanazitumia vizuri kwangu mimi kama mtanzania wa kawaida ambaye hana fursa ya kuingia kwenye vikao vya wakubwa kujua mipango yao, barabara zetu bado zinadai, drainage system kama vile haipo, maji safi na salama kidogo bado ni ya shida kama kipindi cha magamba, au ni nini kinakwamisha haya. Ofisi za jiji bado wizi mtupu na mipango ya mji haijaeleweka wala kuwekwa wazi, jamani mpo au mlishahamia Dar kama waliowatangulia..
 

hebu tuambie ni mda gani umepita tangu halmashauri hiyo inayoongozwa na chadema ipitishe bajeti yake ya kwanza?
 
Mkuu bajeti sina uhakika nayo ila kama nilivyosema kwa mwananchi wa kawaida ambaye hapati nafasi ya kukaa na hawa watu, kile ambacho anakiona machoni kwake ndicho atashika, in any case bajeti waliyoikuta wakati wanaingia madarakani ipo na mimi nadhani lazima tofauti yao na waliowatangulia inabidi ionekane kama imani ya wana Mwanza itabakia
 
naunga hoja mkono wabunge wetu inabidi watueleze mipango na mikakati yao ni ipi
 
Mkimaliza maanadamano tunataka mikakati si porojo kama magamba??
 
Mikakati ya chadema ipo wazi nayo ni kuziba mianya yote ya wizi ya ccm, kuanzia bajeti ijayo angalia halmashaur5i zote za chadema kama utaona wizi wa kijinga kama zile za wenzetu wazee wa kulindana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…