Nilitegemea baada ya serikali kutoa kandarasi ya kuingiza mafuta mengi kwa kampuni moja basi watumiaji wa nishati hiyo tungepata ahueni kidogo...lakini imekuwa kinyume baada ya shehena hiyo kufika nchini na kushishwa tumetangaziwa na EWURA kuwa mafuta bei juu tena. sasa lipi bora turudi kule kule kwenye soko huria au huyu fisadi mmoja aendelee kutakamua walipa kodi. Nahisi na hili wangunge wa DSM wangeliundia muungano lingekuwa la msingi kabisa
Haya wale wabunge wetu wanaotutea sisi wanyonge wanasemaje? Walishirikishwa kabla EWURA hawajatangaza hii bei mpya? au ushirikishwaji ni kwa Magufuli peke yake?
Tushazoea, ni ajabu bei ya mafuta ya taa kuwa sawa na bei ya petroli, hii ni kuwaumiza walalahoi kwa makusudi, ni vyema tukawajua ccm kuwa ni chama fisadi na maslahi, pia kina wenyewe ambao ni matajili, masikini tulie kwani hatuna mwenyewe.
EWURA kama TAKUKURU, hawana tija yo yote kwa taifa...ni mzigo tu wanatuongezea gharama za bure za uendeshaji wa serikali. Kabla ya Ewura hatukuwa na matatizo ya ukosefu wa mafuta wa mara kwa mara. Hasara ambayo wananchi huwa tunaipata wakati mafuta yanapoadimika ni kubwa hata wengine hupoteza maisha kwa kukosa usafiri wa kuwafikisha kwenye vituo vya afya, kuliko hata hilo punguzo la "sh. 22/- kwa lita. Iachwe bei ya soko itawale, hii itatuhakikishia uwepo wa mafuta wakati wote na hivyo wananchi kuendelea na shughuli zao kama ilivyokuwa miaka michache iliyopita.
Tusilalamike wazee,wanatutia adabu ili tupate akili,na tujue ushabiki wa vyama hauna maslahi yoyote,kama hatuthamini maisha yetu wenyewe tukaeni kimya basi,tutalalama na kunung'unika hadi lini?waacheni wachukue chao mapema.