MWANA WA UFALME
JF-Expert Member
- Sep 10, 2010
- 578
- 144
wanahubiri maendeleo lakini hawajui kuwa pesa zilizopo hapa Tanzania ukizichanganya na uhuru wa watu na haki ya kuhoji mambo yapatiwe majibu hatuna haja ya misaada!
Wenyewe wanaona raha kupoteza muda na pesa ili kuficha hizo variables za maendeleo na mafanikio. Tutawalaumu viongozi sana lakini mwishowe tutagundua kuwa viongozi waliwekwa hapo na sisi (hata kama ni kwa nguvu) hivyo tujilaumu wenyewe kwa kutochukua hatua yoyote au kuwaunga mkono wanochukua hatua!
My take kwa uchunguzi wa bomu hili unavyoendelea;
Uchunguzi huu unazunguka tu wagonjwa na viongozi wa chadema
Hii ni dalili kubwa kwamba huu sio uchunguzi bali ni jitihada za kuficha uhalifu,
Huwezi kusema tukio limetokea toka juzi na hadi leo polici wanahangaika kutafuta wagonjwa na wabunge kuwapeleka mahakamani, wakati mhalifu wanamjua vizuri na ni kipenzi chao.
Bora turudishe jeshi la sungusungu, hili linaweza kuwa na nizamu zaidi. Arusha morani wanatosha kuilinda. Hakuna haja ya kuwa na chombo cha umma kinachofanya kazi ya kuua watu huku viongozi wakubwa kama waziri mkuu akishangilia kwa kazi njema.
Je kwa kauli ya Pinda, nyuma ya pazia yawezekana jamaa wanaandaa promotion ya aliyemaliza kazi aliyotumwa huku wakijishughulisha kumlinda asifahamike?
.....hata leo ktk mahojiano yao kati ya Polisi na viongozi wakuu wa CDM (Mbowe na Lema), kubwa zaidi kwa upande wa polisi itakuwa kutaka kujua viongozi wa CDM wana ufahamu kiasi gani juu ya ukweli wa kilichotendeka na siyo uchunguzi ili wajipange jinsi ya kujihami kwa upande wao(polisi)
Kwa ushauri wangu, wangekomaa tu bila kutoa huo ushahidi. Kitakachotokea ni wao kuwekwa ndani ili wapelekwe mahakamani na ndiyo wakatoe ushahidi huko. Kwa wale wanojua kusoma gestures language, ni dhahiri kuwa hili swala limeshawakoroga polisi wenyewe( haswa jana alipokuwa akiongea Chagonja kwenye taarifa ya habari ya ITV). Anaonekana hana hakika, lakini pia kushindwa kutoa msimamo wa polisi juu ya jambo lenyewe.
Mbowe na Lema wanatakiwa kuwa werevu zaidi wanapoongea na hao polisi kuepuka mazingira yeyote ya kutoa huo ushahidi.
Hayo ni maoni yangu!