Madhabau ya wachawi

MANYORI Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2012
Posts
462
Reaction score
343
Ndugu zangu,ukisikia kuokoka kwa tafsiri ya kawaida ni kuacha dhambi.Mtu anapobatizwa ni kiashiria cha kufuta dhambi zake.Kwa msingi huu waumini wa madhehebu karibu yote na viongozi wao hutazamwa kama watu waliokombolewa.
Hii ina maana kuwa katika maisha ya kibinadamu historia za mambo yao mabaya hazifutiki katika mtiririko wa matukio yao bali katika roho ndimo huhesabika kusafishwa kama theruji.
Tunapokaa makanisani,misikini,na pengine vilingeni tusisahau kuwa madhabahu zetu zinahudumu waliokuwa wamepotea(kondoo wa bwana)
Vitendo vya watumishi kwenye maeneo hayo kuwaagiza waumini kuleta vitu fulani fulani kama mchanga wa nyumbani kwao,kupakwa mafuta ya baraka,kunyunyuziwa maji ya baraka n.k n.k ni ishara kuwa kazi ya shetani inaendelea pale.Makuhani kugeuka kuwa wapiga ramli madhabahuni na mambo mengine ya kipagani ni vithibitisho kuwa pana madhabahu ya Kishetani.
Asubuhi njema.
 
Mkuu unamaanisha kuwa kupakwa mafuta au kunyunyiziwa maji ya baraka ama kupeleka mchanga ukaombewe huo nao ni uchawi?
 
Kama ni uchawi ina maana watumishi wa sasa ni wachawi?

Je hakuna watumishi wawezao kuwashinda hao wachawi?

Nakumbuka mtume Petro na hata mtume Paulo waliwaendesha mputa wachawi wa enzi hizo maana vivuli vyao , vitambaa walivoviombea vilipindua madhabahu za wachawi

Mimi naamini wapo watumishi leo hii wanaoweza kufanya ishara na maajabu ili kuponya kwa njia ya miujiza.
 
Kwa kawaida,muujiza hufanywa pasipo kitu au na kitu.Lakini haya ya kuagizwa michanga ya majumbani mwenu,kununua au kupakwa mafuta ya baraka,kunyunyizwa maji msiyoyafamu yatokako ndiyo uchawi wenyewe huo.Hayo na mengine kama hayo ni maagizo ya kichawi kabisa wala hayana nasaba za utakatifu.
 
Naona una hasira na wapakwa mafuta wa shetani.

Ila wapakwa mafuta wa BWANA wapo kazini hata sasa wanaombea picha, documents , maji, nguo, nk
Wahusika hupokea muujiza kupitia vitu hivyo yanapofaka maombi.

Mimi ni shuhuda wa maombi ya namna hiyo , nilimshinda adui yangu aliyevamia kiwanja changu huko makabe.
Haikuwa vita ya kitoto yeye alienda kwa wapiga ramli ili anidhurumu kiwanja changu , lakini mimi nilienda kwa pastor wangu akaniombea na akaniomba nikachote na mchanga ili nao uombewe .

Nilimshinda huyu maana alikimbia na tunguri sake na kesi ikaisha.

Ipo nguvu ktk maombi kupitia vitu husika naamini hakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…