Mheshimiwa Spika mi
nawashangaa sana hawa wapinzani,wao hawaoni jema hata moja lililofanywa
na serikali hii ya chama tawala,huko majimboni kwao serikali imewafanyia
mengi sana,kweli shukrani ya punda mateke.
Mheshimiwa spika,nirudi sasa katika hoja,kwanza nimpongeze Waziri kwa
umakini wake wa hali ya juu na hotuba maridadi yenye kujali maisha ya
wananchi na yenye kutekelezeka,hongera sana serikali yetu sikivu kwa
utekelezaji wa ilani ya chama chetu pasipo kujali kelele za wapinzani
Mheshimiwa Spika,jimboni kwangu ni kama sio Tanzania,barabara za lami
jimboni kwangu tunaishia kuziona kwenye tv,kila mwaka bajeti
zinatekelezwa pasipo hata kuleta japo moram jimboni kwangu.
Japo sio mahala pake naomba nifikishe kilio chetu,maana mbali ya
kutokuwepo barabara jimboni kwangu umeme ni bidhaa adimu sana jimboni
kwangu,kuhusu maji ndo usiseme watu wanakunywa tope kama maji ya
kunywa,zahanati ipo moja nayo haina hata daktari hata mmoja.....
Mwisho naunga mkono hoja 100%,nawaambia wapinzani walie tu mwaka huu
hawana chao,sisi ndo chama dume,mwendo mdundo,
nawaambia wamebugi meeni.