Maajabu ya Zanzibar, hawalimi, hawafugi lakini wanakula wanashiba

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,490
37,334
Aliyesema kilimo ni uti wa mgongo au kale kamsemo ka mhenga kuwa kama mnataka mali mtayapata shambani aje Zanzibar. Hata ule msemo wa kwenye bible kuwa asiyefanya kazi asile aje Unguja atengue kauli yake.

Unguja nzima ng'ombe walioko hawazidi 1000, mashamba yaliyopo yanatosha kulisha wilaya moja au mbili lakini hutosikia Zanzibar wana njaa au wamekosa chakula.

Saa nne watu wanacheza bao na dhumna ila ikifika mchana madogo wanakuja kuwaita baba zao kijiweni waende wakale msosi nyumbani.
 
Zanzibar pesa wanazipata kwenye, uvuvi na biashara za ndani na nje ya nchi na wanunuzi wakubwa wa mazao ya bara na kuuza Zanzibar pia ndio wafanyabiashara wakubwa bara mfano wapemba wamejaa huku wakifanya biashara bara na Zanzibar.

Pia ndio wameshika sekta ya utalii kuanzia sehemu za vyakula, nyumba za kupangisha wafanyakazi wa sekta ya utalii kama mahoteli nk hupanga vyumba vya nyumba zao Kwa bei Kali na wapangaji wengi wafanyakazi huko wanatoka bara ambao wamejazana hasa kwenye kazi za mahoteli mamia ya kitalii yaliyoko Zanzibar.

Mleta mada unaonesha hujafika Zanzibar

Ferry Dar wavuvi wa Zanzibar huleta samaki Kila siku wakiuza wanageuza wanarudi zao Zanzibar
 

Soma vizuri andiko, lengo ni kuonesha kuwa kilimo sio shughuli pekee ya kujenga uchumi wa nchi.
 
Hujafika Zenji wewe! Umaskini uliopo huko, ni balaa, nenda Paje, Uroa, understand uone umaskini, hakuna cha ajabu, bila ma hotel ya kitalii, fedha ni ngumu Zenji, vijana kama sio madereva wana kuwa beach Boys, sex toys, kazi, za mahotelini zinafanywa sana na mabinti kutoka Bara, wa zenj, Imani za dini ni kikwazo, mabinti wa Zenji wao ni kuzaa tu na kuvaa ushungi! Na kusubiri pipe usiku.
 
Uchumi wa bluu ndugu! Baharini kuna viumbe na vyakula mara elfu kuzidi kwenye mavumbi huko!
 
Haijapata kusikika baa la njaa limeikumba Zanzibar kiasi cha kupelekewa chakula cha bure na serikali. Hiyo ndio hoja yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…