Tunapoendelea kuomboleza na kusikitika na madhila ya ajali ile, kwa upande mwingine napo maaajabu ya Mussa na ajali ya Igunga yanaendelea.
Walitokea kina Mwigulu Nchemba kutaka sheria zikiukwe kwa madereva kukamatwa kwa makosa yasiyokuwa na adhabu hiyo. Sasa kumeibuka wanojiita wadau wanaopendekeza hadi kuwapo na madereva wawili kwenye malori na kuwa ati mtu mmoja anapaswa kuendesha masaa nane tu kwa siku. Kisichofahamika composition ya hawa wanaoitwa wadau ni kina nani hasa na uzoefu au ufahamu kiasi gani kuhusu shughuli za usafirishaji mizigo?
Pamoja na kuwa ajali ya Igunga ilisababishwa na mashimo ambayo TANROADS wamekuwa wakiyatelekeza katika barabara zilizo nyingi hapa nchini labda kwa sababu zao yaonesha bado jitihada za kumtafuta mchawi asiyekuwapo zitaendelea.
Kwa sasa Hatutadanganyika! Inafahamika na ni wazi kuwa ajali ya Igunga chanzo ni mashimo ambayo TANROADS kayatelekeza. Hizi kelele zingine labda kama mnataka kutulazimisha. Hakika kwa mwendo huu wa kujaribu kutafuta sababu za kutengenezesha mtatufikisha hata wale ambao hatukutaka kuambatana na Dada Mange April 26 kufikiria upya.
Please stop Insulting our Intelligence. Tunaowasikiliza tu binadamu danganya toto hizi sasa zinatosha na hazina tena nafasi katika Tanzania ya sasa.
Inakera kuona sababu kamili zinapindishwa wakati ukweli unafahamika hata na mototo mdogo.
Haya ni yale ya kumwacha aliyefyatua risasi na kumshitaki aliyeandamana na kutuaminisha kuwa asingeandamana wasingefyatua risasi. Ama kweli haya ni hapa kwetu tu.