Maajabu Kuhusu Mafao Mifuko ya Jamii

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
855
Wakati mfuko wa jamii wa LAPF ukitoa fao la kujitoa kwa wanachama wake bila ya masharti, mfuko wa jamii wa PPF umesitisha fao hilo tangu mwaka jana mwezi wa 5. Sababu zinazoelezwa na PPF ni kwamba, wanasubiri maelekezo toka serikalini.

Kituko na Maajabu:
Huku wakisema fao la kujitoa limesitishwa, ni PPF hao hao wanaotoa fao hilo kwa watu wanaopunguzwa makazini. Ila kwa wale wanaofukuzwa kazi, hawapewi fao hilo. Haya yote yanafanyika huku mfuko huu ukiwa chini ya SSRA chombo ambacho kina visimamia na kutoa muongozo kwa mifuko hii.

Wakati haya yakiendelea, vijana wengi ambao wamekuwa wanachama wa PPF, na ambao wamepoteza ajira kutokana na kufukuzwa hovyo na waajiri wahuni, wameendelea kuteseka mitaani wakati pesa zao zinashikiriwa na mfuko huo wa PPF.

Kama wewe ni mhanga, ungana na wahanga wengine kupaza sauti kupitia page maalum iliyoanzishwa kwa kugonga na ku-like link hii hapa: Fao La Kujitoa Maisha Yangu
 
LAPF inatoa fao la kujitoa mpaka kesho ndo mana naamini hawa jamaa ni mfuko bora ukilinganisha na mingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…