Maproducer wameacha kuzalisha mziki wengi wao sababu mziki hauwalipi ,wamekuwa watu wazima amajukumu yanaongezeka malipo ni yale yale na wengi wao walioweka utaratibu wa malipo kila kazi yao itakapotumika wamekimbia.
Maproducer wa zamani wameacha mziki sio kwamba labda hawana content hamna,bali mziki hauwalipi na wasanii hawaheshimu creativity yao kwani wengi wao wanaamini bila wao,producer hawezi kuwa mkubwa mwisho wa siku Lamar kageukia katika Car wash yake na biashara yake ya chakula,Duke namuona anakampuni yake ya kutengeneza ferniture,kuweka partion kwenye maofisi ,Majani akawa yupo CMEA ,Master jay ana mishe zake nyingine,kwa kifupi kazi ya uproducer haina future nzuri.
Maproducer wa sasa hivi hata wakeshe studio lakini hawawezi kutoa product kama maproducer wa zamani .