M4C Mufindi lini?

nkisumuno

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
208
Reaction score
72
Wananchi wa Mufindi tunaomba M4C mje Mufindi maana tangu ratiba ilipoharibiwa na polisi siku walipomuua Mwangosi tunaona kimya.

Mufindi ni mojawapo ya wilaya yenye maliasili nyingi lakini wakazi wengi wamepumbazwa na CCM kwa muda mefu huku wananchi wake wakishindwa kusomesha watoto.

CHADEMA njoni makamanda ili kuwafunua blanketi lililowafunika wananchi na baadhi yao wakiwa hoi bin taabani kwa ufukara licha ya utajiri mwingi walionao.
 
Wala usiwe na wasiwasi Kamanda. Pamoja na M4C ya mikutano ya hadhara ya kuhamasisha wananchi kuunga mkono mabadiliko kwa kujiunga na CHADEMA ilisimama kdg baada ya CCM kupitia polisiCCM kuanza kuua, bado M4C iliendelea kwa namna nyingine huku ratiba ikifanyiwa marekebisho. Kwa hiyo kiuhakika kabisa haikusimama. Mufindi itakuja/ itarudi mkuu wala usiwe na wasiwasi.
 
Wakija watu kutoka mbali vijana wenu wanalalamika kwamba hawahusishwi.ref: utetezi wa kina shonza aka benazir. Anzisheni taratibu ili kuwapasha wananchi ili kuja kwa viongozi kuwe ni kukamilisha yaliyopangwa. Ni lazima viongozi wa eneo husika wajitolee kwa hali na mali kuwashawishi wananchi wakubali m4c kwani ile tabia ya kina slaa kuondoka na kila kitu kuwa kimya kama hamna kilichokuwa kinaendelea haifai.
 
Hatujasahu msiba wa Mwangosi; mtageuka wachawi kwa roho za watu!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…