Wanadamu kwa tabia tunapenda kusikia kwa masikio yetu 'yasiyotamkwa', yaani yale ambayo jamii inayakataza na kuyakemea. Sasa ili mtu apate hamu/bashasha ya kujifunza lugha ngeni, matusi ndo ya kwanza kumfundisha kwani hayo yatamvuta na kumchangamsha mpaka awe na hamu ya kujifunza mambo ya maana na ya siriaz. Kumbe matusi ni ndoano ya kukuvuta kuingia katika lugha mpya na utamaduni wa wenye lugha; vitu ambavyo ni vizito vyenye kuhitaji muda, umakini na toiling. Matusi mtu hahitaji nguvu nyingi kufunza, na ndiyo maana yanatangulizwa ili kukuandaa kwa kazi inayofuata ambayo ni sarufi ya lugha.