The Infamous
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 731
- 122
wakati wa mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2005, nakumbuka kila mtanzania alikua anakereka na kustaajabika kuwa aliyekuwa waziri mkuu wa serikali ya ccm 1995-2005 mh frederick sumaye alikua anataka kugombea urais kwa kupitia ticket ya ccm.
Mapungufu yake mengi tuliyaona na kuyajua, tuhuma kubwa zikiwa alikuwa akichukua mashamba ya watu kwa nguvu au kwa njia ambazo hazikua halali [these were mere allegations].pia na hela alizotumia wakati wa safari moja alienda marekani naomba mnisaidie kwa kumbukumbu nzuri.
Upande mwingine alichomoza el, ambapo ni kama watanzania tulijisahau sijui au ah? Au ndo ujinga wetu?, maana ni kama alionekana ni mtu msafi kwa mda wa kipindi kile cha mchakato wa uchaguzi 2005. Watu wote tulijua kuwa atakuja kuwa waziri mkuu lakini wachache tuliohoji umakini wake na utendaji wake kazi, hususan tukikumbuka el alikataliwa na alikuwa hakubaliki na mw nyerere kwa kuwa na utajiri mkubwa pasipo kawaida.
Wakati ule [2005] ulikua ukiwalinganisha el na fs ni kama lowasa ali edge ahead, na honestly media ilikua sana against fs.
Sasa tunajua a-q if not z ya el, je kuna ya fs ambayo hatuyajui ambayo yana uzito unao fanana na el au kumzidi.
Tukipima mizani yao nani kamzidi mwenzake mpaka sasa kwa ufisadi?
Nani anaweza ku-come back au anaweza kuwa the come back king, maana najua wote wana hamu ya kuingia kwenye uwanja wa siasa ila maji yamewazidi shingo...
Mundu said:Kuna siku nilikaa na rafiki yangu mmoja, akanambia kwa jinsi nilivyo makini ningekuwa waziri bora sana tz kuliko hawa waliopo... mara kumi zaidi. lakini sifikirii kuingia kwenye siasa. na nadhani kuna watendaji wengi wazuri wako tz, vijana wazalendo lakini wataanzaje anzaje kama siasa zenyewe ndio hizo za kupakaziana! na ukiingia lazima uegemee kwenye kundi la akina fulani, iwe ni mtandao n.k.
Pili, hata kwa hao waliopo, hakuna kiongozi aliye mfano bora na ambaye yupo tayari kuwa groom vijana ili wawe makamanda safi wa kupeleka nchi kwenye neema! nakumbuka mwanahabari mmoja makini pia, wakati akihojiwa alisema... tatizo la kuto groom viongozi lilikuwa moja ya weakness ya baba wa taifa... alipokufa... hakuna hata wa kurithi na kudumisha miongozo yake! Yote aliyoyajenga na kuyapigania, yanaparaganyika sasa!!!
Tanzania nakulilia!!
Nilikua najiuliza imekuaje Sumaye akawa anasemwa sana kwa ufisadi wa mapori tu ilihali kuna mafisadi papa kama akina vijisent tulikua hatuwasikii kabisa?
Baada ya kusoma post zilizotangulia hapo juu nimepata mwanga kuwa ulikua ni mchezo mchafu wa EL kummaliza. Hizi media zetu nazo kwa kweli zinachangia sana kuwaenzi mafisadi, hazitendi haki.
Pinda ndo safi maana yeye si fisadina anatuonea donge tunaovaa suti zetu kwa kuwa nchi hii ni masikini hivyo tuvae mashati ya batiki
Mkuu,Kuna modern dictatorship. Kuna mambo hayaendi bila mkono wa chuma, come on we need that sooner rather than later!
Pinda ndo safi maana yeye si fisadina anatuonea donge tunaovaa suti zetu kwa kuwa nchi hii ni masikini hivyo tuvae mashati ya batiki
Mkuu Joka kuu!!Mundu,
..mbona kuna vijana wengi tu wamejitosa kwenye siasa?
..Zitto,Masha,Adam Malima,Stella Manyanya,Muhonga, wote naweza kuwaweka ktk kundi la vijana.
..kuhusu kuwa groomed nafikiri Mwalimu ali-groom wanasiasa wengi tu kuja kushika nafasi za juu. labda tatizo hakutamka hadharani "fulani ndiyo mrithi wangu."
..chukulia mwanasiasa kama John Malecela. hata kama Mwalimu alikuja kukosana naye baadaye, lakini zile nafasi za ndani na nje alizoshika nadhani zilikuwa maandalizi tosha ya kuwa Raisi.
..hata JK naye toka kuwa Naibu Waziri, baadaye Waziri wa Nishati na Madini, halafu Waziri wa Fedha[kijana kuliko wote Tz], na mwisho Waziri wa Mambo ya Nje, naamini pia ilikuwa ni nafasi ya kujifunza na kujiandaa kuja kuwa Raisi.
..kama unaona tuna viongozi wabovu siyo kwasababu ya walinyimwa nafasi ya kujiandaa au hawakuwa groomed, ni kwasababu wahusika hawakuwa serious kutumia nafasi walizopewa kujifunza.
Majembe yetu UKAWAwakati wa mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2005, nakumbuka kila mtanzania alikua anakereka na kustaajabika kuwa aliyekuwa waziri mkuu wa serikali ya CCM 1995-2005 Mh Frederick Sumaye alikua anataka kugombea urais kwa kupitia ticket ya CCM.
Mapungufu yake mengi tuliyaona na kuyajua, tuhuma kubwa zikiwa alikuwa akichukua mashamba ya watu kwa nguvu au kwa njia ambazo hazikua halali [These were mere allegations].Pia na hela alizotumia wakati wa safari moja alienda marekani naomba mnisaidie kwa kumbukumbu nzuri.
Upande mwingine alichomoza EL, ambapo ni kama watanzania tulijisahau sijui au ah? au ndo ujinga wetu?, maana ni kama alionekana ni mtu msafi kwa mda wa kipindi kile cha mchakato wa uchaguzi 2005. Watu wote tulijua kuwa atakuja kuwa waziri mkuu lakini wachache tuliohoji umakini wake na utendaji wake kazi, hususan tukikumbuka EL alikataliwa na alikuwa hakubaliki na Mw Nyerere kwa kuwa na utajiri mkubwa pasipo kawaida.
wakati ule [2005] ulikua ukiwalinganisha EL na FS ni kama lowasa ali edge ahead, na honestly media ilikua sana against FS.
sasa tunajua A-Q if not Z ya EL, je kuna ya FS ambayo hatuyajui ambayo yana uzito unao fanana na EL au kumzidi.
Tukipima mizani yao nani kamzidi mwenzake mpaka sasa kwa ufisadi?
Nani anaweza ku-come back au anaweza kuwa the come back king, maana najua wote wana hamu ya kuingia kwenye uwanja wa siasa ila maji yamewazidi shingo...