Lowassa: Tumewashika CCM Pabaya

Ocampo four

JF Senior Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
5,789
Reaction score
2,159
Mgombea urais wa Ukawa kupitia CHADEMA Ndg. Edward Lowassa kasema kwa sasa Chama Cha Mapinduzi kiko hoi.... Lowassa kasema Ukawa wamewashika pabaya sana CCM na ifikapo tarehe 25 hawachomoki hata kwa dawa...

Lowassa kawaomba vijana, wakina mama, wazee na makundi mbalimbali siku ya kupiga kura (25.10.2015) kuwahi asubui sana katika vituo vya kupiga kura na kumchagua Lowassa, wabunge wa Ukawa na madiwani wa Ukawa...

Katika hatua nyingine mchambuzi wa siasa Professor Mbele kasema safari hii Ukawa watashinda kwa asilimia nyingi. Mbele kasema haoni miujiza ambayo CCM wanaweza kufanya kwa hizi siku 41 zilizobaki na kubadilisha mawazo ya wananchi wakati asilimia 89% ya wapiga kura washafanya uamuzi na mojority watamchagua mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa....

Mytake:... Wazee wa Lumbumba tukutaneni 25.10.2015.

==============================

Chanzo: Mtanzania
 

Hata Mzee wa kaya JK kakiri jana akiwa anamnadi mgombea urais wa Zanzibar kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni kama mchezo wa mpira wa miguu hivyo timu yake yaani CCM magamba watumie mtindo wa kukaba mtu kwa mtu, kwa maneno yake mwenyewe alisema " Man to Man" Maneno haya yanatudhihirishia kitu kimoja tu kwamba CCM inashindwa.
 
mwache mzee ajifariji Ila ifikapo Siku ya Siku asije kuanguka kwa presha
 
mwache mzee ajifariji Ila ifikapo Siku ya Siku asije kuanguka kwa presha

Hakuna dalili wala kishiria chochote kinachoonyesha kuwa CCM itashinda..... Kwa hizi siku 41 wajiandae kisaikolojia kutoka madarakani
 
Mmeshikana pabaya ukawa wenyewe,hakuna wakuwashika pabaya watu wenye akili hata siku moja,mwizi mwizi tu hata awe handsome,mbona hamkemei ufisadi?adui namba nne baada ya ujinga,maradhi,na umasikini.
 
Mimi nafurahi sana kusikia hayo maneno mazuri,ila kuna habari policcm wameingiza magari mapya defender za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha ccm inarudi kundini na kibaya zaidi kuna habari pia maafisa wa jw watavaa uniform za police kuhakikisha kazi yao inaenda vizuri,kikubwa ni kuombea taifa amani ili hawa ccm waikabidhi nchi ikiwa salama,jamani hizi ni mbio za kupokezana vijiti,ccm wamekimbia kwa miaka 50,na wamefanya mengi mazuri na mengi mabaya,sasa wakabithi tena kijiti kwa ukawa na wao wakimbie tuone watatufikisha wapi,then mchezo ukiwashinda tunarudisha kijiti kwa ccm ndo hivyo tu,maana wote tunachohitaji ni maisha bora na pesa tuione,sio wachache wahodhi kila kitu bila kuulizwa,hilo ndo hatutaki kabisa tena kulisikia
 

Aliye hoi zaidi ni CCM au yeye mwenyewe ambaye hata kupanda jukwaani anapandishwa kwa kushikwa masaburi, hata kipaaza sauti anashukiwa. Kwahiyo kitatokea bahati mbaya akawa Rais akipenda kwenye mikutano ya kimataifa Kama UN ataomba ahutubie akiwa amekaa
 

Mataifa ya nje wako macho sana katika uchaguzi huu Mkuu..... Kuna watu wasipoangalia watashitakiwa haraka sana....
 
Mmeshikana pabaya ukawa wenyewe,hakuna wakuwashika pabaya watu wenye akili hata siku moja,mwizi mwizi tu hata awe handsome,mbona hamkemei ufisadi?adui namba nne baada ya ujinga,maradhi,na umasikini.

Ni kweli Nyerere alituachia maadui watatu, nani kutuongezea adui namba nne?
 
Ccm kushindwa imejitakia. Hata wagombea wa wapo very disorganised kwa kwa kuishushua serikali iliyopo madarakani mbele ya wapiga kura. Huwa najiuliza Jakaya ana moyo wa aina gani kwani Magufuli anamtungua za uso kuhusu ulegelege, wizi na ufisadi mbele yake yeye kaganda tu na kujichekesha. Ningekuwa mie nampora kipasa sauti na kumjibu kuwa hata wewe ni mmoja wetu. Wanajichanganya na kutumia raslimali za nchi vibaya.
 
jamani ukawa na na malofa wengine fanyeni research!!reseach always bring a goog answear!!!njoeni na tafiti hapa c porojo za robot!!!ni mikoa ipi lowasa ataongoza kwa asilimia 90 na ipi pombe magufuli ataongoza kwa 90%!!!!!kwa mfano dar es salaam wamejiandikisha watu 2.8 milion!!wakati dar kuna wakazi 8 milion!!!acheni mambo ya media na upambe!!!dr magufuli ndiye rais mpaka sasa!!!research zinaonyesha anaungwa mkona kwa 90% mikoa ya simiyu,ruvuma,njombe,katavi,pwani,morogoro,dodoma,tanga,geita,tabora,shinyanga,mara,na rukwa!!!lowasa ana ungwa mkona kwa 90% manyara,arusha,kilimanjaro,singida,na iringa!!!!!na kwingine tanzania wanazidiana kwa karibu sana
 
kweli kwa sasa ukitaka kuwa ukawa lazima ujipime usije ukawa na akili kama za NYUMBU WA SERENGETI NATIONAL PARK!!!njoon na thread za kweli
 
ccm haiondoki madarakani leo wala kesho. poleni sana
 
Ni kweli Nyerere alituachia maadui watatu, nani kutuongezea adui namba nne?

Kwa maneno yako inaonesha kwamba Nyerere alishindwa kuondoa hao maadui watatu na ndio maana unasema ...alituachia...

Kwa maana hio unasema kwamba mpaka leo hii maadui ni wanne. Hivyo maadui wale watatu bado wapo.

Huoni kwamba unakubali hoja kwamba serikali iliopo madarakani imeshindwa kuondoa maadui hao watatu/wanne kwa miaka yote iliyokuwa madarakani?
 
watu kama vile wamechqanganyikiwa sijuwi ccm imewafanya nini asilimia kubwa ukiwauliza watu kuhusu ccm wanakuwa na majibu ya hasira dhidi ya ccm na hasira ambayo haiwezi kwisha kwa miezi 12 au zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…