Lowassa ndani ya nyumba

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,521
Reaction score
96,267
Waziri Mkuu,aliye achia ngazi kwa manufaa ya uma ,mh Edward Lowasa anatoa azimio la kumuunga mkono rais juu ya hotuba yake ya kuhusu Eac
 
huyo mtu sipendi hata kumsikia
 
naona hili tamko kama limekaa kisiasa zaidi limeandaliwa mahususi kumjenga Lowasa na kuwamaliza membe na sita kwa vile awali walisema kuwa tanzania inasubiri talaka.
 
wapo kwenye mchuano mkali sana hawa watu sijui ngoja niendelee kuitunza kadi yangu ya kupigia kura kama mboni ya jicho panapo majaaliwa niwafyeke
 
Mheshimiwa Edward N.Lowasa, Mbunge wa Monduli na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu ktk awamu ya kwanza ya uongozi wa Rais anayemalizia muda wake sasa Jakaya M.Kikwete. Nilifuatilia mchango wake alioutoa bungeni majuzi alipokua anachangi hoja moja wapo bungeni Dodoma. Kwanza alijikita moja kwa moja kwenye hadhira ya kuutaka Urais ujao. Amejenga kujiamini ili kuushawishi uma kuwa yeye ndio 'Action Man' (mtu wa maamuzi) pekee nchini anayepaswa kupewa ridhaa ya kuongoza umma. Alionekana wazi kutoridhishwa na ukimya uliokuwa umetanda nchini dhidi ya sitofahamu ya EAC. Alipigia Chapuo SADC, na ukanda wa biashara Kongo na kuonekana wazi kuichana EAC. Swali hapa linakuja iweje tena leo anakuja na hoja ya kumuunga mkono Kikwete baada ya hotuba yake kwa umma kupitia Bunge na msimamo wa Taifa kuendelea na EAC. Kumbe Lowasi ni sawa na mimi tu wote tuko nyuma ya PAZIA. Hongera Kikwete kwa kumaliza ukimya.
 
Mi naona hata Ngeleja anausaka urais kwa nguvu zote. Kwa kwwli 2015 itakuwa kivumbi. Inawezekana visisiem vingi vidogo vikazaliwa.
 
Huu uzi unafundisha sana. Kumbe wengi tunawapenda au kuchukia watu kishabikishabiki tu. Hakuna mwenye sababu za msingi zilimfanya ampende Lowasa licha ya kuwa alikuwa anamchukia. Vivyo hivyo watu wanamchukia Magufuli bila sababu na watampenda baadae bila sababu. Kweli wabongo bongo lala.
 
Umenikumbusha mbaaaaaali sana

Viumbe hatari vinavyoweza kumpoteza kwa dakika chache kifikra ni hiki kinachoitwa mtanzania asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…