mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,040
Mimi watz nashindwa kuwaelewa kabisa kwa jinsi walivyompokea huyu fisadi mkuu wa ccm na kumpa hadhi ya juu kabisa eti akagombee urais.hivi anadhani urais ataupata?ashindwe na alegee
Kwa hiyo saivi ile The List of Shame inabadirika na kuwa The List of Fame??????Sawa!! Ila ni ccm hii hii ndiyo iliyopinga vikali Lowassa alipoitwa fisadi na wakina slaa,ni ccm hii hii ndiyo iliyotishia watu kuwa kama kuna mwenye kujua ufisadi wa lowassa na aende kuupeleka mahakamani,ccm ilituaminisha kuwa hakukuwa na chochote cha ufisadi kumhusu lowassa,mwenyekiti wa ccm na rais wa JMT alisema kuwa ile ilikuwa ni ajali ya kisiasa, kauli ya wapinzani ya kutaka awe mahakamani/jela kwa tuhuma zile za richmond ni fedheha kwa kamati ya mwakyembe iliyomtuhumu hivyo bila kuwa na ushahidi wowote wa maana, tazama leo ccm inasema itaenda mahakamani kwa kuwa tu eti lowassa ameichafua kwa kusema ukweli kuwa alikatwa kimizengwe,lakini haikuona haja ya kwenda mahakamani kumfungulia kesi ya ufisadi kipindi kamati ya mwakyembe inaleta ripoti inayomhusisha lowassa kwenye wizi huo,hawakuona haja ya kumhoji,natural justice haikuwa na nafasi wakati huo wala juzi mlipomtuhumu kugawa rushwa, sasa kamati ilisema ni mwizi,wapinzani wakaamini na kuwaaminisha watu hivyo,ccm wakasema si mwizi wapinzani wameamini na kunchukua,ccm imegeuka tena ghafla na inasema ni mwizi!!!! Kha!!! Viongozi wa ccm wajiuzulu tu!! Hawajui wanalosimamia.
Whether shame or fame ccm walimshindwa sawa? Au shame when in cdm and fame when in ccm? Ni nani waliomwita lowassa jembe? Ni nani ndani ya ccm aliyeitwa mzee wa maamuzi magumu? Basi ndiye huyo huyo ndio yuko ukawa sasa!! Endeleeni kumwita majina yale yale mliyokuwa mkimwita huko kwenu! Manake hata huko ukawa pia wanamwita vilevile,tatizo nini?Kwa hiyo saivi ile The List of Shame inabadirika na kuwa The List of Fame??????
Avatar yako haifanani na busara na hekima. Shame on you. Ukawa wanatufanya watanzania mazuzu kweli kweli. Yaani inafadhaisha sana. Ukawa wote ni wachumia tumbo tu jamani looo!!!!
Kwa iyo tuchukue statement yako kuwa whether shame or fame alafu tufanye uamuzi???????Whether shame or fame ccm walimshindwa sawa? Au shame when in cdm and fame when in ccm? Ni nani waliomwita lowassa jembe? Ni nani ndani ya ccm aliyeitwa mzee wa maamuzi magumu? Basi ndiye huyo huyo ndio yuko ukawa sasa!! Endeleeni kumwita majina yale yale mliyokuwa mkimwita huko kwenu! Manake hata huko ukawa pia wanamwita vilevile,tatizo nini?
Kwa wenye uchungu na taifa hili wameliona hili. Kinachofanyika sasa ni sawa na wale wapumbavu wanaosema bora mtoto wangu afe ili niwe tajili. Total insane.