Lowassa kuhamia CHADEMA na kugombea Urais: Ni Ulaghai, Unafiki na Uzandiki Uliotukuka

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,221
26,031
Tanzania na Watanzania tunapitia katika kipindi kigumu nafikiri kuwai kutokea katika taifa letu. Ni kipindi ambacho tunajiuliza kuwa tumwamini nani? Mbona wale tuliojua kuwa ni watu wa kuwaamini nao wamebebwa na nguvu ya fedha??? Tunapitia kipindi ambacho sio kwamba sie ni wa kwanza kukipitia la hasha hata wenzetu wa Italy na Thailand walishawai kukipitia ila tofauti ni kuwa hizi nchi ni za tofauti sana na Tanzania kuanzia kiuchumi hata kisiasa.

Kwanini nasema hivi?
Kutokana na hali halisi kuwa Tanzania ni nchi ambayo kimaendeleo tunaweza kusema kuwa ni kama ndege iliyo kwenye njia yake kuelekea kuruka, yaani ni nchi ambayo inafunguka zaidi kifursa kiasi ambacho kwa watu wakubwa wa ndani na wa nje imegeuka kuwa sehemu wanayoiangalia sana. Hii imetokana na fursa za maliasili, madini ambayo inasemwa hadi leo yaliyochimbwa ni asilimia 10 tu na mafuta na gesi.

Kwa matajiri na watu wenye nguvu ya kifedha ambao wanataka waendelee kumaintain status quo yao au wanataka waendelee kukua zaidi na zaidi wanajua kuwa wakiweza kuikamata Tanzania leo basi watakamata hizi fursa zote na siku ya mwisho Forbes itawatambua.

Matajili ni watu wenye akili sana na wanajuaga sana mahali popote pale, ukitaka kula mema ya nchi basi kikubwa ni kwa gharama yeyote ile muwekeni mtu wenu kwenye top post ya hiyo nchi. kwa nchi zingine top post kiserikali ni waziri mkuu kama italy na Thailand ila kwa Tanzania ni RAIS. Ukishamuweka tu malengo yako yote ya kibiashara yatatimia.

Kama nilivosema hapo juu kuwa yanayotokea leo Tanzania sio yameanzia hapa la hasha yameanzia huko mbele na mfano mzuri ni italy ambapo kulikuwa na Bilionea ambaye sasa yuko jela anajulikana kama Silvio Berlusconi na Thailand kulikuwa na bilionea anayejulikana kama Taksin Shinawatra. Kwa msio wafahamu hawa watu hawa ni matajili wakubwa sana na walitumia sana nguvu yao ya pesa kutengeneza ushawishi wa kisiasa kwenye nchi zao, kwa Thailand ilibidi jeshi(system) iingilie kati kumuondoa Shinawatra ila kwa italy ilibidi wapate msaada wa nje ili kuweza kuiharibu syndicate ya bwana Silvio Berlusconi na hata leo hii wanashukuru ni bora ameondoka na yuko jela.

Hali ilivokuwa Tanzania sasa:
Kwa hapa Tanzania kuna syndicate ilishajipanga tangu mda kuwa lazima mwaka 2015 tuweke mtu wetu. N i kundi kubwa lenye nguvu ya pesa tena sio kawaida ni sana ambalo lilijipanga kisawa sawa kuwa lazima tuikamate CCM na tuiforce imuweke mtu wetu. Walijipanga vizuri sana kuanzia makanisani, misikitini, bodaboda hadi vyuo vikuu. KWA KIFUPI walimpa mtu wao fedha nyingi sana ili ajenge ushawishi kwa sababu walijua weakeness kubwa ya watanzania/waafrika(na binadamu kwa ujumla) ni fedha. Zilitolewa hela zisizo za kawaida makanisani, misikitini na hata meeneo mengi kama bodaboda na vyouni, walitafutwa wahariri wa vyombo vya habari wakaongwa fedha nyingi sana na kwa kifupi hawa watu waliweza kununua asilimia 90 ya vyombo vya habari.

Walivofika dodoma walikuwa na uhakika kuwa iwe isiwe lazima nguvu ya fedha itatamalaki kiasi ambacho mtu wao atapita ambaye ni EL. ila hamadi kilichotokea dodoma kila mtu anakijua kwa sababu CCM walishtuka kuwa tunakoelekea tutakuja kulaaaniwa na vizazi vyote vijavyo vya watanzania kwa sababu hawa watu sio watu wazuri na hawana nia njema na mama Tanzania ikabidi kutokana na hali ilivokuwa waseme inatosha na lazima kweli ya haki ishinde dhidi ya fedha chafu.

Wakamkata na wakaamua kumchukua mtu aliyekuwa hana makundi, hajawekwa na wenye fedha na hana wa kumlipa fadhila wakati atakapokuwa anaendesha nchi yaani John Pombe Magufuli mambo yakatulia.;

Kwa upande wa hawa watu kibaya zaidi hawakuwa na plan b kwa upande wa CCM, walitawanyika ila kiongozi wao na mtu wao kwa sababu yeye nia yake kuu ni kuingia magogoni tu wakasema lets go the other side. Walijua wanayo pesa na wanayo pesa na kiukweli kwa upande huo hamna anayeweza kushindana nao, wakaenda kuwashawishi viongozi wa upinzani. Kuna taarifa zinasema kuwa walikubaliana kugharamia kampeni yote kuanzia uraisi hadi ubunge ya upande wa pili, walikubaliana kuwawezesha upande huo kifedha na viongozi wa upande huo waliwekwa sawa kifedha.

Ukiliangalia hili suala juu juu unaweza kufikiri ni jambo la kawaida sana ila hapana. Kuna kitu hapa ambacho watanzania lazima waamke na wakione nacho ni hadi hawa wameweza kuingiliwa na fedha???????

Katika dunia ya leo mwanasiasa anatakiwa awe mtu predictable na asiwe mnafiki kiasi ambacho mtu aliyempa kura anatakiwa awe na uhakika nae kuwa nilimpa kura huyu mtu kwa sababu anaamini katika A, B, C na hizo ndo zilizonishawishi mie kumuamini na kumpa nafasi kwenye akili yangu.

Mwaka 2007/8 Chama kilichojijengea sifa kubwa nchini Tanzania Chadema kilitoa kile kilichoitwa The list of Shame ambapo walitoa majina ya watu 11 wao waliowataja kuwa ni mafisadi, wanaolitafuna taifa na kuliangamiza taifa. Walisema kuwa wana ushahidi kamili usio na shaka juu ya hawa watu na kama hawa watu wanabisha waende mahakamani. Walisema hawa watu hawastahili kuwa mitaani sehemu wanayostahili kuwa ni jela. Na hiki ni kitu kilichowapa public trust ya kiwango cha juu kabisa, hiki ni kipindi ambacho chadema ndo ilianza kujijenga mioyoni mwa watanzania kuwa ni wakombozi wa kweli, watu wanaongea ukweli, sio waongo na yote wanayosema ni kweli tupu kwa hiyo ndo watu wanaostahili kupewa nchi.

Chadema hawakuishia hapo walizunguka nchi nzima kwenye mikutano na kampeni mbalimbali wakiendelea kuitaja iyo THE LIST OF SHAME, ambayo no 9 alikuwapo Edward Lowassa.

Sio huyo tu washirika wa Lowassa yaani mzee wa vijisenti na the Kings Maker Rostam Azizi washawai kutajwa na Chadema kuwa ni watu mafisadi na wasiofaa.

Kichwa cha mada kinasema ni ulaghai, unafiki na uzandiki kwa sababu pamoja na hiki chama kumtaja huyu mtu ila viongozi wao wamekula matapishi yao wenyewe na leo wamempokea huyu Lowassa na wanamnadi kuwa ni mtu safi, mwenye weredi na anayefaa.

Kuna kitu kimekuwa kikiendelea kwa hawa viongozi kutoa majibu mepesi eti siasa ni dynamics na sio static eti mtu unaweza kubadirisha gia angani wakifikiri watanzania ni mambumbumbu sana kiasi ambacho hawawezi kuhoji na hawafuatilii mambo yanayofanyika duniani huko.

Napenda kuwaambia viongozi wa Chadema kuwa katika siasa za 21st century mwanasiasa akisema jambo alafu ikitokea otherwise au ikitokea tofauti na alivosema au kuuaminisha umma uwa anajiuzuru. Mfano wa haya ni kama ilivotokea juzi Scotland pale waziri mkuu na kiongozi wa chama cha Scotish National Party alipojiuzuru nafasi zake zote baada ya kile kitu alichokuwa akiwaaminisha wascotland kuwa nchi yao inafaa kujitenga kufeli kwenye referundum. Sio huko tu hata England Ed Milband nae baada ya chama chake kushindwa kwenye kushawishi kitokana na sera zake alibidi ajiuzuru. Huu ndo ustaarabu mpya kwenye siasa kwa kifupi siasa za dunia ya leo ni kuwa endapo mwanasiasa ukisema jambo fulani lile jambo likija tokea tofauti na ulivouaminisha umma au chama chako inabidi ujiuzuru.

Sasa kwa Chadema na ukawa what thet were supposed to do ni kuwa kabla Lowassa hajatambulishwa rasmi au soon after kutambulishwa wale viongozi wote waliokuwa wanauaminisha umma na kudai wana ushahidi juu yake kuwa ni fisadi walitakiwa kula matapishi yao kwa wao kujiuzuru nyadhifa zao zote ndani ya chama chao na kuomba msamaha kwa jamii ya Tanzania kwa upotoshaji mkubwa walioufanya.

Ila kwa majibu mepesi wanayoyatoa kama aliyatoa jana Mchungaji Msigwa kwenye kipindi cha Madamoto, kama aliyoyatoa Lema au kama aliyoyatoa Lissu na ziadi na zaidi kama aliyoyatoa mwenyekiti wao Freeman Aikael Mbowe wakati anamkaribisha Lowassa basi its obvious kuwa HUU NI ULAGHAI, UNAFIKI NA UZANDIKI ULIOTUKUKA.

Nakataaa kudharauliwa na viongozi wa ukawa kuniona mie siwezi kufikiri ila wao ndo wanaweza kufikiri kwa niaba yangu.....

Tukutane Oktoba.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA
 
CCM ing'oke kwanza mambo mengine baadae!
CCM inaundwa na watu wasafi na wachafu, kibaya zaidi wale wachafu mnawachukua mkiwaacha wasafi ndani ya CCM alafu eti muing'oe CCM ya wasafi kwa kuwatumia CCM wachafu????? Samahani sana

Nakataaa kudharauliwa na viongozi wa ukawa kuniona mie siwezi kufikiri ila wao ndo wanaweza kufikiri kwa niaba yangu.....

Tukutane Oktoba.
 
Mkuu Lord denning uwe una summarise mabandiko yako badala ya kuandika kama unaandika hukumu!!! Fanya case summary mkuu ili tuweze kusoma na kuchambua; nadhani umenielewa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Lord denning uwe una summarise mabandiko yako badala ya kuandika kama unaandika hukumu!!! Fanya case summary mkuu ili tuweze kusoma na kuchambua; nadhani umenielewa.
Hahaha Asante Mkuu, nimekusoma, unajua tushazoea kushusha mavituz huku kwenye field yetu sasa tunapitiwa mda mwingine.
 
Hakika ni ulaghai wa wazi kabisa hata mtoto anayenyonya analiona hilo. Hapa kwa kweli kama hao viongozi wakiongozwa na Dr. Slaa wanataka kuzitendea haki nafsi zao wanatakiwa kujuzulu mara moja na kuachana na chama cha mafisadi. Wanatakiwa wasutee na nafsi zao hasa ukizingatia Msigwa ni mchungaji na slaa ni padre
 
Asante nalipokea ila tukutane Oktoba.

Pitia katuni ya kIPANYA leo kwenye gazeti la Mwananchi kuna ujumbe wenu mzuri sana.

chadema haiisi kwa kufuata katuni ya kipanya...kipanya hatoi dira ya nchi....mliambiwa juzi politics is a game of dynamics...tumebadilia gia juu kwa juu.....mlitaka kuligeuza taifa hili shamba la bibi ..safari hii mtanyooka tu
 
image.jpg
 
chadema haiisi kwa kufuata katuni ya kipanya...kipanya hatoi dira ya nchi....mliambiwa juzi politics is a game of dynamics...tumebadilia gia juu kwa juu.....mlitaka kuligeuza taifa hili shamba la bibi ..safari hii mtanyooka tu
Endeleeni tu kuwafanya watanzania wazezeta kwa majibu yenu mepesi hayo.

Tukutane Oktoba.
 
Nashangaa CHADEMA inavyosema haitaki kuongozwa na CCM wakati mgombea Uraisi wanaemtegemea na tumaini lao ni kutoka CCM na bado wanakuja wengi kutoka CCM. Hii ngoma CHADEMA wanayoicheza na kujiaminisha ni wajanja wamechemsha na wataendelea kutawaliwa na CCM ndani na nje ya chama Chao
 
Viongozi hawa waliuaminisha umma wa watanzania kuwa Lowassa ni fisadi,tena fisadi anayedhoofisha maendeleo ya Tanzania,fisadi ambaye utajiri wake haujulikani anautoa wapi, fisadi ambaye anamiliki majumba hadi Ulaya,
fisadi ambaye ndiye alishiriki kwenye sakata zima la richmond.

Hata wakamtaja kwenye ile "list of shame" wakasema wanaushahidi wote hata kusema watampeleka mahakamani.

Viongozi hawa hawa wakazunguka nchi nzima kwa mbwembwe nyingi wakiimba wimbo uleule.

Viongozi hawahawa waliposikia Lowassa kachukua fomu ya uraisi kupitia CCM, wakanukuliwa wakisema kuwa "badala ya mafisadi kuwa jela Leo wanachukua fomu ya uraisi" .

Juzi tar.27/7/2015 viongozi wa ukawa wametutungia wimbo mpya sisi watanzania, watanzania ambao wengi wetu sikuizI tunajielewa, watanzania ambao tuliamini kabsa maneno ya UKAWA. Leo UKAWA wanatuambia kuwa Lowasa sio fisadi.

Anafaa kuchukua fomu ya uraisi sio kwenda jela tena, Amekuwa msafi to the maximum that amewazd hata baadhi ya viongozi wa ukawa ambao walitajwa kugombea uraisi.

Leo anachukua fomu ya kugombea urais yule mtu waliotuaminisha kuwa ni fisadi na mwizi kumbe sio, hivyo basi kuonyesha dhana uwajibikaji kwakuwadanganya WATANZANIA.

Ninaomba Viongozi wa UKAWA mjiudhuru na kuwataka radhi watanzania radhi kwa kuwadanganya kabla ya Tarehe 25 OCTOBER.

Nawasilsha.
 
Back
Top Bottom