Love besides time

AmbaB

Member
Joined
Sep 1, 2016
Posts
51
Reaction score
27
Na Ambangile, B

Muda wako ni kitu cha msingi sana ambacho familia yako inahitaji toka kwako, mume wako anashida saana na muda wako kuliko pesa unayoweza kumpa, halikadharika mkeo anashida sana na muda wako pengine kuliko kitu kingine chochote toka kwako, mpe muda[emoji3514]

Kaa na mkeo, pigeni urabu pamoja, ni TIBA HII[emoji3514]

Kaa na mumeo, mpe umbea wa mchana kutwa, msimulie kuhusu majiran zenu wanavyoenenda asipokuwepo, Semelea kwake[emoji3514] ni palizi ktk ndoa yako[emoji108]

Baba, chukua Henessy, pata Savannah pamoja na mkeo mkiws nyumbani kwenu huku mkiwajadiri watoto wenu na uzao wenu wote, maisha ndiyo haya sasa[emoji3514]

Kijana nikueleze ukweli [emoji112] ,ukiwa bado unahangaika na maisha ya kutafuta pesa, jitajidi saana kuwa na muda wa kutosha wa kukaa pamoja na mkeo[emoji3514] tenga muda na wala achana na insta wala facebook hata whatspp wakati huo, kaeni nje kunyweni pombe pamoja, tafakarini pamoja na wala asikuone upo busy na cm, jiweken karantine pamoja, NI IBADA HII[emoji3514] hata mkilewa Mungu atawasamehe....

Ulivyofika kwenye ndoa, rafiki yako mkubwa ni mmeo/mkeo, punguza ule muda wa kila siku upo na Mwakatuma Nwakaupo naPaul S John, Abrahamu Nzowa ....wakati wa kukaa na mkeo uwe mwingi zaidi japo usiwasahau washika dau hawa watakaoshika jembe kukuzika[emoji123]

Dadaangu, ni kweli upo busy sana na kazi, ofisn kwako, lkn kumbuka kutafuta muda wa kuwa pamoja na mumeo, tafakari hata uumbaji wa dole gumba la mumeo, mcheke kwa nn anavidole vibaya namna hiyo, hebu sifia nywele pilipil za mumeo, na ndevu zake zisizokuwa na ushirikiano kama waarabu wa Dubai, namaanisha Mjue vema mumeo physically[emoji3514]

Pambaneni kuyatafuta maisha msije sahau kupalilia uhusiano wenu wala kustawisha kwa maji ya uzima ambayo ni MUDA, Muda wenu ni asset kuu ya ndoa yenu, kupendana kunaanzia na muda unaojivunia kushinda na mwenza wako, je upo tyr kupata harufu ya mkeo/mmeo kutwa nzima ?Ni upendo wa Agape huu [emoji123][emoji3514]

Kwa kipindi hiki cha Covid 19 ,msisahau kuweka sanitizer mezani(msije mkainywa mkilewa[emoji849]) ,kumbushaneni measures za kujikinga na janga[emoji3514] zaidi kaeni pamoja kwa Muda, MUDA NI TIBA YA NDOA [emoji120]

ASIWEPO MTU WA KUTAMKA NAPOTEZA MUDA KUKAA HAPA NA WEWE[emoji735], hata kama hamna pesa huo ni uwekezaji tosha kwenye ndoa yenu.

Invest plenty of time with your husband/wife[emoji3514]

Bishaneni, ongezen weledi pamoja....Chukua Cm muoneshe post ya Ambangile then endeleen kupombeka mpaka muda mtakaoitwa mkapate chakula [emoji2936]

MUDA MUDA MUDA =MALI[emoji3514][emoji3590]

Na Ambangile[emoji123]
 
Yupo wapi Hannah aliyedai mnawekeana bet kila mwezi ili mmoja akideviate basi mwingine ale pesa... Watu wanajali muda mama....Ukiingia kwenye deep love hata hayo mengine hutayawaza.
 
Yupo wapi Hannah aliyedai mnawekeana bet kila mwezi ili mmoja akideviate basi mwingine ale pesa... Watu wanajali muda mama....Ukiingia kwenye deep love hata hayo mengine hutayawaza.
Kwahiyo umekuja kunitupia dongo huku?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hapo umefariji wenye ndoa zao

Embu fungua uzi unifariji mm niliyeumizwa

😎😎😎😎😎
 
Hapo umefariji wenye ndoa zao

Embu fungua uzi unifariji mm niliyeumizwa

😎😎😎😎😎
Nipe case yako specifically...........eeeh ...usije kuta naanza kukuumiza mm mwenyewe...love has no formula dear
 
Kwamba nikae na Mke wangu aanze kunipa umbea wa mchana kutwa kuhusu kuhusu majirani?
Huo muda sina na akifanya hivyo namvunja moyo.
 
Eeh..wa kwangu nikimsifia handsome hapendi.. nisubiri apate kitambi nianze msifia huenda akafurahi..πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…