Habari ndugu zangu, mimi ni mhitimu wa shahada ya Sayansi ya Elektroniki na mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nimemaliza mitihani yangu ya mwisho mwezi huu, nikiwa nasubiri matokeo na cheti nilikua naomba kama kuna mtu anaweza nisaidia nafasi ya kufanya kazi ya kujitolea katika kampuni yake/yao ili niweze kuongeza ujuzi katika fani husika. Katika miaka yangu ya chuo niliopitia nina wastani wa kupata GPA ya 4.0 kati ya 5.0.
Naimani umu JF kuna watu wa rika mbalimbali na wenye ujuzi mbalimbali hivyo naimani mtanisaidia. Kwa ataetaka CV na Provision Statement of Results naweza kumtumia kupitia ujumbe mfupi(PM). Ahsanteni.