Liwalo naliwe

pole naniii unamanisha huna utulivu kwenye ndoa sio?basi mumbe Mungu wako sana ukuondoe kwenye hilo fungo

Bahati mbaya sina hiyo Ndoa! Ndio natafuta huyo wa kunikamata anitengenezee mambo nikamatike!
 
Bahati mbaya sina hiyo Ndoa! Ndio natafuta huyo wa kunikamata anitengenezee mambo nikamatike!

Sasa we kwa nini unataka ukamatwe usipendi kwa hiyari yako?dawa zikiisha?au hujui kupenda au huna ela shauri zako tafuta pesa upendwe!natania japo namanisha
 
mwenzio umemwambia uovu wako kakusamehe hapo hapo, halafu wewe umempa muda ufikirie na kufanya auamuzi kama utamsamehe..unachekesha kweli!! haya, fanya maamuzi utakayoyaona ni sahihi!!
 
Sasa na pesa zikiisha?

Sa zikiisha si mtakuwa mshaingia ndani kwa hiyo chohote kitakubalika si unaona mlokole nyama ya d*d* kala na amejua na bado kashindwa kuchukua uamuzi? kama alivyofanya mke wa huyu mlokole kwa hiyo mtaendele kuishi pesa. hazivunji ndoa, hardly ,ila pa kuanzia lazima uwe nazo
 


Yaani ndugu yangu nadhani hujaelewa maana ya Wokovu(kuokoka).Kuokoka ni kujisalimisha kwa Yesu, Kumkiri Yeye kwa kinywa chako kuwa ni Bwana. Kuyaacha yale yote zamani ulifanya(Kuwa kiumbe kipya ya kale yote yamepita) Kubadilika kutoka katika hatua moja kwenda katika hatua nyingine nzuri zaidi. Kiafya, kimazingira, kiuchumi na kielimu. Sasa wewe naona unataka urudi Misri wakati uko safarini kuelekea kanani.

Sikuzote ndani ya wokovu jifunze kusamehe na kusahau,Mkeo huyo ametubu kwa kile alichokutendea kama wewe ulivyotubu uliyoyafanya kinyume na mpango wa Mungu.Kwani usipo samehe Umeuacha wokovu maana maandiko yanatuamuru
"NINYI KILA MSIMAMAPO NA KUSALI, SAMEHENI, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehi, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu" (Marko 11, 25, 26 ).

Maana yake, kutokusamehe kunahesabiwa kuwa ni kosa mbele za Mungu, na ni dhambi inayotutenga na uso wa Mungu, ili tusijibiwe maombi yetu toka kwa Mungu. Kutokusamehe ni uasi, Dhambi ni uasi (1 Yohana 3:4) Dhambi ni kuasi maagizo ya Mungu.

Lakini kama ulimpokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako unatabia ya kusamehe ndani yako.Maana maandiko yanasema "Bali wote waliompokea (Kristo) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu." (Yohana 1:12,13)

Sasa nakuomba ndugu yangu kama uliokoka kwa kumaanisha unatabia hii ndani yako:
Kuyafuta makosa na kutoyakumbuka tena ni tabia ya Mungu ambayo imo ndani yako sasa.Ulipompokea Kristo moyoni mwako na kumkiri kuwa ni Bwana wa maisha yako, pia ulipokea ndani ya moyo wako tabia hii ya Mungu ya kufuta makosa na kutoyakumbuka.Hii ndiyo tabia inayotakiwa ionekane katika maisha yako unapokosewa na mtu.
 

Ndipo Petro akamjia Yesu na kumwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?”
Yesu akamjibu, ‘‘Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.’’ Mathew 18: 21-22
 
Nnachokuhurumia ni pale ambapo utakuta humpendi from moyoni uliona sababu ya hizo dawa lazima uwe na mtihani sana lkn kama unampenda basi samehe tuu
 
hii ni stori au ni laivu laivu bila chengaaaaa....?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…