Habari zenu wanajamvi.
Leo ninapenda kuchukua nafasi kuwashukuru nyote kwa kuwa na imani na Timu ya Tanzania ya mpira wa miguu tangu hapo awali mpaka tamati yake hii Leo.
Ku... la bibi yako
Licha ya kutambua wazi kuwa hatutafika popote kwenye michuano hii, bado mkaendelea kuamini kuwa "Kuku atameza Papai".
Leo ndio tunaenda kufunga pazia la michuano hii kwa upande wa timu yetu kwa kichapo cha "bao moja kwa nunge".
Naomba tuendelee kuwa pamoja na timu yetu hata kama tu najua kabisa kuwa tunaenda kufungwa. Maana hakuna namna pekee ya kuonyesha uzalendo zaidi ya kukubali hali halisi.
Iandaeni mioyo yenu maana Imeandikwa. "Mwana wa Adamu atashinda mechi chache za kwanza, siku ya pili atakula kichapo na siku ya tatu atapaishwa na Lesotho" Taifa 4:2-0.
Kwanini unaitabiria vibaya timu ya taifa lako ?Habari zenu wanajamvi.
Leo ninapenda kuchukua nafasi kuwashukuru nyote kwa kuwa na imani na Timu ya Tanzania ya mpira wa miguu tangu hapo awali mpaka tamati yake hii Leo.
Licha ya kutambua wazi kuwa hatutafika popote kwenye michuano hii, bado mkaendelea kuamini kuwa "Kuku atameza Papai".
Leo ndio tunaenda kufunga pazia la michuano hii kwa upande wa timu yetu kwa kichapo cha "bao moja kwa nunge".
Naomba tuendelee kuwa pamoja na timu yetu hata kama tu najua kabisa kuwa tunaenda kufungwa. Maana hakuna namna pekee ya kuonyesha uzalendo zaidi ya kukubali hali halisi.
Iandaeni mioyo yenu maana Imeandikwa. "Mwana wa Adamu atashinda mechi chache za kwanza, siku ya pili atakula kichapo na siku ya tatu atapaishwa na Lesotho" Taifa 4:2-0.
Mkuu....Kwanini unaitabiria vibaya timu ya taifa lako ?
Au wewe si raia wa nchi hii.
We mapenzi yako ni kwa timu ya Yanga Afrikans pekee.
Kabila gani wewe ?
Wana wachezaji lukuki kuliko Tanzania wanao cheza soka la kulipwa nje ya nchi....Lesotho kieneo nikama mkoa wa Mara. Ni kamamkoa wa 17 kwa ukubwa Tanzania.
List of Tanzanian regions by area - Wikipedia
Geography of Lesotho - Wikipedia
Kwa wingi wa watu nchi nzima haifikii hata nusu ya watu wa Daresalaam. Ni kama idadiya watu wa wilaya ya Kinondoni tu.
Kufungwa na ki nchi hiki ni aibu.
Bado hujasemezana nami kwenye suala la msingi nililoliulizia.Wana wachezaji lukuki kuliko Tanzania wanao cheza soka la kulipwa nje ya nchi....
Mbona huwa hutabiri Taifa Star inashinda kwenye mechi za ushindi ?Mkuu....
Si suala la kutabiri mabaya...Kwani nani alikuwa na hakika kuwa cream ya timu ya mpira wa miguu ya Tanzania angemfunga timu ya mseto ya Zambia...?
Huu ni uhalisia tu.
Uzembe wetu...Bado hujasemezana nami kwenye suala la msingi nililoliulizia.
Inakuwaje ki nchi kidogo hicho, chenye eneo kama la mkoa wa Mara tu, mkoa wa 17 kwa ukubwa Tanzania, na chenye watu kama wilaya ya Kinondoni tu, kiwe na wachezaji wengi sana wanaocheza soka la kulipwa nje kutuzidi Tanzania?
Lesotho kwa idadi ya watu tumewazidi karibu mara 30.
Kwanini wao si wazembe na sisi ni wazembe?Uzembe wetu...