Hiyo ni yako akiba, ama ya ndugu uliiba,
Uliachiwa na baba, ama ya mama mahaba,
Hicho kibubu si haba, kiache kijaze kibaba,
Mapenzi upofu.
Hata boma ujengalo, kumbe kisa ni hidaya,
kakubana mpogolo, imeshakutoka haya,
utageuka kipolo, ukome maisha haya,
Mapenzi upofu.
Mapenzi kweli upofu, apendae hupofuka,
Akili upata ufu, kuelewa hufutika,
Mapenzi yakija kifu, wazimu unafumka,
Iko siku utajuta.