Ziara ya Kerry haina dhimira ya kutatua mgogoro wa Syria bali ni kuishawishi Russia kukubali Assad ang'olewe madarakani. Na ndiyo maana US wameanzisha vuguvugu la kuipinga serikali halali ya Assad, kwa kuwasaidia. wapinzani na vikundi walivyoviita. vya msimamo wa wastani. Wamewasaidia kufanya mapinduzi. ila Assad akaomba msaada Russia kuzima ndoto zao. Baada ya hapo US wakaona wasapoti mpango wa kusitisha mapigano. Huku wakiendelea na mapambano dhidi ya magaidi wa IS na Al Nusra Front.
US wanataka kumng'oa Assad kwa nguvu ili wapate maslahi huko Syria, maana Assad ni kikwazo kwa maslahi yao. Russia nao wanamaslahi huko Syria na ndiyo maana wakaamua kumsaidia Assad ili walinde utawala wake unao wezesha Russia kunufaika. Haya ni mazungumzo ya kugawana maslahi baina ya Russia na US ndiyo maana utaona wanafanya mazungumzo yabayohusu Syria bila ujumbe wa wawakilishi wa Syria. Utaona kuna mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu huko Geneva.
Haya mataifa makubwa hususani yenye kura ya turufu (Veto power ) kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa yanachochea na kuvuruga sovereignty ya mataifa mengine , wanatengeneza matatizo na wanaenda kwenye baraza la usalama UN kujadili na kuamua kutoa suluhisho la matatizo ya mataifa mengine bila kuyajumuisha.