Nionavyo hapa TZ kuhusu siasa za vyama vingi ni sawa na mtu akuambie ubuni kanuni ya kubadili maji chumvi baharini kuwa maji baridi.
Abishae na aseme hapa ni kwa jinsi gani chama kilicho shika usukani hivi sasa kitapokonywa usukani.
Waliotengeneza mfumo huu na namna ya kudhibiti bahari isiwe maji baridi wana sababu na nyingi ni nzuri tu kulingana na nyakati.
Vyama vya upinzani huenda vinajua ukweli huu, huenda vinaendelea kufurukuta kwasababu za ubahatishaji. Kwamba, yanaweza tokea makosa ya kiufundi chumvi ikawa sukari.
Ndio maana kuna matukio ya watu kutoka upinzani na sijui ni kwenda au kurudi walikotoka na baadhi ya vyama kuonekana ni vyama pandikizi.
Ni maoni ya raia wa kawaida tu, msijishughulishe sana kufuatiliana au kushambuliana.