Lema kuiteka Muheza kesho

JERRY

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
630
Reaction score
504
Mbunge wa jimbo la arusha mjini mh. G.lema kesho ijumaa anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika uwanja wa jitegemee mjini muheza ikiwa ni ufunguzi rasmi wa kampeni iliyopewa jina la chadema ni msingi.
Katibu wa cdm kanda ya kaskazini amani golugwa alisema jana kuwa mkoa huu umeteuliwa wa kwanza kufanyika mkutano huo kwa lengo la kampeni hiyo kufika katika ngazi za chini , alikodai wananchi wake wamefunikwa blanketi jeusi na wabunge wa ccm (by burhani yakub , mwananchi)
 

Nakushukuru Amani Golugwa.
 
Nendeni mpaka bombani,tongwe,km7,ubembe,matopeni,bwembera nk,watu wanataka kuwasikia mnasema nini!
 
ccm mwaka huu kazi mnayo,japo wabishi ajabu ila mpera mpera mnaoupata Allah anajua


kila la kheri cdm,sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,nashukuru toka awamu ya kwanza nilikuwepo mpk awamu hii ya 4 ila sikuwahi kuona chama makini kama chadema.
 
safi sana , Nimefurahishwa sana na kauli mbiu yao ya ' KUWAFIKIA WALE WOTE WALIOFUNIKWA BLANKET JEUSI NA WABUNGE WA CCM ' Pipoooooooooooooooooz !!!!!
 
Pls lema njo had amani hali ni mbaya sana maziwa ya wananchi yanamwagwa chini kisa gari yashindwa kuja barabara mbovu lt 7000 juz zimepotea kila mmoja analia
 

itakuwa na impact sana kama atajikita kwenye ngazi za kata ikiwezekana na vijiji pia blanket la huko halipitishi hata hewa.
 
Wanabodi ukweli unabaki pale pale ukombozi wa fikra unao enezwa na M4C nchi nzima ni mithili ya Tsunami na hakuna awaye yeyote awezaye ku-uzuia.

Endapo Magambaz hawataki kubadilika na kusoma alama za nyakati, basi Mabadiliko yatawabadilisha automatically.
 
Huo mkoa ulolala lakini pana mwelekeo wa kuamuka mfano Lushoto, bigup aluta continua mapambano bado yanaendelea.
 
Hongereni CHADEMA kwa hatua hii murua.
Lema unakaribishwa Tanga kwa Wagosi wa ndima na kaya. Hili ni la msingi sana kwa CDM ili kuzidi kuijiimarisha hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.

Ni aibu kwa mkoa mkubwa kama Tanga kutokuwa na Jimbo hata moja la upinzani. Hii inaonyesha kuwa CCM ameshateka mawazo ya Wabondei,Washambaa,Wazigura,Wadigo na Wambugu. Tanga wanatia aibu kwa kuonekana wamezubaa na wako nyuma ya wakti kwa kuiendekeza CCM kwa sababu ya kudeka kwingi.

TANGA TUMIENI FURSA YA UJIO WA CHADEMA ILI MUAMKE TOKA USINGIZINI. TUNATAKA TANGA MWAKA 2015 MFUTE MAWAZO YA ATI KUWA MKOA WA TANGA NI NGOME YA CCM!!!

TANGA WAKE UP AND SHINE!
 
Tuamshie hao watu wa tanga ....Kanda nyingine mchangamke- huku mbagala napo jumapili kuna mkutano mkubwa zakiem- karibuni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…