Ok. Kwa mujibu wa katiba yetu, mahakama inapaswa kuwa huru. Iweze kutoa haki bila woga wala upendeleo (without fear or favour). Hivyo dhana ya kutojadili mambo yaliyoko mahakamani ina lenga kutokuathiri mwenendo wa kesi. Hata hivyo linalozuiwa ni kujadili (kujenga hoja juu ya mwenendo wa kesi/kujadili jinsi kesi inavyoendeshwa) na siyo kuzuia mtu kutaja matukio yaliyowahi kutokea ambayo yameripotiwa mahakamani. Mfano, huwezi kumzuia mke wa msigwa asiseme mumewe amewahi pigwa. Hivyo upinzani kulaani matukio yaliyofikishwa mahakamani, mf utesaji wa ulimboka, hakuingilii uhuru wa mahakama. Tatizo ni uchama, ambapo hata AG amesahau kuwa amewahi kuwa jaji badala yake anaact kama katibu mwenezi wa shina flani la ccm!