Mbona unawaulizia hao washikaji Ulizia Alikiba Alikosea wapi mpaka leo hii aanze kupambana na Diamond?????habari wadau..
nazani wote tunaona kishindo alichokuja nacho dogo diamond plutnumz toka wimbo wa mbagala ulivyomtoa... hajarudi nyuma tena ni hit by hit mpaka kushika tanzania nzima na baadae akaanza tawala east africa na then africa nzima wakamjua balaa lake...
nawaza tu wasanii wakubwa waliotawala mziki wetu miaka ya nyuma kina lady jaydee, proff jay, juma nature, inspekta haroon, wao walikosea wapi...
mbona hawakusumbua hata kenya na uganda watukubali mziki wetu...
je diamond ni ana skills kubwa za mziki zaidi yao au ni ana bahati ya mafanikio..
nasikia remix ya namba one ile na davido... diamond alimshawishi davido akubali kwa kumlipa usd 5000... je kina juma nature enzi zao za peak wangekubali kumlipa msanii wa nje hata milioni moja tu ya madafu ili akubali kushirikishwa??
kwani ali kiba alimtafufa R kelly kama mtoa mada anachomaanishaZamani walikuwa wanafanya mziki mzuri hivyo hawakuhitaji kujitangaza kama anavyofanya domo...ndio maana mpaka leo hujui kuwa kingkiba alishafanya collabo na msanii mkubwa duniani kama robert kelly na huko anakopita domo wao kina ay weshapita na kina sean kingston miaka hiyooooo....na HAWAJITANGAZI WANAACHA MUSIC WAO UWATANGAZE DUNIANI.
Tuzo za Kora zilikuwa zinatolewa kwa kanda kwahiyo ilikuwa rahisi sana kushinda kama unakimbiza kwenye kanda yako! So, hao akina Jide walikuwa wanachukua Best in East Africa. Leo wasanii wa Tanzania wanawekwa TOP categories za Africa.jide alishatwaa mpaka tuzo ya kora pale south
nature alishakua nominated tuzo ya kora ila alishindwa kwenda kupafomu sababu alikosa nauli
kama ni kutoboa hawa watu walipambana mno acha kabisa kuwazungumzia mdau
Kiba hajawahi kufanya collabo na R Kelly bali ilikuwa ni One8 Celtel Project waliofanya ngoma na R Kelly.Zamani walikuwa wanafanya mziki mzuri hivyo hawakuhitaji kujitangaza kama anavyofanya domo...ndio maana mpaka leo hujui kuwa kingkiba alishafanya collabo na msanii mkubwa duniani kama robert kelly na huko anakopita domo wao kina ay weshapita na kina sean kingston miaka hiyooooo....na HAWAJITANGAZI WANAACHA MUSIC WAO UWATANGAZE DUNIANI.
nadhani mkuu umetoa jibu sahihi.Watu wanataja habari za media na social networks! Wanachosahau ni kwamba media na social networks zinatengeneza mazingira sawa Afrika mzima!
Kuna wasanii kibao wa South Africa na Nigeria walikuwa wanafahamika Afrika mzima... wao walikuwa wanatumia FB, Instagram? Twitter?! Jibu HAPANA na kwahiyo social networks ni nyenzo tu! Afrika kote tulikuwa tunategemea radio, TV na magazeti lakini bado wasanii wa Naija & SA walikuwa juu!
Timu ya Diamond ipo very strategic. Kwanza walifahamu muziki wa Tanzania ulikuwa unaishia Kenya; PERIOD. Tanzania kama nchi nayo haikuwa maarufu kwa chochote miongoni mwa watu wa kawaida Afrika! Kwahiyo no body paid attention kwa kinachotokea TZ!
So, collabo za Diamond vs Nigeria & South Africa ndizo zimemfanya atambulike Afrika na hatimae kuitambulisha Bongo Flavor nje ya TZ & Kenya.
Kwa nchi kama Tanzania ingekuwa ngumu sana kupenya Nigeria au hata SA bila ya collabo na hit makers wa huko kwa sababu muziki wetu ulikuwa haufahamiki!
Nigeria ndiyo Marekani ya Afrika na SA ni kama UK linapokuja suala la tasnia ya burudani! Nyimbo zako zikishaanza kuchezwa Nigeria hesabu zitachezwa kote kusini mwa Sahara.
AY alifanya kosa la kimkakati! Alianza kutaka kufahamika US wakati hata Botswana alikuwa hafahamiki! US hakuingiliki kirahisi unless USHIRIKISHWE na hit makers wa huko(sio KUSHIRIKISHA)!
So, siri ni collabo! Ni collabo za Diamond ndio zimetambulisha Bongo Flavor nje ya East Africa na wengine hivi sasa wananufaika na hustle zake. Ajabu ni pale hata baadhi ya wasanii wenyewe wanapojaribu kumponda Diamond kwa kufanya collabo!
Hawa wanasahau kama sio hizi hustle za Diamond probably hadi kesho ingekuwa wanaishia Kenya tu hapo... sana sana Rwanda!
Siku hizi watu wanateleza wanataka kujidanganya ni uwezo wao! Wanasahau miaka 50 iliyopita pia tulikuwa na wanamuziki wakali lakini na wenyewe walikuwa wanaishia Kenya!nadhani mkuu umetoa jibu sahihi.
anaepinga hili ni mpuuzi asiyetambua mchango wa simba kwenye game ya bongo fleva hapa Tz.
ifike mahala simba apewe heshima yake.