Lady Jaydee, Mwana Fa, Juma Nature walikosea wapi enzi zao kutotawala Afrika kama Diamond Platnumz?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,469
2,000
habari wadau..

nazani wote tunaona kishindo alichokuja nacho dogo diamond plutnumz toka wimbo wa mbagala ulivyomtoa... hajarudi nyuma tena ni hit by hit mpaka kushika tanzania nzima na baadae akaanza tawala east africa na then africa nzima wakamjua balaa lake...

nawaza tu wasanii wakubwa waliotawala mziki wetu miaka ya nyuma kina lady jaydee, proff jay, juma nature, inspekta haroon, wao walikosea wapi...

mbona hawakusumbua hata kenya na uganda watukubali mziki wetu...

je diamond ni ana skills kubwa za mziki zaidi yao au ni ana bahati ya mafanikio..

nasikia remix ya namba one ile na davido... diamond alimshawishi davido akubali kwa kumlipa usd 5000... je kina juma nature enzi zao za peak wangekubali kumlipa msanii wa nje hata milioni moja tu ya madafu ili akubali kushirikishwa??
 
Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,464

Mbona unawaulizia hao washikaji Ulizia Alikiba Alikosea wapi mpaka leo hii aanze kupambana na Diamond?????
 
avogadro

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
4,066
2,000
Walipata umaarufu sio kwa kujua taaluma ya uimbaji bali kwa kuimba mipasho ya kiswahili. Unakuta melody iliyomfanya asikike hana uwezo wa kuibadilisha kila siku sauti ile ile anabadilisha tuu mashairi . Waliopo sasa hivi wanafanya tafiti na hata kama kuna baadhi ya miondoko hawaiwezi wanawashirikisha wa nchi nyingine na kuwafunika funika na wenyewe waonekane wanajua, kupitia hilo unakuta wamepata uzoefu mkubwa.
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
6,479
2,000
Hapo kuna kitu kinachoitwa vision ,uthubutu wakuwa risk taker na creativity, wote mnaweza kufanya kitu kimoja, ila kama huna vision na creativity basi utaishia hapa hapa
 
mkojo wa bhange

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
566
1,000
Zamani walikuwa wanafanya mziki mzuri hivyo hawakuhitaji kujitangaza kama anavyofanya domo...ndio maana mpaka leo hujui kuwa kingkiba alishafanya collabo na msanii mkubwa duniani kama robert kelly na huko anakopita domo wao kina ay weshapita na kina sean kingston miaka hiyooooo....na HAWAJITANGAZI WANAACHA MUSIC WAO UWATANGAZE DUNIANI.
 
Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,399
2,000
Huu Mziki zamani hizo ulikuwa unaonekana ni wa kihuni, wakapambana hadi ukaanza kueleweka kwenye Jamii na Wasanii wakaanza kutambulika na kuwa maarufu japo pamoja na umaarufu wao hawakupata kipato walichostahili, Wajanja walikuwa wanawadhulumu kwa kuwaingiza Mikataba ya Kikanjanja then wananufaika wao badala ya Wasanii ukizingatia wengi wao Elimu hawakuwa nayo..,
Kilichowarudisha nyuma zaidi ni kutotambua kuwa Mziki ulikuwa ni ajira kwao, hivyo walipaswa kuwekeza zaidi kwenye huo Mziki, wao wakawa wamebweteka na huu umaarufu wao bila kuwa na Mipango yoyote ya kuwaendeleza!
 
Janma

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
424
500
Zamani walikuwa wanafanya mziki mzuri hivyo hawakuhitaji kujitangaza kama anavyofanya domo...ndio maana mpaka leo hujui kuwa kingkiba alishafanya collabo na msanii mkubwa duniani kama robert kelly na huko anakopita domo wao kina ay weshapita na kina sean kingston miaka hiyooooo....na HAWAJITANGAZI WANAACHA MUSIC WAO UWATANGAZE DUNIANI.
kwani ali kiba alimtafufa R kelly kama mtoa mada anachomaanisha

jina lako mmmh
 
ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
12,112
2,000
jide alishatwaa mpaka tuzo ya kora pale south
nature alishakua nominated tuzo ya kora ila alishindwa kwenda kupafomu sababu alikosa nauli
kama ni kutoboa hawa watu walipambana mno acha kabisa kuwazungumzia mdau
 
kasulamkombe

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
2,234
2,000
SWALI HILO HILO WAULIZE NA KINA BOBAN NA NGASA.UKISEMA NI MITANDAO MINGI WAKATI HUU KWANI HAO WANAMZIKI WAMEKUFA MBONA BADO HAWAIBUKI.HATA KIBA MNAMTETEA TU BURE LIMEZUBAA KAMA MUHA WA KAGERA NKANDA.SASA ANGEKUWA MBALI SANA.SAMATA NA DIAMOND NDIO WANAJUA WANACHOKITAFUTA NA WANA SUBIRA YA KUWEKEZA MUDA.KIPAJI NA HELA ZAO KWA MAENDELEO YA BAADAYE.PIA WANAJUA KUCHAGUA MARAFIKI,PARTNER,MAMENEJA ,PROMOTA WAZURI.KWA UFUPI WANAJIZUNGUSHA NA WATU WAZURI.NA WANAKUBALI KUJIFUNZA KWA WALIOFANIKIWA.MFANO MZURI SIKILIZA KIINGERZA ANACHOZUNGUMZA DIAMOND SASA NA LINGNISHA NA WAKATI ANAANZA.ENGLISH YAKE INGAWA NI FORM FOUR ALIYEFELI NI NZURI KULIKO WENGI CHUO KIKUU NA HASA WAZEE WA EXPANSION JOINT KAWASHINDA WENGI SANA
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,135
2,000
Watu wanataja habari za media na social networks! Wanachosahau ni kwamba media na social networks zinatengeneza mazingira sawa Afrika mzima!

Kuna wasanii kibao wa South Africa na Nigeria walikuwa wanafahamika Afrika mzima... wao walikuwa wanatumia FB, Instagram? Twitter?! Jibu HAPANA na kwahiyo social networks ni nyenzo tu! Afrika kote tulikuwa tunategemea radio, TV na magazeti lakini bado wasanii wa Naija & SA walikuwa juu!

Timu ya Diamond ipo very strategic. Kwanza walifahamu muziki wa Tanzania ulikuwa unaishia Kenya; PERIOD. Tanzania kama nchi nayo haikuwa maarufu kwa chochote miongoni mwa watu wa kawaida Afrika! Kwahiyo no body paid attention kwa kinachotokea TZ!

So, collabo za Diamond vs Nigeria & South Africa ndizo zimemfanya atambulike Afrika na hatimae kuitambulisha Bongo Flavor nje ya TZ & Kenya.

Kwa nchi kama Tanzania ingekuwa ngumu sana kupenya Nigeria au hata SA bila ya collabo na hit makers wa huko kwa sababu muziki wetu ulikuwa haufahamiki!

Nigeria ndiyo Marekani ya Afrika na SA ni kama UK linapokuja suala la tasnia ya burudani! Nyimbo zako zikishaanza kuchezwa Nigeria hesabu zitachezwa kote kusini mwa Sahara.

AY alifanya kosa la kimkakati! Alianza kutaka kufahamika US wakati hata Botswana alikuwa hafahamiki! US hakuingiliki kirahisi unless USHIRIKISHWE na hit makers wa huko(sio KUSHIRIKISHA)!

So, siri ni collabo! Ni collabo za Diamond ndio zimetambulisha Bongo Flavor nje ya East Africa na wengine hivi sasa wananufaika na hustle zake. Ajabu ni pale hata baadhi ya wasanii wenyewe wanapojaribu kumponda Diamond kwa kufanya collabo!

Hawa wanasahau kama sio hizi hustle za Diamond probably hadi kesho ingekuwa wanaishia Kenya tu hapo... sana sana Rwanda!
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,135
2,000
jide alishatwaa mpaka tuzo ya kora pale south
nature alishakua nominated tuzo ya kora ila alishindwa kwenda kupafomu sababu alikosa nauli
kama ni kutoboa hawa watu walipambana mno acha kabisa kuwazungumzia mdau
Tuzo za Kora zilikuwa zinatolewa kwa kanda kwahiyo ilikuwa rahisi sana kushinda kama unakimbiza kwenye kanda yako! So, hao akina Jide walikuwa wanachukua Best in East Africa. Leo wasanii wa Tanzania wanawekwa TOP categories za Africa.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,135
2,000
Zamani walikuwa wanafanya mziki mzuri hivyo hawakuhitaji kujitangaza kama anavyofanya domo...ndio maana mpaka leo hujui kuwa kingkiba alishafanya collabo na msanii mkubwa duniani kama robert kelly na huko anakopita domo wao kina ay weshapita na kina sean kingston miaka hiyooooo....na HAWAJITANGAZI WANAACHA MUSIC WAO UWATANGAZE DUNIANI.
Kiba hajawahi kufanya collabo na R Kelly bali ilikuwa ni One8 Celtel Project waliofanya ngoma na R Kelly.

Huwezi kusema Stevie Wonder amewahi kufanya collabo na Michael Jackson simply because Michael Jackson alikuwa ndie lead artist kwenye We're the World Project na na Stevie Wonder alikuwa ni mmoja wa wana supergroup wa United Support Africa walioimba wimbo We're the World.
 
J wizzy

JF-Expert Member
Sep 2, 2016
344
500
Watu wanataja habari za media na social networks! Wanachosahau ni kwamba media na social networks zinatengeneza mazingira sawa Afrika mzima!

Kuna wasanii kibao wa South Africa na Nigeria walikuwa wanafahamika Afrika mzima... wao walikuwa wanatumia FB, Instagram? Twitter?! Jibu HAPANA na kwahiyo social networks ni nyenzo tu! Afrika kote tulikuwa tunategemea radio, TV na magazeti lakini bado wasanii wa Naija & SA walikuwa juu!

Timu ya Diamond ipo very strategic. Kwanza walifahamu muziki wa Tanzania ulikuwa unaishia Kenya; PERIOD. Tanzania kama nchi nayo haikuwa maarufu kwa chochote miongoni mwa watu wa kawaida Afrika! Kwahiyo no body paid attention kwa kinachotokea TZ!

So, collabo za Diamond vs Nigeria & South Africa ndizo zimemfanya atambulike Afrika na hatimae kuitambulisha Bongo Flavor nje ya TZ & Kenya.

Kwa nchi kama Tanzania ingekuwa ngumu sana kupenya Nigeria au hata SA bila ya collabo na hit makers wa huko kwa sababu muziki wetu ulikuwa haufahamiki!

Nigeria ndiyo Marekani ya Afrika na SA ni kama UK linapokuja suala la tasnia ya burudani! Nyimbo zako zikishaanza kuchezwa Nigeria hesabu zitachezwa kote kusini mwa Sahara.

AY alifanya kosa la kimkakati! Alianza kutaka kufahamika US wakati hata Botswana alikuwa hafahamiki! US hakuingiliki kirahisi unless USHIRIKISHWE na hit makers wa huko(sio KUSHIRIKISHA)!

So, siri ni collabo! Ni collabo za Diamond ndio zimetambulisha Bongo Flavor nje ya East Africa na wengine hivi sasa wananufaika na hustle zake. Ajabu ni pale hata baadhi ya wasanii wenyewe wanapojaribu kumponda Diamond kwa kufanya collabo!

Hawa wanasahau kama sio hizi hustle za Diamond probably hadi kesho ingekuwa wanaishia Kenya tu hapo... sana sana Rwanda!
nadhani mkuu umetoa jibu sahihi.
anaepinga hili ni mpuuzi asiyetambua mchango wa simba kwenye game ya bongo fleva hapa Tz.
ifike mahala simba apewe heshima yake.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,135
2,000
nadhani mkuu umetoa jibu sahihi.
anaepinga hili ni mpuuzi asiyetambua mchango wa simba kwenye game ya bongo fleva hapa Tz.
ifike mahala simba apewe heshima yake.
Siku hizi watu wanateleza wanataka kujidanganya ni uwezo wao! Wanasahau miaka 50 iliyopita pia tulikuwa na wanamuziki wakali lakini na wenyewe walikuwa wanaishia Kenya!

So, upo sahii kabisa! Ni mjinga tu ndie anaweza kupinga mchango mkubwa wa Diamond ktk kuivusha Bongo Flavor nje ya East Africa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom