Nani amekwambia ndani ya ndoa kuna
Mashindano ya Miss Tanzania???Ndoa haina
Lundenga kama Jaji..Ni wewe na Yeye basi...Mtu
anapochagua ''kituko chake'' MUACHE,yeye ndoa
najua kwanini kile Kituko kinamfaa kuwa Mke..Mke
sio Muonekano wa nje,mke ni Akili yake ikoje...Makalio hayaendeshi ndoa,just incase you
didnt know. Na nyie Wanaume mnaoshangaa
Mwanamke anapoamua kuolewa na 'sura ya
mjomba' na kuanza kumnanga 'Shosti nae ndo
nini kuolewa na mtu mfupi kama Kashata za
Magomeni',Muache na Kashata yake,anajua ataitengenezea Kahawa na ndoa itakuwa
tamu...Wanawake wenye akili huwa hawachagui
Misuli na 6packs wala sura nzuri,wanachagua mtu
mwenye Productive heart,anaweza kuwa maskini
sasa lakini ndani yake kuna Utajiri ambao
magube-gube hawauoni ila yeye ameuona na ana uhakika atauvumbua siku moja...Wewe kaa hapo
sagula-sagula sura kama uko mitumbani Karume
halafu uone kama hujaibuka na ndondocha la
kihindi....