Kwanini wazazi?

Lisa

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2009
Posts
1,549
Reaction score
1,075
Habari za Asubuhi wana MMU!
Naomba kuuliza swali kwa wazazi wenzangu ni kwa nini kama mume na mke wametofauiana ndani ya nyumba, basi utakuta baba anakuwa mkali kw watoto, na wakileta mchezo anawachapa bila ya sababu kuwa, AU unakuta mama anakuwa mkali kwa watoto kiasi ambacho amefanya kosa dogo basi hasira za baba zitamwishia yeye, sasa hapo watoto wnaingiaje kwenye ugomvi wenu? Na kama aliyekukosea ni mkeo au mumeo kwa nn usimuadhibu yeye?

Embu wazazi wenzangu nielezeni inakuwaje hapo?

CC Mtambuazi, Asprini, Gfsonwin, mwanajamii one, watu 8, kaka kiiza, Maddame B, The Boss, DR RIWA, na wengine wote humu Jf mnakaribishwa kuchangia.
 
Hasira ni mbaya sana kwani mtu anaweza kufanya kitu asichokitarajia.
 
wazazi wa siku hizi ndo wako hivo, enzi zetu mtu amakula kibano lakini watoto hawaoni changes zozote zile
 
unafanya masihara kama kanyimwa siku mbili mfululizo lazima hasira ziishie kwako
 

Nawakilisha wazazi wote, hapo baba/mama anamalizia hasira zake kama ilivyo kwa rais J.K akigombana na mkewe hasira zote kwa wananchi au waziri au Mkuu wa mkoa hata boss wako hapo akigombana na mkewe/mmewe hasira zote kwa wafanyakazi kisaikolojia ni kwamba anamaliza hasira zake
 
Ile ni kuwa ukiwa na hasira na umechukizana na mwenzio, inafika muda unalaumu siku uliyokutana na huyo mwenzi wako
Dhambi inakuja unapochukia hata watoto ambao mmezaa naye mwenzi wako,
kama usingezaa vile. Ila wale hawana kosa. Halafu unahisi kama wanaweza kuwa upande wa mwenzio ambaye by the time ni mbaya wako
 
Defense mechanism, anatafuta mnyonge wake na yeye....!!!
 
Defense mechanism, anatafuta mnyonge wake na yeye....!!!
hahahahaah! sasa hiyo inakuwa mbaya sana, kwa sababu wale watoto hawajui chochote, kwa kweli huwa tunawakosea watoto wetu.
 
unaweza kukuta ni hasira tu, nami ishawahi kunitokea, mana nilimchapa kibao mtoto mpaka nikamwonea huruma, na sijarudia mpaka leo, yani huwa inakutokea gafla, ila kama mzazi ni mtu wa hasira mara kwa mara anaweza kuwaumiza watoto,
 
Kama mzazi huwa najitahidi sana kutomalizia hasira kwa watoto ni mbaya tunawaathiri kisaikolojia kwa kuwapa adhabu ambazo hawastahili.
 


Inawezekana hasira huwafanya wazazi waliogombana kuona kana kwamba watoto nao kwa kiasi fulani wanachangia ktk ugomvi huo, hasa ugomvi wa mama na baba unapokuwa umeanzia kwenye mahitaji ya watoto. Mfano, mama anakumbushia ada ya mtoto wakati baba hana hata shilingi moja, au mama anakumbushia hela ya chakula kwa ajili yake na watoto au matumizi yoyote kwa ujumla wakati mzee hana kitu, hapo mtoto ukikatiza lazima viboko vichukue hatamu!!! Na mbaya zaidi ombea tarehe za mwisho wa mwezi ziwe bado hazisomeki!!!

Kwa ugomvi nje ya mahitaji, nahisi ni suala la kisaokolojia zaidi, yaani wazazi huwa wakali kwa watoto labda kupunguza stress za ugomvi au pengine ni 'natural behavior' ya ku-release tension baada ya ugomvi kwa baadhi ya watu.

Ila binafsi, huwa siungi mkono tabia za namna hii.
 

Hahahahahaa! umenichekesha sana, kama ni hivyo kwa nn usimpige mkeo aliyeuudhi, au kukunyima sakalamenti takatifu , badala yake hasira zako zinakwenda kwa watoto, mm huwa inanikera sana, inafanya watoto wanakuwa na wasiwasi wanapokuona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…