Kwanini watawala wetu hawaogopi kuiingiza nchi yetu katika machafuko?

Mcben100

JF-Expert Member
Apr 8, 2013
379
559
Habari za asubuhi ndugu zangu watanzania, Mtanisamehe kwa sababu mimi sio mwandishi mzuri na pia uandishi sio fani yangu. Niende moja kwa moja kwenye maada hapo juu.

Ni wazi kabisa kuwa viongozi wetu hawana huruma wala tahadhali yoyote juu ya usalama wa nchi yetu. Especially tangu awamu hii ya tano iingie madarakani. Hii inatokana na aina siasa ambayo imekua ikitumika katika kutawala nchi hii toka hii awamu.

Kumekua na uonevu mkubwa hasa kwa wapinzani na hakuna strategies zozote zinazofanywa kuboresha usitawi wa watu wanaoitwa wanyonge ndani ya nchii. Huku utawala huu ukijinasibu kuwa unapigania haki za wanyonge.

Lakin tumeona uonevu mkubwa ukifanywa hata kwa wasio wanachama wa vyama pinzani ili mradi uwe na maoni tofauti na hawa watawala.

Uonevu huu umeambatana na vitisho au adhabu zisizo halali ( zisizo kwa mujibu wa sheria) juu ya watu na nyama vyenye mtazamo tofauti na hawa viongozi. Matamko yenye kuudhi na kuchochea hasira miongoni mwa wananchi na wanachama wa vyama si tu vya upinzani hata ndani ya chama tawala chenyewe matokeo yake kuibuka kwa watu wanaoupinga utawala huu waliopo ndani ya chama wenyew mfano kina Benard Membe lakin ikumbukwe kuwa watu km hawa wapo wengi ndan ya chama ila wapo tu kimya.

Hivyo basi mambo yanayofanywa na serikali hii yanaweza kuchochea hasira miongoni mwa wananchi, vyama vya upinzani na hata ndani ya chama tawala chenyewe na kusababisha hata kutengenezwa kwa vikundi vya waasi na hivyo kuharibu kabisa amani ya nchi hii.

Tumeona jinsi CCM inavyofanya kwenye huu uchanguzi wa serikali za mitaa, tumeona jinsi viongozi wa upinzani wanavyohangaishwa kila siku kwa kesi za kubambikiwa, tumeona waandish wa habari wanavyonyanyaswa wengne wamepotea na hawajulikani walipo wengne wapo jela na kesi zao zenye kila dalili kua ni za kubambikiwa zikipgwa kalenda kila siku ili waendelee kusota mahabusu ama jela.

Yote haya yanafanya na serikali yetu na yanaweza kupelekea uvunjifu mkubwa wa aman ndani ya taifa letu hili ambalo waasisi wake walilijenge kwa misingi ya amani umoja na upendo mpka wakat huu wa awamu hii ambayo haijali tena umuhimu wa misingi hii.

Hoja ni kwamba kwanin uongozi huu hauogopi kutupeleka katika machafuko. Na nitahadhalishe kuwa pind nchi ikifika huko kuirudisha tena katika amani iliopo sasa itakua ni ndoto.

Najua wapinzani ndio watakao shutumiwa/kusingiziwa kuhusu machafuko iwapo yatatokea. Tumeona waziri wa mambo ndani akianza kujihami kwa kuwasingizia wapinzani kuwa wana njama ya kuvuruga aman ya nchi mara tu walipojitoa kwenye uchaguzi wa serikal za mitaa richa ya kuwa zipo sababu kemkem zilizosababisha wajitoe. Hii ni wazi kua serikal inajihami na wanataka kuwabambikia zigo la lawama za machafuko wapinzani iwapo yatatokea.

Nitoe tu wito kuwa jukumu la kulinda amani ya nchi hii sio la wananchi ama vyama vya upinzani peke yao bali ni letu sote ikiwemo serikali na chama tawala.

Kwa Tanzania inaonekana wananchi na vyama vya upinzani ni wavumilivu sana jambo ambalo mpka sasa ndilo linaendelea kuishikilia amani ya nchi hii. Lakin serikal inaonekana kutokujali kabsa labda kwa sabab wao wanajua kua iwapo machafuko yakitokea wao hayatawahusu ama itakua rahis kwao kukimbilia nje kuokoa nafsi zao kwa vile wanauwezo mkubwa kiuchumi.

Pia niseme tu kuwa iwapo yatatokea machafuko katika nchi hii serikali ya awamu ya tano inahusika kwa asilimia 100, na hakuna wa kulaumiwa zaidi yake. Damu itakayomwagia ya raia wasio na hatia itakua juu yenyu na vizazi nyenu. Tujifunze kwa yaliyotokea kwa wenzetu, DRC, SUDAN, SOMALIA n.k.

Ni malize kwa kuliombea taifa hili amani lipite salama katika kipind hiki kigumu cha utawala wa awamu hii dhalim awamu ya tano. Naliombea kwa mwenyezi Mungu alivushe salama pia kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani. Na kama akipenda aliepushe kabisa kuendelea na awamu hii isiojali usitawi wa wanyonge bali kikundi kidogo cha mafisadi.

Mungi ibariki Tanzania Mungu ibariki afrika.
 
Demokrasia ina mambo mengi ukizidiwa hoja unarudi nyuma kusahihisha unajipanga upya

Wapinzani wamepoteza mvuto,warudi nyuma wajitafakari walipokosea
 
Cha kushangaza tuna raisi, tuna maraisi wastaafu, tuna washauri wa raisi, tuna viongozi wa chama CCM, tuna tume ya uchaguzi tunawasimamizi wa uchaguzi na tuna usalama wa taifa. Sasa sijui wanachokifanya ni nini kama wanahatarisha usalama kiasi hiki. Wao wanavizia tunaokomenti mitandaoni. Tatizo letu ni kuchumia tumbo. Inasikitisha kuona tulipofika
 
Wanajidanganya na nguvu za giza mungu wa CCM mwenge Nyamrunda kuwa ataendelea siku zote kuwafanya watanzania Mazezeta, kumbe tumeshashtuka, Wananchi wakichoka hakuna cha Mwenge Nyamrunda wala nini, sema hili zee halijali amani ya nchi maana kikinuka linarudi kwao Rwanda.
 
Uko sahihi kuwa wewe sio mwandishi na huna hoja. Ndio maana ulichikiandika hapa ni utumbo mtupu
 
Sababu hawajawahi kuona machafuko na hata yakitokea wao na familia zao watakua washasepa nchi za nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…