STARTUP COMPANY,
Kuna mkanganyiko mkubwa Sana wa maana ya Startup ni nini unakuta hata baadhi ya Founder wa STARTUP kibongobongo hawana uwelewa wa kitosha kwamba STARTUP ni nini na inasifa gani, kunaweza kukawa na maana zaidi ya moja ya hili neno hii itategemeana na nani ana define STARTUP.
Kina maana mbili za STARTUP kulingana na nani ana define
1) Normal Enterpreneur: kwao Startup ni Biashara yeyote ile inayoanza au inayoiuwa katika hatua za mwanzo kabisa za operation zake mfano umefungua kibanda Cha Juisi Kama Cha Makjuice, kiduka Cha nguo basi hizo ni STARTUP kwasababu Biashara zinazoanza.
2) Startup Ecosystem: hapa tuna define STARTUP kama Biashara ilinayoanza au iliyo katika hatua za mwanzo kabisa za operation inayolenga kuteka soko lake Jipya na kukua kwa haraka zaidi hii Ni kutokana na kureta solution mpya katika soko lililopo mfano wa STARTUP hi ambazo sasahivi zishatoka kwenye STARTUP ni Uber, Facebook, Amazon, Arbnb
📌Kwanini unzishe STARTUP na sio BUSINESS
STARTUP unaweza kuazisha kwa low cost na ukakua kwa haraka zaidi ukilinganisha na Biashara, hii leo ukitaka Kuanzisha Bank kama Equity utahitaji mtaji mkubwa sana wa Billions of money zaidi ya Billion 50 ambapo wengi hawana uwezo huo na ukifanikiwa Kuanzisha pia utapata faida kulingana na market share ya soko iliyopo lakini njia pekee ya wewe Kuanzisha Bank kirahisi ni Kuanzisha STARTUP maana unaweza anza kwa low cost na ukakua kwa haraka kufika thamani ya Bank kwa Seed Capita ya 10 Million unaweza kuanza Fintech STARTUP yako n within 6 years ukawa na thamani sawa na Bank ambayo ilikuwa ngumu kwa mtaji wake Kuanzisha mifano Kama NALA MONEY, Shocketpay nk
📌Kwanini INVESTORS wanawekeza kwenye STARTUP na sio BIASHARA ya kawaida
Ni kwasababu STARTUP thank yake inakuwa kwa haraka zaidi kutokana na kafanikiwa kuwa na soko lake Jipya kwenye industry husika mfano UBER imechukua soko lake pekee kwenye nyanja ya usafirishaji suala linalofanya UBER kuwa na Super Profit kutokana na ushindani mdogo ukilinganisha na Biashara za kawaida zinazojihusisha na usafirishaji
Hatua za kupitia kuwa kutengeneza STARTUP yako
1)Kutambua tatizo lililopo kwenye jamii
2)Kufikiria Solution yake
3)Kufikiria sehemu ya Biashara ya solution hio (Business Model)
4)Kuanzisha/Kutekeleza Solution hiyo kwa msaada wa Technology
5)Kufanya matangazo kufikia soko lako/walengwa
6)Kufanyia kazi njia za kuaingiza Pesa na solution yako (Monetization)
BOTTOM LINE
📍Nafanya User Interface Design ya Mobile App yenye kizingatia User wanahitaji nini kwenye App au solution yako
📍Natoa ushauri want wazo lako/Solution yako na njia Nzuri zaidi za kufikia soko
View attachment 2399117