Kwanini sijikubeti tena maishani

Sasa mcheza kamari anakuwaje nanidham yapesa ??? Umeshawai kucheza kamari labda.
Kama hujui nidhamu ya pesa itakushinda na utakuwa tegemezi tu ila kama una nidhamu mbona simple tu.... Mwaka wa 7 huu kwenye fani
 
Mwaka 2012??
Naomba unijibu maswali haya niamini kama story hii ni ya ukweli!!
Je ulifanya kazi zako hizo na mtaji wa betting muda gani? Je uliporudia ulirudia form ngapi? Na ukamaliza mwaka gani? Baada ya kufaulu ulisoma elimu ipi ya juu(diploma au degree)? Naomba uwaambie hawa GT kwa kipindi hiki cha miaka mitano umewezaje kuacha shule mpaka leo umemaliza chuo na kupata ajira?
 
Kitu msicho kitambua vijana wengi ni kwamba, Kubeti pia ni urahabu
Ni urahibu ...umenikumbusha msamiati wa kamishina sianga wa ngada (madawa ya kulevya) juu Ya jamaa waliyeenda kumkamata wakamkuta ana waambia yuko na Bill gate,
Urahibu ...ulevi wa kupindukia wa madawa ya kulevya
 
Ni urahibu ...umenikumbusha msamiati wa kamishina sianga wa ngada (madawa ya kulevya) juu Ya jamaa waliyeenda kumkamata wakamkuta ana waambia yuko na Bill gate,
Urahibu ...ulevi wa kupindukia wa madawa ya kulevya
Urahabu ndio lugha fasaha, tena mujarab pasi na shaka
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Pole. Jana nimepiga mpunga wa maana na sasa najisomea hapa matokeo mbalimbali za mechi tano za mwisho kwa timu ninazotia pesa leo. Tatizo ni matumizi yako na sio betting.
 
Pele bt haka ni kadrama umekatunga... Tunashukuru kanatia ufahamu kwa vijana wanao beti
 
Hapa ndugu ulichokifanya ni kuhamasisha watu kubet, amini amini nakuambia.
Hata kama ulikuwa na nia nzuri ya kuhamasha tusibet lakini wengi watahamasika.
 
Hahahaa, kuna hapo aliposema eti alikuwa na milioni 9 tu akafungua cd Library, saloon ya kiume, mgahawa, playstation....Dah hajawahi shika hata milioni 2 huyu jamaa
 
Watu wengi hasa huku TZ ambako kubet ndio kumenza hivi karibuni wanadhani ni biashara na unaweza ukatengeneza mahela kila siku.
Kubet ni bahati, na hao wanaoendesha huo mchezo wa kubet wanafahamu kabisa kwamba wanaoshinda ni kwenye asilimia ndogo sana. Kwahiyo kwa ni biashara lakini wewe unaye bet ni bahati.
Jiulize mwenyewe kama ungeendesha hiyo biashara ya kubet na watu wakawa wanajishindia tu je utapata faida gani? Na je utawalipa vipi hao wanaoshinda shinda?
Kubet ni bahati kwa sababu siku ambayo utaweka hela zako kwenye timu anayoiamini kwa asilimia zaidi ya mia itashinda lakini siku hiyo mambo yakagauka. Hapo kuna alternative 3, kushinda, draw au kufungwa. Na tumeshaona mara nyingi sana timu kubwa zenye uhakina wa kushinda zikifungwa au kutoka draw.
Kwa hiyo huo mchezo mmoja tu kuna nafasi tatu. Kushinda, draw au kufungwa, Sasa ukiweka mkeka ukaongeza mechi nyingine zikawa mkeka wa mechi 2 inamaana bahati au asilimia ya kushinda inazidi kuanguka, maana unakua na chance 6 za kuchagua mmoja wapo. Inamaana huo mchezo uchague chance 2 kati ta Sita. Mmoja wao akifungwa basi usha poteza kote. Na unapozidi kuongeza huo mkeka ndio inazidi kua ngumu kushinda.
Kwahiyo ndugu zangu mnapo bet mjiangalie sana na mtafakari sana. Cheza kwa hela ambayo ni ya ziada na hata ulipoteza haitakuuma.
 
Mwanafunzi anasoma akiwa na chaguzi mbili afauli au afeli, hiyo ni kamari..

Mhitimu anatambua fika kuwa uwezekano wa kupata ajira au asipate ajira kwa kile alichokisomea ..

Mkulima anayetegemea mvua na yeye pia hua ana-bet, mvua ikiwa ya uhakika kwake ni faraja na ikiwa tofauti inakuwa kaliwa..

Siasa nayo ni ku-bet, unawekeza nguvu na rasilimali nyingi huku ukijuwa fika kuna kushinda na kushindwa..

Kufanya biashara nako ni-bet, kwani itategemea na mapokeo ya wahitaji wa bidhaa au huduma husika!

Hivyo basi maisha ya mwanadamu yanajiendesha kwa mambo ya kubahatisha, japo yametafsiriwa kwa namna tofauti tofauti..

UNAPOJIANDAA KUSHINDA, USISAHAU PIA KUNA NA KUSHINDWA PIA.
 
Ndugu yangu msomi uliyeanzisha mada, mbona uandishi wako una makosa mengi sana!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…