Kwanini mkoa wa Mbeya?

Huliza

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2017
Posts
448
Reaction score
1,114
Naulizia hii ya waimba nyimbo za injili, Wachungaji wa makanisa ya kilokole kwanini wengi wanatoka mkoa wa Mbeya?

Hawa wachungaji wa Mbeya wametapakaa nchi nzima wakihubiri injili na wokovu, Huwa najiuliza maeneo ya Dar es Salaam mengi mpaka mitaani wachungaji wa haya makanisa wengi wao wanatoka mkoa wa Mbeya

Je nini kipo nyuma ya huu mkoa wa Mbeya?

Je huko Mbeya kuna shule nyingi za biblia kuliko maeneo mengine?

Je Mbeya hii imani ya Kuhubiri na kueneza ulokole ina Misingi kutoka nchi gani?

Mfano hawa ni baadhi ya wachungaji wenye asili ya Mbeya na wenye majina makubwa na kuna wachungaji wengi wapo mkoani na hata maeneo mengi ya miji mikubwa

1.Mtume Mwamposa,Na kuna shehe (Ustadh Mazinde) aliwahi uliza hivi kweli Mtume anaweza kuwa mnyakyusa na akotokea Mbeya?

Shehe Mazinde aliumia baada ya kuona waislamu wanatoka Zanzibar na Tanga kwenda kuombewa na Mwamposa

2.Mwalimu Mwakasege.Huyu kwa wale wasiofungamana na upande wowote wengi wanamfahamu sana na anafuatiliwa na malaki ya watanzania kwa mafundisho yake

Inasemekana baada ya Lagos Nigeria kwa Afrika mkoa wa Mbeya ni wa pili Afrika kwa kuwa na makanisa mengi

Inasemekana kila baada ya hatua kadhaa mkoa wa Mbeya utakutana na makelele watu wakiimba na kusifu huku wachungaji wakitoa injili na maombi ya nguvu

Turudi kwenye waimba kwaya na Gospel kwa ujumla, Nadhani hapa ndio mwisho wa kazi yenyewe, Watu wa mkoa huu ukiwakuta wanaimba kwaya, wanaimba kwa hisia sana na unaweza Fikiria Leo ndio mwisho wa hii dunia

Maajabu wanaimba na kulia sana lakini mkoa wa Mbeya hauishi matukio ya vituko na maajabu kila wakati

Mwaka huu kuna mlima hapo Mbeya umesababisha ajali mfululizo haijawahi kutokea na ukamfanya Makamu wa Rais Philip Mpango kwenda kutazama eneo husika linalosababisha ajali, Cha kushangaza baada ya siku kadhaa wachungaji wakaenda kupiga maombi hapo Mlimani
 
Mkuu, si kwa ubaya, ila unaonekana unafuatilia sana mambo yasiyokuhusu, labda nikushauri, kama unaona wanafaidi sana kuhubiri na kuimba, FANYA NA WEWE! Nchi ni huru hii mkuu.
 
Mwamini Yesu awe Bwana na Mwokozi wako. Acha kulialia hapa.
 
Kati ya hayo maswali mimi ntakujibu moja tu, kuhusiana na wingi wa mashahidi wa Yehova kwa Tanzania, Mbeya ni wengi zaidi kwasababu ya ukaribu wake na Zambia, kumbuka kwa AfriKa, Zambia ndio nchi yenye mashahidi wengi wa Yehova, ni zaidi ya laki 4 na wao jukumu lao kubwa ni kuhubiri pengine imepelekea wao kuwa wengi mbeya, japo Tanzania nzima licha wa wingi wetu, mashahidi wa Yehova bado hawafiki elfu20. Kuhusu wakristo wengine sifahamu mkuu, huo ndio mchango wangu
 
Msalimie About Misholi...
Sijui ana unasaba na Ayubu?.. Kazi zake zinanibariki sana
 
Wapo wengi sana ila ukiangalia kiundani ni kama kila kabila kuna sehemu wamedominate.
 
Bila kusahau mabaa na guest kama zote huko
 
Arusha,mwanza moshi morogoro pia kuna movement za injili kama mbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…