Katika hili naungana na JK na Sitta kuliangalia kwa macho mawaili.
Nyerere alipotaka muungano wa EAC Kenya ilikataa na KIbaki alipiga kura akiwa mbunge kukataa hilo. Nyerere alipoanzisha juhudi za EAC Kenya wakaiua kwa vile Tanzania na Uganda ni tegemezi.
Baada ya vituko vyote hivyo Kenya wanataka muungano leo hii jioni, hivi hujiulizi ina maana Kibaki amekuwa na akili baada ya miaka 50!
Kinachoongelewa ni ardhi tu na sio miundo mbinu, elimu au afya, jiulize ni kwanini. Angalia population ya Rwanda, Kenya na Uganda halafu fikiria miaka 20 ijayo itakuwaje.
Kwanini wasiilaumu Tanzania kwa miundo mbinu au elimu ila suala la ardhi tu!!!
Tanzania imesema kama wanaona wanaweza kwenda peke yao basi na waende. Kenya na Rwanda wameanza na wala Tanzania haijalalmika. Kwanini wasubiri kama wanaweza kuungana wao. Wanasubiri nini?
Uganda na Kenya waligombea kisiwa cha KM 1, halafu unataka Tanzania iachie kila kitu. Kama wao wanataka ardhi iwe ya jumuiya kwanini walifikia mahali pa kutangaza vita kwa KM 1 tu. Fikiria kwanza na tanguliza busara Rutashu..
Mwisho, EU ina matatizo makubwa sana leo na wanafikiria kila nchi kurudi katika sarafu yake n.k. Wameanza miaka 50 iliyopita na bado wana matatizo sasa sisi wa miaka 10 tukurupuke tu.
Hili la muungano lina interest zao vinginevyo wangekomalia uchumi, soko la pamoja, elimu na afya. Wao wamekomalia suala moja tu ardhi. Kwa hili lazima Watanzania tuwe macho kwasababu tumeshaonja shubiri ya mwaka 1977. Mimi niliyaona kwa macho yangu. Kama si Mchina na mataifa rafiki nchi ilikwama kabisa.