Siku zote nimekuwa najiuliza swali ambalo ni gumu sana kupata jibu kuhusu jamii yetu, Hivi ni kwa nini viongozi wetu hasa wa upinzani wamejikita sana kwenye kuongelea mambo ya Gesi na Madini? kama kweli wao ni wazalendo na wana uchungu na nchi na wananchi wake kiasi hicho, mbona sijawahi kusikia hata siku moja wakipinga mtindo wa Serikali kwenda kutibu Viongozi wa nchi nje ya nchi, mbona sijasikia mtu akiomba muongozo wa spika juu ya hilo?
Kuna wale ambao wanaweza wakapuuzia hili na kudharau, lakini kwangu mimi hakuna dhambi na Usaliti mkubwa kama huo, ni ubinafsi ambao hauelezeki kwa wananchi ambao kila siku mnapiga kelele kwamba mnawatetea, sasa mnawatetea inapokuja kwenye Gesi na madini tu? Wapinzani wanawezaje kukaa kimya kwa jambo kama hili? Kwanini hawalipi umuhimu wowote kama Madini au Gesi? Je, kuna kitu kinawagusa wananchi zaidi ya afya yao? Au kwa sababu labda afya ya mwananchi wa Tanzania hawezi kuwaalika kwenye makongamano kama Gesi na Madini? au kwa sababu afya ya Watz haiwezi kuwakutanisha na wazungu kama Gesi na Madini?
Mwisho kwangu mimi sioni tofauti yoyote ya wapinzani na CCM, labda watu wanawashabikia tu kwa maana ni kipya lakini siamini kama wako kwa ajili ya wananchi kwa maana hawajanishwawishi bado, kama wananona ni jambo la kawaida na lakukubalika kwa Serikali kupitisha bajeti ya kupeleka Viongozi nje ya nchi kwa matibabu, watawezaje kuwatetea wananchi itakapokuja kwenye mambo kama Elimu !