Inashangaza watu ambao kwa nguvu zote walimkataa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais aliyepewa ridhaa ya kuongoza nchi na watnzania wengi sana.
CHADEMA walikataa hata kujadiri hotuba yake, bila aibu wakatoka nje ya bunge kwa madai kwamba hawawezi kujadili hotuba ya Rais najisi hivyo na hotuba ni najisi.
Sasa leo wanamtaka Rais ashiriki nini ktk kuondoa dosari kwenye mchakato wa katiba?
Je unajisi wake umekwisha, nani alimtakasa?.
Tatizo lenu magamba, kila kitu mnakifanya propaganda.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ameelezea kwa ufasaha sana, kuhusu maamuzi ya kamati kuu yao, ya kuwa condition moja, inayopaswa kutawala katika mazungumzo, ya kusaka muafaka wa kurudi kwao, kwenye bunge la katiba, ni kuheshimiwa kwa maoni ya wananchi, kama yalivyokusanywa na Tume ya Warioba, na wao Ukawa, hawatakuwa tayar kurejea kwenye bunge la katiba, kama hawatahakikishiwa kuwa Rasimu itakayojadiliwa kwenye bunge hilo ni ile Rasimu, iliyoandaliwa na Tume ya Warioba, yenye maoni ya wananchi, na siyo Rasimu mbadala, iliyoandaliwa pale Lumumba, yenye maoni ya watu wachache sana, ambao wao maslahi binafsi na ya chama chao, ndiyo wanayoyapa kipaumbele, kuliko maslahi mapana ya Taifa hili la Tanzania.
Inawezekana magamba, wakaamua kwa makusudi kabisa kupotosha msimamo huo wa Ukawa, wakisaidiwa na vyombo vyao vya habari vya propaganda, lakini msimamo huo wa Ukawa, hauwezi kubadilika kwa kutumia propaganda machinery za wanaccm!