Nimekuwa nikitazama programu za chaneli za Tv mbalimbali hapa Tanzania na nimegundua kitu ambacho napenda kuwajulisha.
Hivi taarifa ya habari kuonekana katika chaneli za ETV na Clouds TV ni lazima au ni ubunifu tu?. Kama ni ubunifu basi wanakosea na wabadilike haraka iwezekanavyo. Kuna mambo mengi kuhusu sanaa yanahitaji coverage na mda huo wangetumia kutengeneza na kurusha vipindi vingine vya sanaa.
Kuna chaneli nyingi hapa Tanzania zilizojikita katika habari za mchana, usiku na mubashara wakati wowote kama ITV, Chanel 10, Star Tv kwa uchache, hivyo basi sioni sababu za msingi kwa chaneli kama Clouds Tv na ETV kuwa na mtindo wa aina moja.
Na kama TCRA inahusika na kipengele cha "ulazima" basi ni kipengele kibovu na kifanyiwe marekebisho haraka sana.
Sanaa nchini Tanzania bado haijapata coverage ya kutosha na masuala mengi kuhusu sanaa kwa upana bado yana changamoto zinazohitaji ushawishi wa watengenezaji wa vipindi, waandishi na tasnia nzima kwa ujumla kufika sehemu sahihi.