Kwako Tundu Lissu

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
894
Reaction score
994
30 Juni, 2019
Nakuandikia nikiwa nimeguswa sana na hatua zilizochukuliwa dhidi yako za kukuondolea ubunge.

Imeniuma kama ilivyowauma Watanzania wengine ambao wanakumbuka kupigwa kwako risasi nyingi mwilini tarehe 07 Septemba, 2017. Maumivu na uchungu wa unyama ule sio jambo ambalo linatarajiwa binadamu kumfanyia binadamu mwenzake.

Wapo wanaoshambuliwa na kufa papo hapo na wengine kufa baadaye, lakini kwa Tundu Lissu, Mwenyezi Mungu amenyoosha mkono wake upo hai mpaka leo ukiwa umepitia matibabu makubwa ya upasuaji mara kadhaa ili kutengeneza viungo vyako vya mwili.

Napomshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai wako, pia nawashukuru Madaktari wote kuanzia wa Tanzania, Kenya na Ubelgiji ambao wamefanya juhudi kubwa kunusuru maisha yako na kwa upendo wa Mungu upo hai mpaka leo na tunakusikia tena ukinena.

Kwa sisi wacha Mungu uhai wako mpaka leo ni zawadi kutoka kwa Mungu na ni upendeleo mkubwa kwako na kwa sisi tunaokupenda. Kwa sababu wapo waliopigwa risasi na sasa wapo ardhini wamezikwa.

Juzi Spika wa Bunge Job Ndugai ametangaza kufutwa kwa Ubunge wako, hii ilikuwa inahitimisha majibizano ya mara kwa mara yaliyoanza tangu ulipopata nafuu na kukuwezesha kuzungumza. Ilikuwa ni hatua ya uchungu mwingine mkubwa kwetu tulioona dhahiri inakuumiza zaidi. Kwamba kwa kutokuwa Mbunge sasa hata stahiki za ubunge hutopata tena.

Jambo hili ni chungu sana.

Ninalo neno la kukwambia na ninaomba ikikupendeza na wote wanaonisikiliza ikiwapendeza tulisome.

Haina mashaka kwamba jambo ulilofanyiwa halikupaswa kabisa kufanyiwa siasa, ni uhalifu dhidi ya uhai wa binadamu, lakini kwa bahati mbaya sana, narudia kwa bahati mbaya sana wewe mwenyewe na jamaa zako wa chama chako cha siasa mkaanza kutumia mashambulizi dhidi yako kama ajenda ya kujijenga kisiasa dhidi ya wapinzani wenu wakubwa ambao ni chama cha mapinduzi CCM ambacho ni chama tawala.

Nasema tena ni bahati mbaya sana kosa hili ulikubali kulianzisha wewe mwenyewe na wenzako wa CHADEMA. Kwa hesabu za kawaida kuanzia pale binafsi nilijua kwa sababu mmelipeleka huko basi CCM wasingeweza kukaa kimya ili muwamalize hasa wakati huu tunapoelekea chaguzi.

Kauli zako ulizokuwa unazitoa ukiwa kitandani zilivumiliwa kidogo na mara kadhaa CCM wenyewe walisikika wakisema hawawezi kujibizana na mgonjwa. Hata jamaa zako wa CHADEMA walipojaribu kuchokonoa walivumiliwa kwa mazingira hayo hayo.

Kana kwamba hiyo haitoshi ukaamua kufanya ziara ya nchi za Ulaya na Amerika ukifanya jambo hilo hilo la kuwasulubu CCM na Serikali kimataifa kwa mahojiano yaliyojaa mbwembwe nyingi na kashfa nzito dhidi ya Rais, Spika na CCM kwa ndio waliokushambulia kwa sababu walitaka kukudhibiti usiwaseme. Uliapa kuwa utawamaliza kwa kueleza walichokufanyia.

Kwa wenye akili tukaona hapa sasa ajenda imehama kutoka mgonjwa kwenda mpambanaji.

Wewe mwenyewe na wenzako wa CHADEMA mkaendelea kushinikiza taasisi mbalimbali za kimataifa ziinyime ushirikiano Tanzania ikiwemo fedha za miradi ya maendeleo na mkafanikiwa kwa kiasi fulani. Kwa wenye akili tukajua hapa mtawapoteza wafuasi wengi wanaoelewa madhara ya kampeni hii.

Wewe mwenyewe na wenzako CHADEMA mkatamka mara kadhaa kuwa hamjali kuhusu gharama za matibabu yako, kwamba mtalipa na mkaitisha harambee Watanzania na wengine wachange fedha za matibabu yako. Wenye akili tukajua hapa mnakwenda kupoteza nguvu muhimu ambayo ni fedha kwa matibabu na ustawi wa siasa zenu.

Na mengine mengi mengi.

Yote haya mlikuwa mnafanya juhudi ya kuishughulikia Serikali, Spika, Rais na vyombo vya dola vya Tanzania ambavyo mmevichafua sana kimataifa.

Umefanya yote hayo ukiwa unafahamu kuwa pako mahali ambapo unaowashughulikia wanaweza kulipa kisasi. Ukiwa unajua kuwa unabanwa na sheria za mwajiri wako ambaye ni Bunge, ukiwa unajua kuwa unamchafua anayetoa fedha za matibabu yako, ukiwa unajua unaowachafua wanao uwezo wa kukuondoa katika kiti chako cha ubunge na wakatangaza jimbo lipo wazi na litagombewa na wengine ili wananchi wa Singida Mashariki wasikose mwakilishi.

Katika mazingira hayo, ulitarajia nini?

Kwa mawazo yangu kilichosababisha uondolewe Ubunge ni wewe mwenyewe na wenzako ndani ya CHADEMA. Mnadanganyana sana na mmekosa kabisa ubunifu wa kufanya siasa katika mazingira ya sasa. CCM inawashinda na mnamalizika kwa kukosa maarifa.

Leo umefukuzwa Ubunge, muda mfupi ujao atapatikana Mbunge mwingine wa Singida Mashariki na kwa muda wa mwaka mmoja na miezi kadhaa atajijenga kisiasa na kiuchumi, maana yake ni moja tu mwakani kwenye uchaguzi mkuu kama utaamua kuomba tena Ubunge tayari utakuwa una mpinzani anayetetea kiti chake. Haitakuwa kazi rahisi. Hapa umepigwa vibaya sana na sidhani akina Mbowe kama wanakushauri vizuri na nina mashaka kama hawatakutelekeza. Siamini kama wataendelea kukugawia fedha bila kazi ya kufanya na siamini Watakubali kukupisha kwenye nafasi zao ama matarajio yao ya kisiasa.

Najua wapo watakaobeza mawazo haya lakini huo ndio ukweli. Hapa hesabu za kisiasa hazijakaa sawa na sasa ndugu yangu Tundu Lissu umeshaondolewa kwenye ajenda, itakulazimu uanze kupambania kuondolewa kwako na kutafuta huruma ya wananchi wakati jamaa wanasonga mbele.

Na ni kujidanganya sana kwamba katika dunia ya leo utajenga siasa yako kwa kutegemea watu wale wale ambao walitutawala na leo bado wametukalia kiuchumi. Kwamba unalofanyiwa utasema Ulaya na Amerika, ni kupoteza muda, mwisho wa siku Tanzania ni nchi huru inayojiamulia mambo yake yenyewe. Unaweza ukadhani uanasheria wako utakusaidia lakini kumbuka mahakama utakazozitegemea ni za Tanzania, Majaji wanateuliwa na Rais na vyombo vya ulinzi na usalama vipo chini yake.

Labda kama unaamini kwamba Tanzania inaweza kuingia kwenye vita na Taifa fulani kwa ajili yako. Au unaamini kuwa wewe ni mtu bora kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania kwamba suala lako ni la kufa na kupona. Mimi siamini hayo yote.

Ninachokiona ni kutaka kukutumia kama mtaji wa kisiasa. Kwamba uendelee kuisema CCM, Serikali, Spika na vyombo vya dola ili ionekane CHADEMA inaonewa. Very poor strategy.

Katika mazingira haya ambayo Serikali ya Rais Magufuli inafanya miradi mikubwa ya maendeleo iliyoshindikana tangu nchi ipate uhuru, inatetea wanyonge na kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii ambayo ndio mahitaji makubwa ya wananchi, siasa hizo zina nafasi finyu sana. Ni kuumizana na mwisho wa siku unaanguka.

Kosa kama hili wamefanya wanasiasa wengi na hawakufanikiwa. Akina Kiiza Besigye, Morgan Tshivhangilai na wengine wengi. Fight against the ruling regime must be smart and productive. Any miscalculation is a serious loss.

Niishie hapo nawatakia Jumapili njema.

H.M Kituta
Mtanzania Mpendahaki.
 
Kuna vitu vinauma sana lakini .Hivi ni kweli Ndugai ajui alipo Tundu Lisu?. Kweli mtu aliyepigwa risasi nyingi vile apone kwa mwaka mmoja? Kweli panahitaji elimu ya chuo kikuu kujua kuwa anatakiwa kujijenga kisiasa asije kufutika kabisa kwenye ulimwengu wa siasa? Kwani binge limemtuma nani kufuata taarifa za mgonjwa na kumshauri namna ya kufanya ili aweze kuendelea kuwa mbunge?
 
Only herb (kaya)will heal our nation out of that will nothing.........

Youth have been dumped and ignored at large scale ....


Nothing will be changed if Youth will continue being corrupt. by politicians.....
 
Mgonjwa gani anasafiri hadi london kwenda kufanya interview BBC, lakini anashindwa kwenda dodoma kutoa taarifa?
 
Ukijibiwa nishtue nipo twitter huku
 
Umeanza kwa kujifaragua sana, mara ooooh mara uuuuh lakini ukweli wa roho yako mbaya umejidhihirisha mwishoni mwa thread yako.


Kwa kuwa hujamuelewa aliye mfalme wa tawala zote za dunia hii basi ni vyema ukatulia tu ila baadae utakuja kumuelewa huyo MFALME anavyofanya kazi yake katika dunia hii.
 
Tumchangieni jamani kila mwezi apate walau kakitu
 
Hivi angerudi nchini kungekuwa na uwezekano wa kumruhusu akaendelee na matibabu au clinick huko Italy au angeambiwa Muhimbili wanaweza kuendelea na kazi hiyo?

Passport ikiwa ceased angeendaje huko?
Amelekwepa hili,leo wamembana kwenye kete ya kingi.

Walizicheza kete vizuri hao wakuu.Just to say hongera zao.

Ila kwa imani yangu ni kuwa TZ hakuna upinzani wa kweli Bali wote ni wale wasiojulikana.Wameianza hii Nazi yangu enzi A Babu wa Taifa.

Simuamini the Freeman wala yeyote.

Lisu nae atakuwa amekiuka viapo kiasi cha haya kumjiri.

Kumbika kauli ya Babu wa Tz kuwa uoinzani utatoka wapi.

Tunawaminisha wanaulimwengu kuwa we are multiparty followers Bali tunajua tulivyozichanga karata zero.

Nakaribisha mjadala pale kitivo cha Political Science Mlimani Varsity.
Sasa kama hata kwenda dodoma, si ndio maana akavuliwa ubunge? Why mnalialia
 
Mgonjwa gani anasafiri hadi london kwenda kufanya interview BBC, lakini anashindwa kwenda dodoma kutoa taarifa?
Wewe mutu mwenye akili finyu sana unafikiri umbali wa kutoka alipo mgonjwa kuja DSM kisha Dodoma ni sawa kutoka alipo mgonjwa mpaka London? Kumbuka tu kuwa yule in mgonjwa hawezi safiri umbali mrefu kama Wewe mzima bila kuleta athari za afya.Umekuwa unamuona kupitia clip za video anafanya mazoezi ya kutembea kwa ufupi bado hayupo sawa.Hata kama huamini mungu hata Babu yako naye humuamini ? Yaani Hali ile aliyokuwa nayo wazungu wamepambana kwa viwango vya juu vile lakini hajakaa sawa akija huku Afrika bila shaka tunazika fasta.Sheria isiyokuwa na haki siyo Sheria kabisa na haifai kwa matumizi ya binadamu.
 
Kutoka brussels belgium mpaka dodoma ni km 7500, kutoka brussels belgium to washngton ni km 8506, cha kushangaza ameweza kusafiri kutoka belgium kwenda washngton ila kashindwa kwenda dodoma eti ni mbali! Pumbavu kabisa
 
Hivi nyie munafikiri lissu analo fanya yeye fala anajua nini anacho kifanya na haja hanzia hapa tangu 2001, ni swala la muda tu ni mtu anayeona mbali kwa maana alijua hili lazima litokee
 
Kutoka brussels belgium mpaka dodoma ni km 7500, kutoka brussels belgium to washngton ni km 8506, cha kushangaza ameweza kusafiri kutoka belgium kwenda washngton ila kashindwa kwenda dodoma eti ni mbali! Pumbavu kabisa
Wewe pumbavu tena usiyejua usafiri wa Dunia .Kumbuka hakuna Dege ya moja kwa moja toka Alipo mgonjwa Belgium kwenda Dodoma ila zipo Dege za moja kwa moja Toka Belgium kwenda Washington .Tena ukumbuke tena Usalama wake ni wa juu sana Washington kuliko Dodoma tena ukizingatia kipindi hiki cha ugonjwa.Wewe mbwa usiyekuwa na roho ya kufikiri haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…