Kwako rafiki

Tan1947

Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
40
Reaction score
42
BARUA YA WAZI KWAKO RAFIKI YANGU KUHUSU NDOTO ZAKO

Wasalaam!!

Natumaini u bukheri wa afya na Mwenyezi MUNGU amekujaalia pumzi na uhai Kwa muda huu uusomapo waraka huu.Nami pia ni bukheri wa afya Kwa kudra za Mwenyezi MUNGU naivuta hewa yake pasipo kulipia.

Rafiki yangu mpendwa,Kwanza napenda kukupongeza Kwa Kuwa na NDOTO kubwa kuhusu maisha yako. Kongole!! Rafiki,mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke akalelewa vyema lazima awe na malengo na NDOTO anuwai na adhimu kuhusu maisha yake.Hivyo basi napenda kukupongeza Sana Kwa Kuwa na NDOTO,pengine NDOTO zako ni Kuwa mfanyabiashara mkubwa,mchezaji wa kimataifa,mwanamitindo,ama msomi ama mwanataaluma fulani,narudia tena kukupongeza,kongole rafiki.

Rafiki yangu mpendwa,naandika waraka huu ili kukukumbusha kuhusu mambo kadhaa ili NDOTO yako iweze kutimia.

Ni ukweli usio na chembechembe za uongo Kuwa, Mafanikio hayatokei Kwa bahati mbaya.Abadani,huwezi kufanikiwa Kwa bahati mbaya isipokuwa Kwa mipango.Naam lazima uweke mipango ili NDOTO zako zitimie.Rafiki yangu mpendwa sio kila mpango ni Mpango.Lazima uwe na mipango chanya tena mipango yenye uhalisia mathalani ni kweli una NDOTO za Kuwa mfanyabiashara mkubwa lakini lazima mipango iwe na uhalisia Kuwa huwezi Kuwa mfanyabiashara mkubwa pasipo kuanzia chini,hivyo basi lazima uwe na mipango ya muda mfupi na mipango ya muda mrefu Kwa ajili ya kutimiza NDOTO zako.Rafiki yangu mpendwa,kabla hujawaza kumiliki supermarket ama maduka makubwa lazima Kwanza uwaze Kuwa na biashara ndogo ambayo utaitumia kama ngazi ya kufika huko unapotaka kufika.Ni kweli unatamani Kuwa mfanyabiashara mkubwa lakini usisubiri mpaka uwe na mtaji wa Milion kadhaa ndipo ufungue biashara yako,unatakiwa uanze na kile kidogo ulichonacho.

Rafiki yangu mpendwa lazima pia uelewe Kuwa, NDOTO huwa zinafuatwa,naam lazima uzifuate NDOTO zako,kama unahitaji Kuwa mwanasheria lazima ufuatilie ama Kuwa Karibu na watu ama vitu vitakavyokufanya utimize NDOTO yako vivyo hivyo Kwa biashara ama mengineyo. Mafanikio hutafutwa,je unayatafuta mafanikio yako au umekaa kuyasubiri mafanikio yakufuate Wewe?Rafiki yangu mpendwa nje ya kudra za Mwenyezi MUNGU, mwanadamu pia analo jukumu kubwa la kutumia jitihada zake ili aweze kutimiza NDOTO zake,Usiache kumuomba Mwenyezi MUNGU lakini pia kumbuka kufanya kazi Kwa juhudi na nidhamu kubwa.

Nisikilize,rafiki yangu mpendwa ni kweli unao watu waliofanikiwa katika nyanja za NDOTO zako wanaokuvutia ambao Kwa lugha ya malkia huitwa ROLE MODELS, Ni Jambo Jema na zuri Sana Lakini naomba nikukumbushe Kuwa vitu au sifa unazowaona nazo Leo wametumia muda mrefu sana,nguvu,jasho na nidhamu kubwa kufika pale walipo,Ni kweli unatamani Kuwa mchezaji mkubwa wa kabumbu kama Christian Ronaldo,lakini je unatambua kuwa Christian Ronaldo hutumia muda mwingi wa ziada kufanya mazoezi makali na Kula diet ili aweze Kuwa vile alivyo Leo hii?Najua unatamani Kuwa Tajiri mkubwa hapa barani Africa,Lakini naomba nikukumbushe tu Kuwa,Aliko Dangote alifanya biashara kwa miaka 30 kufika pale alipo Leo hii.Nimeamua kukupa mifano hii michache ili kukumbusha Kuwa Role models wako walipambana Sana mpaka kufika hapo walipo.Rafiki yangu mpendwa usiishie tu kuyatamani mafanikio yao,jifunze pia safari za nyuma ya mafanikio yao.

Rafiki yangu mpendwa,ninayo mengi ya kukuandikia lakini kalamu yangu imeishiwa wino na imeanza kugoma goma, kwa Leo naomba nifikie tamati Kwa nukta hii.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una ujumbe mzuri, ila umepungukiwa na uwezo wa kuufikisha kwa walengwa kwa njia hii ya uandishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…