Binafsi hiyo "KWAAJILI YAKO" hua inanipa utata sana. Naona kama ni namna ya kuanzisha mahusiano ambayo ni complicated tangu mwanzo, maana hata siku akikuchoka anaweza asichelewe kukutupia dongo la " we ndo ulinifanya nikamwacha mpenzi wangu. . .and for what? Huna maana!" . Hapo mshachokana au complication zishakua nyingi. Nimefikiria njia ambayo ni bora kudeal na mtu ambae yupo kwenye mahusiano anayodai hayataki tena bali anataka kuwa nawe , huku nawe ukipenda kuwa nae ni kumtaka ajitoe kwenye situation aliyomo (current mahusiano) bila ya kukuhusisha wewe. Kwamba bila ya kujua kama utampokea au la, avunje hayo mahusiano anayodai hayataki tena alafu ndio arudi kutaka kujua kama unamtaka na kama uko tayari kumpokea au la....?
Sometimes matters of the heart can not be thought by the head.., (ukipenda you can do stupid things and there is no boundary) nadhani effect ya kuwa na mtu mwenye mahusiano ni kuogopa kuumiza third parties, na sio kuogopa lawama in the future kwamba ulinifanya nimwache mpenzi wangu (sababu hakuna aliyelazimishwa), anyway cha kufanya ni kuhakikisha wote wanaachana kwanza mahusiano yao na sio kwamba mna-cheat.
Na issue ya kwamba aache kwanza ili ndio aje akufuate (who knows kama bado utakuwepo.., alafu huoni kwamba atakuwa amekufunga kwamba nimeacha wangu hivyo huna budi kunikubali.., lawama ni palepale)
Hivi watu huwa wanalaumu sababu hawakusema, au sababu walipatana kwamba if A, B au C basi usiniliaumu., wakati mapenzi yapo hot mabaya yote uonekana mazuri na mapenzi yakichuja hata mazuri uonekana mabaya (binadamu hakosi sababu).Naaahhhh. . .Hii haiwezi kuwa na lawama kwasababu unamwambia kabisa asimuache huyo mwenzie kwasababu yako. . .na kumwacha kwake sio guarantee ya kuwa utampokea na ndio haswa maana ya "usimuache kwaajili yangu" inapoingia.
Sio kwa ajili yako tu ni kwa ajili yake pia sababu alikupenda na ulikidhi haja zake za wakati huo, at that particular moment kila mtu alikuwa ana-enjoy na unless ulimpa ultimatum kwamba kamwache mke wako, hakuna wa kulaumu bali yeye mwenyewe.Duh lizy hi kitu imesumbua sana kichwa changu naona kama unanisema mimi... mtu kamuacha mwenzake kwa ajili yangu..
Maisha hayana guarantee, hata ukifanya yote sawa huenda kesho ukaacha au kuachwa.., kwahio cha maana ni kuangalia mtu unayeingia nae kwenye mahusiano ni wa aina gani.., and don't let hofu za kesho itakuwaje sikuharibie leowasiwasi wangu ni kwamba hata mimi ipo siku ntaachwa kwa kwa ajili ya mtu mwingine..
Akufukuzae hakwambii toka..,(kama unaona anafanya hivyo kwa kukukomoa basi hana busara) ila kama wanashare watoto na familia na mwenza wake sio busara kumkataza mwenza wako asiongee na mzazi mwenzake so long as wanaongea issue za watotombaya zaidi ananiambia bado wana wasiliana,nimeshindwa hata kumshangaa
Duh lizy hi kitu imesumbua sana kichwa changu naona kama unanisema mimi... mtu kamuacha mwenzake kwa ajili yangu..wasiwasi wangu ni kwamba hata mimi ipo siku ntaachwa kwa kwa ajili ya mtu mwingine..mbaya zaidi ananiambia bado wana wasiliana,nimeshindwa hata kumshangaa
Hahahahaha. . . I guess hamna haja Konnie. After all. . .Hata ukimkuta hana(alishamwacha) bado anaweza akawa nao baadae akitaka.Mahusiano ni pasua kichwa.
Si kila ukimwacha A kwa ajili ya B, basi utamwacha B kwa ajili ya C.
Inawezekana mahusiano kati yangu na A yapo yapo tu for the sake ya uvumilivu na ile kusema nitaacha wangapi.
Akijitokeza B ambaye ni candidate mzuri zaidi, why not? Naweka mambo wazi na nina move haraka tu kwa B.
Maisha ni mafupi mno kujinywesha klorokwin kila siku lol
kibaya zaidi katika interaction zenu unagundua tayari kila mmoja ana hisia na mwenzake ila tatizo ni mahusiano ya awali mliyonayo.
Tatizo ni nani achukue uamuzi wa kuvunja uhusiano wake kwa ajili ya mwenzake,
Issue ya kuichwa ipo regardless mtu umempata vipi.., nadhani cha maana hapa ni wale ambao wameachwa kama bado wanapenda wanakuwa wanapata maumivu bila hatia, (furaha zenu zinasababisha maumivu)ndo hizo hofu za ikiwa alimwacha je na mimi c ataniacha akipata mwingine nk, na wanaoumia zaidi ni wale walioko kwenye ndoa na mara nyingine hawa wanaopendana huishia kucheat.
Mimi ningependa katika katiba mpya sheria ya ndoa iboreshwe kuwa na ndoa za mikataba ya muda, siyo mpaka kifo kitenganishe.
Doto usiwe na wasiwasi bana. . .
Inawezekana hisia zilishaisha huko zamani, sema tu alikua hajapata msukumo. Kinachoweza kusababisha mahusiano yadumu mara nyingi ni hisia za wahusika na sio yalipoanzia. Kuna walioanza kwa kucheat, wakaishia kuona na mahusiano yao hayana kashkash kwasababu kweli walikutana waliotakana, japo muda mbaya kidogo.