Habari Mlenge .Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita mwaka mmoja uliopita kutoka sasa ,nilisoma mchapuo wa sayansi yaani PCB,nilichaguliwa kujiunga na chuo kikuu kimoja hapa nchini ila kozi ya IT degree,ila haikuwa ndoto yangu,kwani ndoto yangu ilikuwa ni udaktari.Niliamua kufanya application ya diploma ili kupata nafasi ya udaktari dip kuepuka competition ,nimechaguliwa ilakwa bahati mbaya aliyekuwa ananisomesha alifariki dunia,huku ikiwa gharama za hiyo kozi ni kubwa na hakuna any sponsorship.Na chuo tarehe 15/10/2016 kinafungua .Nianzaje kwa hili
Hongera kwa kuchaguliwa kozi ya Diploma. Pole kwa kufiwa.
Pa kuanzia ni kuamini kwamba
with persistence, utaweza kuendelea na masomo yako.
- Changanua ni gharama zipi zinazohitajika ili uweze kuanza masomo yako.
- Changanua gharama za ujumla za kukamilisha elimu yako.
- Katika hizo gharama zote, wewe unaweza kuchangia asilimia ngapi?
Ukianzia na kiasi fulani unachoweza kuchangia, na ukijua jumla ya gharama, unaweza kuwa na mkakati wa kutafuta namna ya kuzipata.
Findology 101 inadai uanzie kutafuta pale ulipo. Je, una mali yoyote unayoweza kuibadilisha iwe hela za kukuwezesha kusoma? Njia yoyote nyingine mbadala?
Mahali pa kuanzia baada ya hapo ni kwenye chuo unachotaka kwenda kusoma. Wana skolashipu yoyote? Je, wanakubali kulipwa ada kwa mikupuo mingi, ili kusaidia wale wasio na uwezo? Wana
waiver ya ada?
Discount? Baadhi ya vyuo vinatoa punguzo la ada kwa wanafamilia wa wafanyakazi. Huna mzazi au mlezi kwenye chuo hicho?
Umeenda Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto? Hapo utaweza kuambiwa njia mbadala zinazoweza kukufaa katika lengo lako. Jaribu kuulizia miradi mbalimbali iliyoko au fursa ambazo zitaweza kuenda na lengo lako.
Asasi zisizo za Kiserikali zenye malengo anuai ambayo yanasharibiana na wewe kupata diploma ya
Clinical Officer. Uko radhi kwenda kufanya kazi vijijini kusiko na madaktari baada ya kuhitimu. Wakikusomesha wewe watakuwa wanasaidia kupunguza vifo na magonjwa ya mama na mtoto, kwa vile utaenda kijijini kwenye zahanati zenye majengo bila matabibu. Kutasaidia kuimarisha huduma za afya ya uzazi na watoto kwa vile kule kijijiini utakakoenda hakuna huduma rasmi za ukunga. Kutaimarisha afya ya jamii, hasa kwa makundi yaliyoko kwenye mazingira ya hatari kwa vile utaweza kuwafikia na kutoa uelimishaji-umma kwa makundi hayo yasiyofikiwa vijijini; kutaboresha mazingira kwa kuwa na watu wenye afya bora.
Jaribu kuwasiliana na asasi hizo, japo zenyewe siyo 'scholarship-granting organizations', lakini pengine zinaweza kuwa na fursa ya kukuunga mkono katika kusoma utabibu ili malengo hayo hapo juu yatimizwe.
Mf.,
Tanzania : EngenderHealth
Tanzania | Jhpiego
http://sawatanzania.org/
Nenda kwa watafiti mbalimbali wa afya, ambao wataweza kukutumia kama
field-assistant. Eg., NIMR Tanzania
Fika kwenye halmashauri yako ya wilaya/mji/jiji. Ulizia fursa zilizopo zinazoweza kutumika kukamilisha elimu yako.
Waone sekta binafsi pia, ukiahidi na kuingia makubaliano ya ajira ya muda fulani baada ya kuhitimu au wakati wa
fieldwork.
Waone wafadhili mbalimbali wengine walioko Tanzania, kama vile,
https://vodacom.co.tz/foundation/projecta/improving_health/healthy_motherhood ,
Asante Africa Foundation | A US Charity to Educate Children in Tanzania and Kenya - Asante Africa Foundation
FCS inspire formation of Tanzania philanthropy forum to serve the vulnerable
MO Dewji Foundation
Of course, tumia
scatter-gun approach. Tuma maombi kamilifu sehemu nyingi. Kwa mujibu wa
Pareto Principle, lazima utapata walau kutoka sehemu moja kwa kila
application tano.
Bottom line: Kwa nini wakusomeshe
wewe na siyo mtu mwingine? Ndoto za kuwa daktari ni sababu ambayo haina mashiko. Wewe kusomeshwa kutasaidia vipi jamii,
on the short-term, na kutafikisha vipi malengo ya kusaidia jamii, aliyonayo mwenye kushikilia pochi?
Mbadala mwingine ni kutumia skills ulizonazo kujitengenezea kipato kwa kutumia Intaneti. Zipo njia nyingi, ila kwa kuanzia nakupatia linki hizi:
40 easy ways to make money quickly (Soma komenti!);
5 Real Ways to Actually Make Money Online
50 Legitimate Ways to Make Money from Home in 2016
All the best!